Sababu kuu zenye Mantiki zilizowafanya na zinazowafanya Wayahudi wengi Wasimuamini Yesu Kristo

Sababu kuu zenye Mantiki zilizowafanya na zinazowafanya Wayahudi wengi Wasimuamini Yesu Kristo

S
rahim ni mzaliwa wa Uru WA ukaldayo, Iraq ya leo. Ni muaramu
Kwa hiyo Iraq siyo arabuni!?..Tena huo mji ambao Leo unaitwa tall Al mughayyar upo 300km kusini mashariki mwa Baghdad

Unaumwa wewe!
Iraq wapo waarabu?😂😂
Tangu lini wamedi/wairaq wakawa waarabu?
Au tangu lini waajemi/wairani wakawa waarabu?
 
Nitajie nguzo kuu za uislam?
Bila Shaka hizo ndio zinamtambulisha MTU kuwa ni muislam.
Baada ya kunitajia, niambie ni nabii gani kuacha Muhammad aliyeshika hizo nguzo kuu za uislam?

Wewe ndio utaanza Kupata Mwanga
Kwa nini unarukaruka kwenye hoja babu!!?..nimekuonesha Ibrahim,Musa nk ni manabii wa Allah kwa mujibu wa Qur'an,umerukia nguzo za uislam
 
Unaumwa wewe!
Iraq wapo waarabu?😂😂
Tangu lini wamedi/wairaq wakawa waarabu?
Au tangu lini waajemi/wairani wakawa waarabu?
Waajemi ni Iran,unamaanisha Iraq si nchi ya kiarabu, really!!!..kwamba Saddam Hussein na Tariq Aziz hawakuwa waarab
 
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani.

Leo Taikon atajadili sababu zinazopelekea wayahudi wengi kutokumuamini Yesu Kristo Kama Masihi wao na waulimwengu.

Andiko hili lijadiliwe Kwa Hoja zisizo na mihemko ya kidini. Kama unajijua Akili yako imefungwa fungwa hii mada haitakuhusu.

Hivi uliwahi kujiuliza ni Kwa nini Wayahudi hawamuamini Yesu Kristo? Yaani Kwa nini wamuamini Musa, Daudi, yona, Daniel, Isaya, Ezra, Joshua, n.k lakini Kwa nini hawataki kumuamini Yesu Kristo?

Embu nawe Fikiria hapo. Kumbuka hata huyo Yesu naye NI Myahudi.

Je, ni Yesu pekeake aliyekataliwa na Wayahudi au kuna manabii Masihi wengine waliokataliwa n mayahudi?
Ikiwa wapo je nini sababu ya wao kukataliwa? Nisirefushe andiko.

Twende sasa!

Wayahudi wanasababu kadhaa za kutokumzingatia Yesu kama Masihi au Nabii aliyetabiriwa katika maandiko kaa sababu kuu zifuatazo;

1. Yesu Mnazareth Hakutimiza Unabii hivyo anakosa vigezo vya kuwa Masihi mtabiriwa.
Hapa kuna mambo ambayo Masihi aliyetabiriwa alipaswa kuyatimiza Siku atakapokuja. Mambo hayo ni pamoja na;

a). KUSHUSHA UTAWALA WA MUNGU NA KUKOMBOA WANADAMU
Masihi aliyetabiriwa moja ya majukumu yake akija ni kukomboa Wanadamu na kushusha utawala wa Mungu. Wayahudi hawamuamini Yesu Wa Nazareth Kwa sababu hakutimiza Jambo Hilo. Hakuushusha utawala wa Mungu na wala hakumkomboa Mwanadamu.

Hii ni Kwa sababu mpaka hapa tunapozungumza Bado Dunia haijakombolewa, madhambi ni mengi, na utawala wa Shetani ndio umetamalaki.

Soma utabiri wa Isaya juu ya Masihi atakayekuja kisha linganisha, je Yesu Mnazareth analingana na utabiri huo;

Isaya 9:6
6 . Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto wa kiume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,
Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.

Ukichambua Unabii huo sentensi Kwa sentensi, je Yesu Mnazareth anatimiza Unabii huo. Embu tuone, "Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;"
Je Yesu alikuwa na uwezo wa kifalme began mwake? Je alitimiza vigezo vya kuitwa Mfalme? Labda Kwa vile hapa Tanzania kizazi cha sasa hakijaongozwa na wafalme. Lakini tunaweza kuchukulia mfano WA mamlaka ya Rais.

