Hata bongo movie wakati wa Kanumba hizi mboyoyo zilikuwepo, hata hao waigizaji wakawa wanasema waneshaipiku Nollywood π€£π€£Kichwa cha habari ndio kinabeba ujumbe wote kwenye thread, au sio? Nyingine zote ni mboyoyo tu. Mimi nakataa kwamba Bongo Fleva imefeli. Imepiga hatua kubwa sana kwenye kila idara. Zamani kulikuwa na watu kibao hawakuwa na vipaji waliingia studio lakini tukasikiliza takataka zao. Siku hizi muziki ni kazi, kama sio fani yako lazima utakaa pembeni. Sitaki kuandika gazeti, lakini ukweli utabaki palepale, mleta mada hajui alikuwa anataka kusema nini
Perfect π―π―π― πππMimi ni mmoja wa wenye jicho hilo la maono na si mtu wakuishia kuangalia tuu Muziki wetu unapopotelea.
Sina chakupunguza kwenye andiko lako zaidi nitalijazia nyama kwa uelewa wangu.
Kwanza Tuelewe Tuna Mashabiki wa Wanamuziki wa Muziki na Si Wapenzi wa Muziki wa wanamuziki.
TATIZO LINAANZIA HAPA.
Media za Bongo zina vitengo vyakukagua Muziki kabla ya kwenda hewani. Vigezo na Masharti wayakaguayo ni yao wenyewe na msanii hutakaa ujue wala kuelewa zaidi ya upeleke track yako kitengo ujue kama itapitishwa au la.
vigezo hivi ni kwa mwanamuziki wa tanzania anayefanyia kazi zake Tanzania tuu.
TATIZO LA PILI NI MATOKEO YA TATIZO LA KWANZA.
Tasnia ya burudani hasa muziki wameachiwa kwa njia zisizo rasmi watu wasiokua na lakuusaidia kwa nyanja yoyote ile ya kisheria, kibiashara, na kiheshima.
Hapo tunaona media ndio zinazohodhi burudani, hivyo mwaka mzima au miaka kafhaa tutakua na wasanii walewale wakifanya muziki uleule na kwasababu waliotofauti nao hawapati nafasi tutaendelea kuamini tupo ktk ubora ila ukitoka nje ya mpaka unaona aibu kuelezea muziki kama muziki wenye sura ya kimataifa.
TATIZO LA TATU CHANZO NI HTATIZO LA PILI.
Kutokana na baadhi ya wasanii kuwa na uhakika wakupata japo showz, interviews na promo za hapa na pale kutokana na wao kuwa katika kundi mojawapo la walijipa udau, huwa wanajisahau nakuamini level ya jina na umaarufu anaoupata unatokana na ubora wa kazi yake kumbe ni ubora wa mfadhili wake
na hapo ndipo Mleta uzi anapotustua tunapoenda ni kwenda kuuzika mziki Bora na tukaendelea kubaki na Bora muziki.
TATIZO LA NNE CHANZO NI YOTE NILIYOYAORODHESHA.
Huyu ni shabiki wa muziki wa kizazi hiki cha sasa hivi, na wapo wengi kweli.
Kutokana na kuboronga tangu mwanzo, shabiki anavyokuja kukutana na Muziki inakua ni huo huo ulioamuliwa akutane nao. Wachache kama mimi na mleta Uzi tunasafiri sana kihisia kupitia wanamuziki wengine ndani na nje ya nchi kiasi tunapata uwezo wakulinganisha au kutofautisha namna muziki wetu unavyobamba.
Iko hivi duniani kwenye mita100 anayeshikilia revord ni mjamaica ila katika kila nchi kuna no 1 wa mbio hizo. Let say wa nvhi yetu atumie dk2 mita 100 na katika kundi lakina Hussein Bolt mshindi wa mwisho awe ametumia dk1, bado wetu kwenye mbio hizo ni wa kwanza ila duniani hata kwenye kumi bora hayupo.
Hapa namaanisha tuna wanamuziki wazuri na Bora kwa hapa kwetu tuu ila nje ya nvhi ni maundergtound ambao hata show za BSS huko mbele hawatapata hata nafasi yakuonekana kutokana nakutolewa ktk round za mwanzo kabisa.
Kitu hiko mashabiki hawakijui na wengi ni watu wakusubiria media zinawaambia wimbo mzuri ni upi na upi basi wao hawana machaguzi mengine na ni wengi wao.
KIPI KIFANYIKE KWA MUZIKI WETU UKUE NA UWE BORA NDANI NA NJE YA NCHI?
