Madhaifu wote tunayo, hata wanaume wenye watoto Mbona huwa tunataka wake zetu wawapende hao watoto tuliozaa nje??
Lazima tukubali kuwa ukiacha na mambo ya kupasha kiporo Hakuna mtu asiyependa mwanaye apendwe.
Kila mtu anahitaji mtoto wake awe kwenye mikono Salama.
Pia tusishau tulikotoka.
Mama zetu walikuwa wanatulea wenyewe kipindi dingi anaondoka zaidi ya miezi 6 kwenda tanga huko Kwenye mkonge, wengine tabora, mtwara etc.
Kama wewe huko tayari kuishi na single mama, usimdharau au kumtukana.
Japo kuna wale ambao walitegesha mimba makusudi, wengi wao ilitokea kama Sisi ilivyotokea kuwapa mimba mabinti enzi hizo aafu mnaitoa.
Wengine waliona yawezekana nafasi ndio hiyo hiyo wakaamua kuzaa.