Je Yesu Mnazareth alikuwa anauwezo wa kirais, yaani mamlaka kama tuyaonayo Kwa Rais? Zingatia Mfalme ni zaidi ya Rais Kwa mambo mengi.

Ukisoma maandiko Yesu hakuwa na uwezo wowote wa Kifalme, alikuwa ni nabii kama walivyomanabii wengine.
Hivyo Sifa hii hakuwa nayo.
"Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,
Baba wa Milele, Mfalme wa Amani
"

Je, Yesu Mnazareth alitimiza Unabii wa kuwa na Sifa ya kuitwa Mungu mwenye nguvu? Je Yesu alileta Amani? Maana Unabii unasema ataitwa Mfalme wa Amani.

Je ni kweli Yesu alileta Amani Duniani? Jibu ni Hapana, Yesu Mnazareth hakuleta Amani. Msikilize Yesu mwenyewe;

Mathayo 10:34 BHN​

“Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.​

Yesu hakuleta Amani Duniani isipokuwa Upanga. Hivyo anakosa kigezo cha Nabii aliyetabiriwa na manabii wa zamani.

Kwa tuliosoma Histori ya Ulimwengu. Ukristo ndio dini pekee iliyoua Watu wengi Duniani katika kuueneza.
Watu wengi wameuawa Kwa sababu ya Kristo au Kwa jina la Kristo. Hivyo hakuwa Mfalme wa Amani Bali alikuwa Mfalme wa machafuko.

Ukombozi uliolengwa na manabii waliotabiri Ujio wa Masihi ulikuwa ukombozi wa Kimwili. Lakini Yesu hakuja kukomboa yeyote Kimwili. Hiyo ni hoja inayofuata baadaye

b) MASIHI LAZIMA AZALIWE KATIKA UKOO WA DAUDI LAKINI YESU HAKUZALIWA KATIKA UKOO WA DAUDI.

Wayahudi wanamkataa Yesu Kwa sababu yupo Kinyume na Unabii wa Masihi aliyetabiriwa. Ndio maana wao wanamsubiri huyo Masihi Kwa jinsi vitabu vyao vinavyoeleza.

Maandiko yanaonyesha kuwa Yesu hakuwa Uzao wa DAUDI. Hii ni Kutokana na sababu zifuatazo;

I) Yesu alizaliwa pasipo na Baba.
Maandiko yanaeleza kuwa Yesu alizaliwa Kwa Njia ya Roho mtakatifu. Hana Baba wa kibinadamu. Jambo ambalo linampotezea Sifa ya kuwa Masihi aliyetabiriwa.

Wayahudi wanaeleza kuwa Masihi aliyetabiriwa angezaliwa kikawaida kama binadamu wengine tena angetoka katika Uzao WA Daudi. Yaani Baba yake lazima awe katika ukoo wa Daudi (Daudi mtoto wa Year).

Mwanzo 49:10 BHN​

“Fimbo ya kifalme haitatoka kwa Yuda, wala bakora ya utawala miguuni pake, mpaka atakapofika yule ambaye ni yake; ambaye mataifa yatamtii.​

Soma Unabii wa Isaya;
ISAYA 11
1 Kutatokea chipukizi katika kisiki cha Yese,
tawi litachipua mizizini mwake.
2Roho ya Mwenyezi-Mungu itakaa kwake,
roho ya hekima na maarifa,
roho ya shauri jema na nguvu,
roho ya ujuzi na ya kumcha Mwenyezi-Mungu.
3Atafurahia kumcha Mwenyezi-Mungu.
Hatahukumu kadiri ya mambo ya njenje,
wala kuamua kufuatana na yale anayosikia.
4 Atawapatia haki watu maskini,
atawaamulia sawasawa wanyonge nchini.
Kwa neno lake ataiadhibu dunia,
kwa tamko lake atawaua waovu.
5 Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga,
uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni.
6 Mbwamwitu ataishi pamoja na mwanakondoo,
chui watapumzika pamoja na mwanambuzi.
Ndama na wanasimba watakula pamoja,
na mtoto mdogo atawaongoza.
7Ngombe na dubu watakula pamoja,
ndama wao watapumzika pamoja;
na simba atakula majani kama ng'ombe.
8Mtoto mchanga atacheza kwenye shimo la nyoka
mtoto ataweza kutia mkono shimoni mwa nyoka wa sumu.
9 Katika mlima mtakatifu wa Mungu
hakutakuwa na madhara wala uharibifu.
Maana kumjua Mwenyezi-Mungu kutaenea pote nchini,
kama vile maji yajaavyo baharini.
10 Siku ile chipukizi wa Yese atakuwa ishara kwa mataifa; mataifa yatamtafuta na makazi yake yatatukuka.
11Siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono wake tena kuwarejesha watu wake waliosalia huko Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Shinari, Hamathi na sehemu za pwani

Unabii huu unaeleza Sifa za Masihi atakayekuja, yaani sharti atokee Katika ukoo wa Daudi. Jambo ambalo Yesu Mnazareth maandiko yanaeleza kuwa hajatokea kwani hakuwa na Baba.