Kwanza kabisa Serikali kama serikali ndio kitu cha kwanza chakuweka haya mambo katika ubora, utaalamu ili faida za kimaisha na uchumi zikapatikane kupitia Tasnia Hii.
Iko hivi ndugu zangu, kwanza niweke interest zangu, mimi ni muandaaji na mwanamuziki chipukizi katika tasnia hii. Kwa uzoefu wangu wa zaidi ya miaka 10 katka shughuri hizo kuna mengi nimeweza kuyajua ni moja ya sababu muziki wetu kuwa hapa ulipo leo.
Bongo hata ukiwa maharufu na kazi zako zipo kwenye Peak, suala la wewe kupata hela bado litabakia kwa watu wanaoweza kuamaua upate au usipate.
Wasanii wengi hawaishi makwao yaani kwake kwasababu gharama za maisha haziwezi kuwa covered na kazi yake ya muziki. Hivyo kupanga kwa walio wengi ni Issue na naweza kusema %70 ya wasanii wenye majina makubwa bongo wanaishi kwakuungaunga ili mradi kesho ifike.
Natukitaka kujua kuna tagizo kubwa leo hii tasnia yetu ina watu wazima wachache sana yaani mtu namke na watoto waishi kwakutegemea muziki. Nwanamuziki akiwa na familia tuu inabidi atafute issue.
Ok Serikali itasaidiaje sasa,
Kwanza kuweka sera za kumlinda msanii kisheria na kibiashara. Kuyalinda mazingira ya kazi zake nakuweka utaratibu halali na wa wazi
Kumlinda vipi sasa?
Kisheria ni kuhakikisha haki zake zote zakisheria anakua nazo.
Na kibiashara nikuhakikisha kile kinachoingia kupitia yeye na yeye amepata.
Mazingira yake yatalindwa kwa kurathimisha biashara ya studio za kurekodia ziwe kama studio za TV na Redio ili pawe na Ada kwa kila studio itakayozalisha muziki. Kwakufanya hivi gharama za kurekodia muziki zitarudi na zitakua kubwa kiasi myu mmoja mmoja kuzimudu anaweza asiweze isipokua mpaka achangiwe au alipiwe na sidhani kama kuna mchango au malipo yakumlipia mgu shilingi milioni 3 akaimbe chura anarukaruka.
Kurekodi siku hizi sio gharama hata mashindano ya mshindi ataenda kurekodi imebidi yafe. Ukirekodi kama dj wa redio au mtangazaji anakujua ngoma itachezwa tuu tena na inaweza isipite kwenye vitengo vyao vyakinyonyaji.
Kwahiyo kama haya yanafanyika serikali ikiweka utaratibu mzuri kuanzia mikataba nadhani nayonitapata kodi halali na kuijua biashara inaendaje, kwa mfano mgu anakuambia gharama za bideo ni siri ya management, serikali inavhukua kodi shing ngapi kutoka kwa mtenenezaji? Kwahiyo ipite sheria tuu mikataba ya tasnia ya burudani haitakiwi kuwa siri.
Wadhamini wanatoa hela nyingi kwenye vipindi vya burudani lakini wasanii wanaoweka burudani hizo hawapati kitu, kwahiyo ligoje tamko tuu kwa kila anayeweza kuingia katika chati za muzizki media hoyote ile ale % kadhaa za mdhamini wa kipindim hii italeta maana ya kuwa msanii flani anatrend, inamaana mpaka hela nazo zitatrend na yeye kuliko hivi sasa jina kubwa na bado watu wanalala njaa.
KAMA NINGELIKUA MIMI NI SERIKALI KWANZA NINGEANZIA STUDIOZ ZOTE NAZITOZA ADA KWA MWAKA SI CHINI YA MILIONI TANO MPAKA KUMI.
MEDIA ZIENDE NYIMBO ZITAKAZOTOKA KATIKA STUDIO ZINAZOTAMBULIKA KISHERIA.
SERIKALI IZITAMBUE TUU KAMPUNI ZINAZOSIMAMIA WASANII NA KUSAMBAZA KAZI ZAO NA SI IWE KWA MTU BINAFSI. KWAKUFANYA HIVI HAYA MAKAMPUNI YATAKUJA MTAANI KUTAFUTA WANAMUZIKI NA WATAHAKIKISHA WANAWAPATA WALE WALIO BORA TUU, HAPO MAANA YA MUSIC REBAL NA RECORDING REBAL ITAGFANYA KAZI MAANA NIKIONACHO SISI GUNA RECORDING REBAL NA SI MUSIC REBAL.
