Mwanzo nilitaja neno 'muumba' kwenye hoja yangu,ukadai Nina majibu mfukoni,nikauliza universe na wewe na viumbe wengine wametoka wapi,Sasa hivi wewe ndiyo umeleta neno mungu muumba wa kila kitu.Mkuu,
Unajua hata wewe kuwa na swali ambalo hujui jibu, au hatukubaliani jibu, ni ushahidi kwamba hakuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote?
Angekuwepo Mungu huyo, wote tungekuwa na perfect knowledge.
Regardless ya ulimwengu ulipotoka, ulimwengu ulivyo, unavyoruhusu mabaya, unaonesha kwamba haujaumbwa na Mungu huyo.
Ungekuwa umeumbwa na Mungu huyo, usingeruhusu mabaya.
Halafu, swali lako la "ulimwengu umetoka wapi", kama ni muhimu sana, litakuja kutuonesha kwamba hakuna Mungu.
Kwa sababu, kama kila kitu ni lazima kitoke "wapi" fulani, hata huyo Mungu naye nitakuuliza hivyo hivyo.
Mungu katoka wapi?
Mimi naomba nijibu tu universe na wewe na Mammalia wenzio mmepatikana vipi!?..wewe ni mtu wa hoja,jibu..ni swali fupi Wala halihitaji 'gazeti'...hayo uliyoorodhesha ni hoja nyingine