Hata Mariam mamaye Yesu angetokea ukoo wa Daudi bado isingemsaidia lolote Yesu kwani kiunabii au kimaandiko Uzao unatoka Kwa Baba.

Hoja hii inaungwa mkono na Wayahudi wengi na kufikia hitimisho kuwa Yesu sio Masihi aliyetabiriwa. Yesu hakuwa na Baba, huyo Yusufu ambaye ukoo wake umetajwa kwenye Biblia hakuwa Baba mzazi wa Yesu. Ndio maana alitaka kumkimbia Mariam.

Wayahudi wanadai kuwa Masihi angezaliwa kikawaida, Kwa kuwa Na Baba mzazi na Mama mzazi na sio kutumia njia ya miungu kutunga mimba. Jambo ambalo Wayahudi wanaliita ni dhana ya upagani wa Kirumi.

C) MASIHI LAZIMA AWARUDISHE WAYAHUDI WOTE WALIOTAWANYIKA DUNIANI WARUDI ISRAEL.
Yesu Mnazareth hakutimiza hilo. Wayahudi walichukuliwa uhamishoni huku na Huko. Na wapo wengine waliobakizwa Uyahudini.

Masihi aliyetabiriwa moja y majukumu yake ilikuwa kuwakusanya na kuwarejesha waisrael wote waliotawanyika warudi nyumbani Yesu hakufanya hilo. Hivyo anakosa Sifa za kinabii za Masihi aliyetabiriwa

ISAYA 11:
10 Siku ile chipukizi wa Yese atakuwa ishara kwa mataifa; mataifa yatamtafuta na makazi yake yatatukuka.
11. Siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono wake tena kuwarejesha watu wake waliosalia huko Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Shinari, Hamathi na sehemu za pwani.

Yesu Mnazareth hakumrejesha hata myahudi mmoja Israel. Hivyo anakosa Sifa za kinabii za Masihi.

Wakristo wanadai Yesu Mnazareth atatimiza hayo kwenye Ujio wa Pili Wakati upande Kwa Wayahudi na vyanzo vya Kiyahudi vinaonyesha kuwa MASIHI atatimiza utume wake Moja Kwa Moja. Katika Biblia hasa ya Unabii wa Masihi aliyetabiriwa hakuna dhana "Masihi Kurudi/kuja Mara yapili.

d) MASIHI ATAKUJA KUKOMESHA MAGONJWA, VITA, TAABU, NJAA N.K
Masihi aliyetabiriwa na manabii moja ya Kazi yake akija atakomesha magonjwa, Vita, Taabu, njaa na majanga mengine. Lakini Yesu Mnazareth hakukomesha chochote Kati ya hivyo kwani mpaka hivi leo, Mambo hayo yapo.
Hivyo anakosa Sifa za Masihi aliyetabiriwa.

Hoja ya kusema kuwa Yesu Mnazareth alikuja Kwa mambo ya ufalme wa Kiroho inazidi kumuondoa Yesu kwenye Sifa za Masihi aliyetabiriwa.

Labda tuseme, Yule Aliyetabiriwa na Yesu Mnazareth kuwa atakuja ambaye Wakristo wanamuita Roho mtakatifu ndiye Masihi ambaye kwa HAKIKA bado hajaja.

E) Masihi hataleta mambo ya utatu mtakatifu ambayo Kwa Torati ni Shirki, ibada za Sanamu.
Masihi ataleta ufalme wa Mungu, Haki yake, na utawala wake. Ataleta Amani Duniani. Hatakuwa sehemu ya Mungu, Ila atakuwa ni sehemu ya Uzao wa DAUDI. Utatu mtakatifu pekee yake unamuondoa Yesu Mnazareth katika Sifa za Masihi aliyetabiriwa na vitabu vya Kale.

Hao ni Wayahudi wanavyomchukulia Myahudi mwenzao yaani Yesu Kristo.