KWAHIYO HATA KAMA KUNA MEDIA ZITAWAMILIKI WASANII ZITABIDI ZIJITAMBULISHE KAMA MUSIC REBAL NA SI REDIO AU TV.
SERIKALI ILAZIMISHE UTARATIBU WAKUWA NA VIPINDI VYA AINA ZOTE ZA MUZIKI UNAOPATIKANA NA KUTAMBULIKA NCHINI, ILI WASANII WAWEZE KUGAWANA CHAKUBURUDISHA.
Bado nipo ngoja nisome kwanza ya wenzangu nisiwachoshe sana.
Mkuu deal nyingi za wasanii unazoziona kuna watu wa kati ambao hula zaidi yako. Na kama hutaki hawakupi, anatafutwa mwingine.Mwaka 2015 alisaini Deal nono kuwa Balozi wa kampuni ya SAMSUNG kwa Tanzania.
Vanessa kasaini deals na Universal Music Africa kala Mamilioni ambayo wengine tutaishia kuyaota tu maishani.
Afu leo analalamikia Mziki. Hapana bana atuache!
Yeye mwenyewe baada ya kusaini alituambia amekubali sababu ni pesa ndefu amelipwa.
Hizi Label kubwa Sony na Universal zina matawi na ukisaini Sony Music Africa au Universal Music Africa.
Basi watakusimamia kazi zako Africa. ila kutusua Uingereza na Marekani kwenye Charts kubwa za Music za UK Top 40 au Billboard100 hilo sahauuuu.
Labda kama umesainiwa Sony UK, Sony America au Universal UK au Universal America. Hapo ndo unaweza angalauuuu ukikaza unaweza tokea kwenye Charts Kubwa znazoheshimika kama UK TOP 40, AMERICAN TOP 40 na BILLBOARD 100.
Na wimbo wako ukiwa Humo maana yake Umebamba UK na America.
Wasanii wetu weeeengi wanalia na Sony na Universal sababu wao wasanii wa Tanzania walidhani wakishasaini tu baaaaasi watakuwa nyimbo zao zipo UK TOP 40 au Billboard 100 kitu ambacho sio kweli.
Mziki wa Tanzania bado mchanga (infant) kwenye level za Kimataifa.
Ndo maana hukuti Nyimbo za Wabongo kwenye Charts kubwa za Kidunia kama Billboard 100.
Dada yetu Vanessa inavyoonekana baada ya kusaini tu alijua tayari atakuwa Levels za akina Ariana Grande, Miley Cyrus, Rihanna, Rita Ora, Selena Gomez, Meghan Trainor, SZA, Sia, Taylor Swift etc... kitu ambacho ndo kimemfanya ajione kama muziki haujamlipa sababu mategemeo yake hajayafikia.
ila katika Level za KibongoBongo na Africa Vanessa akubali tu kuwa Mziki umemlipa. Labda over-spending na shows-off ndo probably zmemgharimu kifedha.
Biashara haziendi hivyo.
Ni udhaifu tu wa nchi zetu ndio maana, taasisi zinazotakiwa kusimamua ushindani kama FCC zipo zipo tu.
Ukiacha monopoly lazima tu consumers wapate low quality products.
Ndio maana hata uwanjani kuna marefa ili kuhakikisha usawa, na hivyo burudani kwa watazamaji.
Hata mimi najua muziki ni biashara ndio maana sijasema mtu asaidiwe, ninachosema katika mazingira kama hayo hata hao wanaomilikiwa na hizo na kukuzwa sana siku wakipigwa chini ndio utajua u ubunifu wao wote na kazi havikuwahi kuwasaidia.
Kwamba dunia nzima media ndio zinazomiliki wasanii, studio, kuandaa matamasha na hao hao ndio promoters kiasi kwamba wasanii wasiokuwa kundi lolote wakiwemo wachanga hawapati nafasi ?Hata USA pako hivo. Bila Label hutusui... Na ukipigwa chini na Label basi una khaki mbaya hata USA pia.
Muziki wa mainstream upon hivo Dunia nzima.
Bongo hapa Media ndo zinafanya kazi kama mapromota (kupromote music) bila Media mziki utasua sua kufika mbali (nation wide).Kwamba dunia nzima media ndio zinazomiliki wasanii, studio, kuandaa matamasha na hao hao ndio promoters kiasi kwamba wasanii wasiokuwa kundi lolote wakiwemo wachanga hawapati nafasi ?
Juma Nature ni overated.Mkuu si wote wamefanikiwa, lakini mtu kama Diamond huwezi sema hajafanikiwa.
Hata kama waliofanikiwa ni wachache lakini huwezi fananisha na zamani.
