Mimi ni mmoja wa wenye jicho hilo la maono na si mtu wakuishia kuangalia tuu Muziki wetu unapopotelea.
Sina chakupunguza kwenye andiko lako zaidi nitalijazia nyama kwa uelewa wangu.
Kwanza Tuelewe Tuna Mashabiki wa Wanamuziki wa Muziki na Si Wapenzi wa Muziki wa wanamuziki.
TATIZO LINAANZIA HAPA.
Media za Bongo zina vitengo vyakukagua Muziki kabla ya kwenda hewani. Vigezo na Masharti wayakaguayo ni yao wenyewe na msanii hutakaa ujue wala kuelewa zaidi ya upeleke track yako kitengo ujue kama itapitishwa au la.
vigezo hivi ni kwa mwanamuziki wa tanzania anayefanyia kazi zake Tanzania tuu.
TATIZO LA PILI NI MATOKEO YA TATIZO LA KWANZA.
Tasnia ya burudani hasa muziki wameachiwa kwa njia zisizo rasmi watu wasiokua na lakuusaidia kwa nyanja yoyote ile ya kisheria, kibiashara, na kiheshima.
Hapo tunaona media ndio zinazohodhi burudani, hivyo mwaka mzima au miaka kafhaa tutakua na wasanii walewale wakifanya muziki uleule na kwasababu waliotofauti nao hawapati nafasi tutaendelea kuamini tupo ktk ubora ila ukitoka nje ya mpaka unaona aibu kuelezea muziki kama muziki wenye sura ya kimataifa.
TATIZO LA TATU CHANZO NI HTATIZO LA PILI.
Kutokana na baadhi ya wasanii kuwa na uhakika wakupata japo showz, interviews na promo za hapa na pale kutokana na wao kuwa katika kundi mojawapo la walijipa udau, huwa wanajisahau nakuamini level ya jina na umaarufu anaoupata unatokana na ubora wa kazi yake kumbe ni ubora wa mfadhili wake
na hapo ndipo Mleta uzi anapotustua tunapoenda ni kwenda kuuzika mziki Bora na tukaendelea kubaki na Bora muziki.
TATIZO LA NNE CHANZO NI YOTE NILIYOYAORODHESHA.
Huyu ni shabiki wa muziki wa kizazi hiki cha sasa hivi, na wapo wengi kweli.
Kutokana na kuboronga tangu mwanzo, shabiki anavyokuja kukutana na Muziki inakua ni huo huo ulioamuliwa akutane nao. Wachache kama mimi na mleta Uzi tunasafiri sana kihisia kupitia wanamuziki wengine ndani na nje ya nchi kiasi tunapata uwezo wakulinganisha au kutofautisha namna muziki wetu unavyobamba.
Iko hivi duniani kwenye mita100 anayeshikilia revord ni mjamaica ila katika kila nchi kuna no 1 wa mbio hizo. Let say wa nvhi yetu atumie dk2 mita 100 na katika kundi lakina Hussein Bolt mshindi wa mwisho awe ametumia dk1, bado wetu kwenye mbio hizo ni wa kwanza ila duniani hata kwenye kumi bora hayupo.
Hapa namaanisha tuna wanamuziki wazuri na Bora kwa hapa kwetu tuu ila nje ya nvhi ni maundergtound ambao hata show za BSS huko mbele hawatapata hata nafasi yakuonekana kutokana nakutolewa ktk round za mwanzo kabisa.
Kitu hiko mashabiki hawakijui na wengi ni watu wakusubiria media zinawaambia wimbo mzuri ni upi na upi basi wao hawana machaguzi mengine na ni wengi wao.
KIPI KIFANYIKE KWA MUZIKI WETU UKUE NA UWE BORA NDANI NA NJE YA NCHI?
Kwanza kabisa Serikali kama serikali ndio kitu cha kwanza chakuweka haya mambo katika ubora, utaalamu ili faida za kimaisha na uchumi zikapatikane kupitia Tasnia Hii.
Iko hivi ndugu zangu, kwanza niweke interest zangu, mimi ni muandaaji na mwanamuziki chipukizi katika tasnia hii. Kwa uzoefu wangu wa zaidi ya miaka 10 katka shughuri hizo kuna mengi nimeweza kuyajua ni moja ya sababu muziki wetu kuwa hapa ulipo leo.
Bongo hata ukiwa maharufu na kazi zako zipo kwenye Peak, suala la wewe kupata hela bado litabakia kwa watu wanaoweza kuamaua upate au usipate.
