M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,027
Chadema wamekuwa wakijipa matumaini hewa kuhusu mgombea wao Lisu kushinda wakisema yuko popular sana.Wakisema wanalalia mtaji wa kura za 2015 ambapo Lowasa alipata kura milioni sita
Kitu kimoja wanasahau Lowasa alikuwa waziri mkuu muda mrefu na waziri aliyejulikana sana vijijini ambako asilimia 80 ya watanzania ndiko wanaishi ndio sababu yake moja kubwa kuzoa kura nyingi
Raisi Magufuli anafahamika vijiji vyote Tanzania nzima na ndiko wapiga kura wengi walioko sio mijini
Hata mijini Lisu anajulikana miji michache hasa kwa vijana wanaoshinda mitandaoni hasa wa Dar es salaam ambao wengi hata kujiandikisha kupiga kura wengi hawajajiandikisha ni washabiki tu wa siasa za mitandaoni
Pigo kuu la kubwagwa Lisu litatoka vijijini .Natoa siri ya wazi kabisa bila kuficha .Vijijini huyu Lisu hawamjui.Ofisi za CCM ZIKO KILA kijiji na hakuna mwanakijij asiyemjua Magufuli ni nani.Chadema waliwekeza viofisi vya hapa na pale vya kuzuga kwa msajili mijini viofisi vichache tu lakini vijini vijiji vingi hawako huko ndiko pigo zito la Lisu litatokea
Ndio maana hata mapokezi yake utakuta walikuwa wengi vijana wadogo hakukuwa na watu wazima na hata maeneo aliyopita watu walikuwa kama wakimashangaa hivi na watu wazima walikuwa wala hawana hamasa naye ni vijana mmoja mmoja tu pembeni mwa barabara alimopita walioonyesha hisia za kumshangilia hapa na pale ikamlazimisha mpiga kamera afiche kupiga kamera kwa aibu akawa haonyeshi kabisa walio pembeni mwa barabara msafara unamopita .Kamera yake ikajikita tu kwenye vijana walioko kwenye msafara wake anayebisha aangalie hizo video za msafara wake toka uwanja wa ndege hadi makao makuu kinondoni camera imekwepa kabisa kuonyesha watu waliojipanga kando ya barabara kuogopa aibu sababu hawakuwepo na waliokuwepo hawakuonyesha hisia za kumshangilia angalia kamera inawaonyesha walioko barabarani tu ambao wengi walikodiwa kumsindikiza.Mpiga picha yeyote akiangalia tu anajua walipiga picha tu za kudanganya wazungu pembeni mwa barabara hakuwa na washangiliaji!!! Pamoja na jiji la Dar kuwa na umati wa watu ful time
Angalia usanii wa Chadema Lisu anapungia mikono wasindikizaji pembeni mwa barabara hakuna wapungia mikono .
Wiki hii yote niko huku vijijini Rukwa & Katavi.... mwamko wa wananchi kumpata kiongozi atakayeweza kuwaondoa kwenye lindi la sasa la umasikini ni mkubwa mno.
Wanachojua ni kwamba chini ya serekali hii hawatapata unafuu wa maisha wowote.
So, ni suala dogo tu la Lissu & co kujipanga vyema, njia ya ikulu kwao October i wazi kabisa!