Mtu kama Juma nature angekuwepo enzi hizi nadhani angekuwa zaidi ya diamond.
Kusaga master minder..Babu Tale anaweza niniPongezi kubwa kwa Diamond platnumz simbaaa, mwamba pekee aliyeweza kusimama mwenyewe na kusimamisha wasanii wake na label yake kuwa moja ya label kubwa hapa Afrika bila pamoja na vita kubwa aliyopigwa na media zote kubwa za burudani nchini ila wameshindwa badala yake wanaanza kuitumia silaha aliyetengeneza mwenyewe.
Anyways,lete ushahidi unaoonyesha prime time promotion ni waandaaji wa wasafi festival.
He is just a puppets,But inawezekana kwasababu Wasafi media mostly kwa asilimia kubwa inamilikiwa na kusaga, diamond kupitia wasafi company ana hisa kiasi kidogo sana ingawa anatumika kama image ya brand but nyuma ya pazia he is just a puppets.
Kuna kikaratasi kutoka TCRA nilishakiona kikionyesha umiliki wa hisa katika Wasafi media diamond ana hisa ndogo sana ni kama 15% if not less....
Mkuu jitahidi uwe na valid infoBut inawezekana kwasababu Wasafi media mostly kwa asilimia kubwa inamilikiwa na kusaga, diamond kupitia wasafi company ana hisa kiasi kidogo sana ingawa anatumika kama image ya brand but nyuma ya pazia he is just a puppets.
Kuna kikaratasi kutoka TCRA nilishakiona kikionyesha umiliki wa hisa katika Wasafi media diamond ana hisa ndogo sana ni kama 15% if not less....
Kwa kipindi kile hakuwa overrated, alifanya vizuri sana mkuu hasa albam yake pendwa ya ugali, ingawa nyimbo karibu zote alimuimba sinta.Juma Nature ni overated.
Samson unatia aibu kushupalia mambo usiyoyajua kwa usahihi.Yeah ni la kusaga sababu ndie mwenye hisa kubwa wasafi media... Diamond is a plated owner not a true /total/complete owner.
Samason na ushambenga wake hutamuona tena akileta ushubwada wake hapa.Hiyo documents uliiona au ulisimuliwa? Kama ulisimuliwa basi hii ndio document yenyewe hebu tizama tena Nasib Abdul ana asilimia ngapi [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
View attachment 1575192
Kuna wasafi tv na wasafi media do you know the difference?!Hiyo documents uliiona au ulisimuliwa? Kama ulisimuliwa basi hii ndio document yenyewe hebu tizama tena Nasib Abdul ana asilimia ngapi [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
View attachment 1575192
Muziki huwa haunaga Formula, unaweza piga sana mistari konzi na hata usitusue wala nini..Juma Nature ni overated.
Wasafi Tv na Wasafi media ,mbona kitu kile kile sawa sawa kusema mamba na reptilia kwani wasafi TV ipo ndani ya Wasafi Media ambayo ndani yake unapata na radio.Kuna wasafi tv na wasafi media do you know the difference?!
Deals na Endorsement zinatafutwa pia ujue. Usizani unakaa tu kisa wee msanii mkubwa basi zitakufata.ππ Zitafute nyingi kisha kula Percentage yako, Ni Ngumu sana kula hii Cake kwa 100% pekee yako hasa ukiwa msanii ambaye huna Loyal fanbase kubwa..Mkuu deal nyingi za wasanii unazoziona kuna watu wa kati ambao hula zaidi yako. Na kama hutaki hawakupi, anatafutwa mwingine.
Why hujiuluzi kwanini Harmonize kapata endorsement kibao kuliko Kiba ?
Kwanza kibiashara Tanzania bado hakuna ushindani huo mkuubwa kiasi kwanba mpaka makampuni yawe that aggressive kwenye marketing.
Hata wasipompa msanii endorsement biashara zao zinaenda, so huna cha kuwafanya hata wakikupa pesa kidogo
Daah umemuumbua Kuna wa2 humu wanaongea uongo sana,[emoji16][emoji16]Hiyo documents uliiona au ulisimuliwa? Kama ulisimuliwa basi hii ndio document yenyewe hebu tizama tena Nasib Abdul ana asilimia ngapi [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
View attachment 1575192
Ndio hivyo, Ila wenyewe wanamedia nyingi zenye nguvu tofaut na sisi unakuta Ni mbili tu, pia Kuna promoters wengiKwamba dunia nzima media ndio zinazomiliki wasanii, studio, kuandaa matamasha na hao hao ndio promoters kiasi kwamba wasanii wasiokuwa kundi lolote wakiwemo wachanga hawapati nafasi ?