Wasanii wengi hawaishi makwao yaani kwake kwasababu gharama za maisha haziwezi kuwa covered na kazi yake ya muziki. Hivyo kupanga kwa walio wengi ni Issue na naweza kusema %70 ya wasanii wenye majina makubwa bongo wanaishi kwakuungaunga ili mradi kesho ifike.
Natukitaka kujua kuna tagizo kubwa leo hii tasnia yetu ina watu wazima wachache sana yaani mtu namke na watoto waishi kwakutegemea muziki. Nwanamuziki akiwa na familia tuu inabidi atafute issue.
Ok Serikali itasaidiaje sasa,
Kwanza kuweka sera za kumlinda msanii kisheria na kibiashara. Kuyalinda mazingira ya kazi zake nakuweka utaratibu halali na wa wazi
Kumlinda vipi sasa?
Kisheria ni kuhakikisha haki zake zote zakisheria anakua nazo.
Na kibiashara nikuhakikisha kile kinachoingia kupitia yeye na yeye amepata.
Mazingira yake yatalindwa kwa kurathimisha biashara ya studio za kurekodia ziwe kama studio za TV na Redio ili pawe na Ada kwa kila studio itakayozalisha muziki. Kwakufanya hivi gharama za kurekodia muziki zitarudi na zitakua kubwa kiasi myu mmoja mmoja kuzimudu anaweza asiweze isipokua mpaka achangiwe au alipiwe na sidhani kama kuna mchango au malipo yakumlipia mgu shilingi milioni 3 akaimbe chura anarukaruka.
Kurekodi siku hizi sio gharama hata mashindano ya mshindi ataenda kurekodi imebidi yafe. Ukirekodi kama dj wa redio au mtangazaji anakujua ngoma itachezwa tuu tena na inaweza isipite kwenye vitengo vyao vyakinyonyaji.
Kwahiyo kama haya yanafanyika serikali ikiweka utaratibu mzuri kuanzia mikataba nadhani nayonitapata kodi halali na kuijua biashara inaendaje, kwa mfano mgu anakuambia gharama za bideo ni siri ya management, serikali inavhukua kodi shing ngapi kutoka kwa mtenenezaji? Kwahiyo ipite sheria tuu mikataba ya tasnia ya burudani haitakiwi kuwa siri.
Wadhamini wanatoa hela nyingi kwenye vipindi vya burudani lakini wasanii wanaoweka burudani hizo hawapati kitu, kwahiyo ligoje tamko tuu kwa kila anayeweza kuingia katika chati za muzizki media hoyote ile ale % kadhaa za mdhamini wa kipindim hii italeta maana ya kuwa msanii flani anatrend, inamaana mpaka hela nazo zitatrend na yeye kuliko hivi sasa jina kubwa na bado watu wanalala njaa.
KAMA NINGELIKUA MIMI NI SERIKALI KWANZA NINGEANZIA STUDIOZ ZOTE NAZITOZA ADA KWA MWAKA SI CHINI YA MILIONI TANO MPAKA KUMI.
MEDIA ZIENDE NYIMBO ZITAKAZOTOKA KATIKA STUDIO ZINAZOTAMBULIKA KISHERIA.
SERIKALI IZITAMBUE TUU KAMPUNI ZINAZOSIMAMIA WASANII NA KUSAMBAZA KAZI ZAO NA SI IWE KWA MTU BINAFSI. KWAKUFANYA HIVI HAYA MAKAMPUNI YATAKUJA MTAANI KUTAFUTA WANAMUZIKI NA WATAHAKIKISHA WANAWAPATA WALE WALIO BORA TUU, HAPO MAANA YA MUSIC REBAL NA RECORDING REBAL ITAGFANYA KAZI MAANA NIKIONACHO SISI GUNA RECORDING REBAL NA SI MUSIC REBAL.
KWAHIYO HATA KAMA KUNA MEDIA ZITAWAMILIKI WASANII ZITABIDI ZIJITAMBULISHE KAMA MUSIC REBAL NA SI REDIO AU TV.
SERIKALI ILAZIMISHE UTARATIBU WAKUWA NA VIPINDI VYA AINA ZOTE ZA MUZIKI UNAOPATIKANA NA KUTAMBULIKA NCHINI, ILI WASANII WAWEZE KUGAWANA CHAKUBURUDISHA.
Bado nipo ngoja nisome kwanza ya wenzangu nisiwachoshe sana.