Uchaguzi 2020 Sababu kuntu 5 za kwanini Rais Magufuli atashinda tena Uchaguzi huu

Uchaguzi 2020 Sababu kuntu 5 za kwanini Rais Magufuli atashinda tena Uchaguzi huu

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Na Bwanku M Bwanku

Dirisha la kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani limefunguliwa na tayali vyama mbalimbali vya siasa vimeanza kazi ya kupita maeneo mbalimbali ya wananchi kunadi sera na mipango yao ili wachaguliwe Oktoba 28

Kuelekea uchaguzi huu yako mambo ya kuyamulika kwa vyama vya siasa na wagombea wao na nafasi yao kwenye uchaguzi huu. Kwenye mijadala kuelekea uchaguzi huu, leo nakuletea sababu 5 zilizodadavuliwa kwa undani za kueleza kwanini mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli atashinda kwa kishindo na kutetea tena kiti chake cha Urais Uchaguzi Mkuu huu

Moja; Kitendo cha Vyama vya Upinzani kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hili ni moja ya kosa kubwa sana ambalo vyama vya upinzani vilifanya, kosa ambalo litaendelea kuwatafuna sana kwa miaka mitano mpaka 2024 huku kosa hilo likimpa nafasi Rais Magufuli kutetea kiti chake kwa awamu ya pili kwa kishindo sana.

Kususia kwa uchaguzi kwa vyama vya upinzani kunawanyima nafasi vyama vyote vya upinzani kukosa wawakilishi wao hasa wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji ambao wangewasaidia sana kuwaombea kura vyama hivyo kwenye ngazi za chini kabisa za wananchi kule vijijini. Leo vyama vya upinzani kwa makosa yao ya kujitoa kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa wanaenda kwenye uchaguzi huu wakiwa kama yatima wasio hata na baba na mama wanaoweza kuwapokea watapoenda mitaani kuomba kura.

Fikilia leo Lissu, Membe au Lipumba akienda kijijini nani ataandaa hata sehemu ya kufanyia mkutano na kuwatafutia kura? Hii inampa nafasi Rais Magufuli kumaliza kazi mapema sana mana tayali ana wawakilishi wengi sana ngazi za chini wanaoweza kufanya kazi hizo kwa ufasaha sana.

Mbili; mtaji mkubwa wa wanachama wa Chama cha mapinduzi; CCM ni moja ya vyama vyenye mtaji mkubwa sana wa wanachama ukilinganisha na vyama vya upinzani. Kwa mujibu wa Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM- Taifa Humphrey Polepole chama hiko kina zaidi ya wanachama million 14 waliojiandikisha na waliopo kwenye database ya Chama nchi nzima. Hapo unazungumzia idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kwenye daftali la wapiga kura kuwa million 29 tu.

Kimahesabu ukitoa wale ambao hawatapiga kura na ambao kwa namna CCM inavyopiga kampeni ni dhahili Rais Magufuli atashinda mapema sana. Mtaji huu unampa Rais Magufuli kutafuta kura nje ya CCM akiwa tayali ana mtaji mkubwa wa wanachama ndani ya Chama ambao hawafikiwi hata robo na wanachama wa vyama vya upinzani.

Tatu; kuvunjika kwa UKAWA. Ukawa kama umoja wa vyama vya upinzani ulioungana mwaka 2015 na kumsimamisha mgombea mmoja tu wa Urais kwa kiasi kikubwa sana ulisaidia sana vyama vya upinzani kuihangaisha CCM kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana kura zote za upinzani zilienda kwa mgombea mmoja tu wa upinzani ambae alikuwa ni Lowassa. Hapo unazungumza vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR na NLD ambavyo viliungana.

Kuvunjika kwa umoja huo wa upinzani unaufanya upinzani karibu kila chama kusimamisha mgombea wake hali inayowafanya wapinzani kugawanyika sana kwa makundi ya kugawana kura zaidi ya makundi 10. Kwa mazingira haya upinzani utagawana sana kura na hivyo kumfanya mgombea pekee wa CCM kukusanya kura kama mchele mbele ya kuku.

Nne; kufanyiwa kazi kwa ajenda mama za upinzani na zilizowaumiza sana Watanzania. Moja ya ajenda zilizowapa nguvu kubwa sana na kuufanya upinzani kunawili sana mwaka 2010 mpaka 2015 ilikuwa ni ajenda ya ufisadi. Mpaka mwaka 2015 hoja hiyo ilikuwa ndio mama na kwa kiwango kikubwa ndio iliwatambulisha sana wapinzani. Hata ukija kwa Watanzania kwa kiwango kikubwa sana walikuwa wameielewa hoja ya upinzani kwani wananchi walichoka sana kusikia stori za ufisadi Serikalini na kwenye ofisi za imma zilizowafanya Watanzania kuendelea kudidimia kwenye umaskini.

