Sababu kuu za Mwakinyo kufungiwa kupigana tena Uingereza

Sababu kuu za Mwakinyo kufungiwa kupigana tena Uingereza

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Habari za ndani kabisa nimepenyezewa kutoka kwa mdau wa masumbwi huko Uingereza!

Uchunguzi uliofanywa na bodi ya ngumi kutoka Uingereza umebaini kwamba;

1. Mwakinyo Alidanganya "cheat" . uchunguzi umebaini kwamba kiatu alichopewa hakikuwa na madhara yoyote, hata hivyo alipatiwa kabla ya siku ya pambano hivyo alikijaribu na kujiridhisha kipo sawa!

Mdau alizidi kusema kitendo cha mwakinyo kusema alichezewa mchezo kwa kupewa kiatu kinachobana ni kashfa kwa bodi ya ngumi Uingereza ambayo ililenga kuichafua taswira ya ngumi nchini humo!

Hivyo mwakinyo kafungiwa kucheza michezo ya ngumi Uingereza kwa mujibu wa kanuni zinazozingatia 'Fair play"

2. Sababu ya pili iliyogundulika ni mazingira ya kuuza mechi! Hili nalo limechangia Mwakinyo afungiwe

3. Sababu ya tatu ni taarifa za kitabibu kutoka maabara ya uwanja wa ndege zilizobaini begi la Mwakinyo halikuwa na vitu vya kawaida kimchezo ambavyo vimetafsiliwa ni ushirikina katika mchezo.
4. Sababu nyingine kubwa kuliko zote ni za kiafya zaidi ambazo zinaweza kuhatarisha maisha yake na wengine katika mchezo wa ngumi! (Taarifa za afya zinabakia kuwa siri ya mgonjwa)

IMG-20220918-WA0000.jpg
 
Bongo walishajua wakasema wanaenda kuchunguza sio kwa ufala aliofanya.

Kusema ndani ya begi Kuna vitu vya kishirikina sio kweli sijawai kuona.

Kashfa ni hizo mbili za juu zaidi kutia aibu kwamba viatu alivyopewa ni kumsababishia kupoteza pambano na kingine ishu ya kuuza mechi.

Ukifuatilia comments niliwai kusema mwakinyo anaweza kufungiwa na hapa bongo pia nilisikia alikuwa hana leseni kutoka kweny bodi ya hiyo michezo na huyo mwenzie smith nae pia ni muhuni alishafungiwa kucheza marekani so hapo wahuni wamekutana na hapa bongo atakuja kukutana na rungu.

Zipo tetesi malipo hatopata kwa uthenge wake .kama mnabisha mtakuja kuona.
 
Leseni alitumiwa akiwa Uingereza
 
Back
Top Bottom