Sababu gani zilifanya Jay Jay Okocha asitwae Ballon D' or enzi zake?

Sababu gani zilifanya Jay Jay Okocha asitwae Ballon D' or enzi zake?

Ni Kama aThierry Henry, alikuwa Mkali kipindi cha wakali wengi sio Kama Siku hizi Messi na Ronaldo zaid ya Miaka 10

Mechi ya Mtoano World CUP 1998 Nigeria vs Denmark Jay Jay alionesha ufundi wa Karne lakin Mwishowe wakalazwa 4-1, naikumbuka sana hii Mechi Kama Jana vile
hii mechi huwa naicheza akilini kwa dk zote 90+, hainitoki kamwe
 
Okocha hakua na mchango kwa timu zake Kubeba ubingwa ukiondoa Nigeria;na wakati Okocha yupo kwenye peak kulikua na mafund wengi sana Weah,Ronaldo de Lima,Dinho,Rivaldo,Mendieta,Riquelme nk
 
1998 hakuchukua, Alichukua mtu mmoja wa kuitwa Victor Ikpeba, Wa pili ndo akawa Okocha, wa tatu akawa Sunday Oliseh. Get your facts right.

Inshort Austin Jayjay Okocha hana tuzo ya mchezaji bora wa africa kwa miaka yote aliyokuwa mchezaji mpira.

Inauma sana kuona mpira haujamtendea haki kama yeye alivyoutendea haki. Kwa mchezaji kama Okocha kukosa tuzo ya mchezaji bora wa Africa inaonesha ni namna gani unaweza usivune ulichopanda.
mkuu complex masahihisho kidogo, nadhani 98 alichukua mustafa hadji Fundi mmorocco yule jezi #7 mgongoni akifuatiwa na kama ulivotaja.

Victor Ikpeba jezi #20 mgongoni alichukua 97 akifuatiwa na N'Doram halafu Taribo West jezi #5
 
Ni sawa, niliangalia vibaya mtiririko. Ila yote kwa yote, Okocha hana hii tuzo.
 
Alikuwa na kipaj lkn alikuwa anapenda kucheza na jukwaa 'show game' na sio matokeo na ndo mana hata timu nying za ulaya hazijamuangalia.
 
Alikuwa na kipaj lkn alikuwa anapenda kucheza na jukwaa 'show game' na sio matokeo na ndo mana hata timu nying za ulaya hazijamuangalia.
basi tu haikutokea ila alikua finest player. mfano AFCON ya 04 alikua mfungaji bora plus MVP na pia at the same time alikua kati ya waafrika watano katika kikosi cha FIFA100.
 
Pa1 mkuu..

Kweli tupo pamoja kwenye huu uzi, sema nimeamua kuachana na huu mjadala kwa sababu kila mtu ana mtazamo wake hivyo ni busara kila mtu kubaki na msimamo wake,

Tena vitu vya ajabu kabisa yaani Gaucho awe sawa na Okocha?
 
Kabla ya yote nambie kwann hakuchezea timu kubwa?
Mfano madrid, barcelona, manchester, inter, ac milan au juve?
Badala yake akachezea bolton na nyenginezo, hata psg aliyochezea kipindi hicho haikuwa timu kubwa
Tuanzie hapo kwanza
 
Back
Top Bottom