Hoja hii kwa kiwango kikubwa sana imefanyiwa kazi na Rais Magufuli kwa kuanzisha mahakama ya mafisadi ambayo ilikuwa ikipigiwa kelele sana na wapinzani. Zaidi Rais Magufuli ameshughulika na ufisadi kiwango kinachoonekana na wananchi ikiwemo tumbuatumbua na kukamatwa kwa wahujumu uchumi. Hii imewapa imani sana wananchi na kuona hawana haja tena ya kuipigia kura upinzani wakati tayali mgombea Urais wa CCM kwenye awamu yake ya kwanza tu ameifanyia kazi kwa kiwango kikubwa sana ajenda hiyo iliyowaumiza Watanzania na kuwapa nafasi wapinzani.

Tano; ubabaishaji wa wagombea wengi wa upinzani. Mpaka sasa sera nyingi za wagombea wa vyama vya upinzani ni vichekesho tupu kwa Watanzania wa leo wanaotaka maendeleo baada ya kuchoshwa na kuyasubili kwa muda mrefu sana. Wakati Rais Magufuli akinadi Hapa Kazi Tu na kueleza namna atakavyoendeleza mapinduzi makubwa ya uchumi kwa awamu yake ya pili, upinzani wamejikita kwenye hoja zilizojaa utani, vichekesho na ubinafsi mkubwa.

Leo Chadema wanakwambia Ni yeye tu huku mgombea wao Lissu akitumia muda mwingi kuelezea tukio lake la kupigwa risasi kuliko atakavyotatua shida za wananchi. Mara ACT wakinadi Kazi na Bata, sera iliyojaa mzaha ndani yake huku wengine wakinadi sera ya kugawa ubwabwa kwenye kampeni zao.

Huu ni utani na ubabaishaji wa wazi wazi unaompa nafasi kubwa ya ushindi Rais Magufuli ambae yeye kwenye mikutano yake amekuwa akijikita kueleza namna atavyoongeza na kuboresha huduma za afya, uchumi na miundombinu wezeshi ya barabara na maendeleo

0657475347
 
Mbona umeacha sababu kuu ambayo katibu mkuu wako aliitaja kuwa ndio msingi wao wa ushindi?Alisema watatumia dola kubaki madarakani!Sasa wewe kapuku unapingana na katibu mkuu ambaye yuko jikoni kabisa?
 
Kujali na kuthamini makundi mbalimbali katika taifa letu hasa yaliyokuwa wamesahaulika mfano wachimbaji wadogowadogo kuwatengea maeneo na masoko ya uhakika.
#MitanoTena kwako Mh.
1599656384354.png
 
Kwa hali ilivyo mtoa maada yupo sahihi sana kwa asilimia [emoji817]% kwa sababu point zilizokuwa zinawapa Kiki Wapinzani karibia zote zimefanyiwa kazi lakini pia kukosekana kwa sera ambazo zinaweza kuwafanya watanzania kuweza kuwaelewa Wapinzani kunampa nafazi kubwa Mheshimiwa Rais Magufuli kuweza kupata kura nyingi sana za ushindi tarehe 28 October.

Lakini pia karibia Wapinzani wote kwa wakati huu wamekosa kabisa maada ya kuwaeleza watanzania na wengi wao hawana hata mwelekeo.

Lakini pia baadhi ya wabunge waliokuwa kwenye vyama pinzani kuhamia CCM pia kunampa point nyingi sana Rais Magufuli
 
Kwa hali ilivyo mtoa maada yupo sahihi sana kwa asilimia [emoji817]% kwa sababu point zilizokuwa zinawapa Kiki Wapinzani karibia zote zimefanyiwa kazi lakini pia kukosekana kwa sera ambazo zinaweza kuwafanya watanzania kuweza kuwaelewa Wapinzani kunampa nafazi kubwa Mheshimiwa Rais Magufuli kuweza kupata kura nyingi sana za ushindi tarehe 28 October.
Lakini pia karibia Wapinzani wote kwa wakati huu wamekosa kabisa maada ya kuwaeleza watanzania na wengi wao hawana hata mwelekeo.
Lakini pia baadhi ya wabunge waliokuwa kwenye vyama pinzani kuhamia CCM pia kunampa point nyingi sana Rais Magufuli
Hapa ni Kijiini na watu wamejaa kiasi hiki kwa hiyo ushindi asilimia [emoji817]
IMG-20200909-WA0184.jpg
 
6. Tume
7. Polisia
8. Mfumo utakao tumika kujumuisha matokeo
8...
9.......
 
Wenye uchungu na taifa hili wanaelewa hasa wale wanaoamini katika uchumi wa kujitegemea na kwenda na kauli moja kuwa TANZANIA ITAJENGWA NA WATANZANIA WENYEWE na sio kila jambo kutolea mfano wa mataifa fadhili
Nijibu swali langu!!! Sijaona jibu bado??
 
Hongera sana Mtoa Mada, Sababu ulizozitaja ni Dhahiri kwamba mwaka huu 2020 wapinzani wako kwenye wakati Mguu katika uchaguzi...
-Hawana hoja za Msingi, Wamegubikwa na Malalamiko na Matusi ambayo wananchi hawahitaji kusikia bali wanataka kusikia Unawasaidia kwa namna gani wao kujikwamua kiuchumi na Kubadili lifestyles zao
 
Back
Top Bottom