Maswali ambayo tunatakiwa tujiulize;

1. Ikiwa Yesu alitoka mbinguni, Kwa nini hakuandaa makao ya Watu wake Kabla hajaja Duniani kuwakomboa?
Badala yake Akaja Duniani kwanza ndipo akaenda kuandaa Makao. Hii maana yake ni nini?

Mungu aliumba makazi, Dunia ndipo akaumba MTU. Nuhu alijenga Safina ndipo akawakomboa Watu wake. Iweje Yesu aanze na ukombozi kwanz alafu ndio akaandae Makao?

2. Je Yesu na Ukristo, Yesu kama mwenye uwezo na Nabii. Kabla hajaja hakuona hatari ya Ujio wake kuwa mamilioni ya Watu watauawa kisa jina lake.

Yaani watalazimishwa kukubali jina lake kilazima hata kama hawataki? Kwa maana mpaka sasa jina la Yesu ndio linashikilia nafasi ya Kwanza Kwa Watu kuuawa ili tuu Watu waupokee Ukristo au waukatae Ukristo.

3. Iweje Yesu Mnazareth alishindwa kutimiza kazi yake Kwa miaka 33 aliyokaa Duniani mpaka awape majukumu Wanafunzi wake?

Je, hakuona kuwa kuna upotoshaji ungeweza kujitokeza Wakati ambapo hatokuwepo?
Ikiwa alilisha Watu zaidi ya elfu tano Kwa mikate mifano na samaki Wawili, akafufua Watu, na miujiza mingine, kumaanisha alikuwa na uwezo.

Ni kipi alishindwa kuhakikisha kila binadamu anayezaliwa automatically, amjue Mungu na habari zake pasipo kufundishwa na yeyote, ili kuepusha kile kiitwacho uongo na habari zake kuingiziwa hadithi za Uongo. Huo ungekuwa muujiza mzuri na wala asingewapa Wanafunzi wake kazi ya Kutangaza habari zake na habari za Mungu.

4. Yesu aliwaagiza Wanafunzi wake kuhubiri Injili. Je hakujua kuwa Miaka na miaka itapita, Vizazi na Vizazi vitapita.

Je, Vizazi ambavyo havikuwepo Wakati wake(Wakati WA Yesu) Sisi tukiwa miongoni mwa Vizazi hivyo, tunapata mamlaka ipi na uthibitisho upi kuwa Injili tuliyonayo ndio Ile aliyoitoa Yesu? Je, tutatumia kipimo kipi kuthibitisha ukweli WA kile tukisemacho?

5. Ikiwa lengo la Kufa Kwa Kristo ni kuwakomboa wanadamu na kuifia dhambi. Je kama dhambi ilikomeshwa na Kifo cha Yesu, ni kwanini Watu wanaendelea kutenda dhambi?

6. Swali la mwisho, ni Jambo Gani linalopelekea Wakristo kuamini Yesu Mnazareth ndiye Kristo/Masihi ilhali hajatimiza robo tatu ya Masihi aliyetabiriwa na manabii?

Kwa mfano, swali alilouliza Yohana Mbatizaji kuwatuma Wanafunzi wake wakamuulize Yesu kuhusu, Je Ni yeye Masihi au wamsubiri mwingine na jibu la Yesu kuwa viwete wanapona, vipofu wanatembea, viziwi wanasikia, na wafu wanafufuliwa. Je hiyo ndio ilikuwa misheni kuu ya Yesu?

Vipi kuhusu kuwarejesha Wayahudi Israel, vipi kuhusu yeye kuwa Mfalme na kuleta Amani na Haki Duniani, vipi kuhusu kuadhibu na kuhukumu?

7. Je Yesu anapowaambia Wanafunzi wake kuwa atarudi tena, je anaongea hayo Kwa kutimiza Unabii upi wa Masihi?

Maana hakuna sehemu Huko Nyuma ambayo ilitabiriwa ataondoka kisha atarudi tena. Ikiwa ndiye aliyetabiriwa, hiyo dhana aliitolea wapi?

Karibuni kwenye mjadala.
Mihemko hapa haitakuwa sehemu yake.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kaka robert ungenisaidia maana ya IMANI?
 
Kwa nini unarukaruka kwenye hoja babu!!?..nimekuonesha Ibrahim,Musa nk ni manabii wa Allah kwa mujibu wa Qur'an,umerukia nguzo za uislam

Wewe ndio hujui maswali yangu yanalenga nini.

Nilikuambia Unitajie manabii wa Dini wakiyahudi, ukanitajia. Nikakuambia VIZURI.

Sasa nilipokuambia unitajie manabii WA dini ya Kiislam naona unarudia walewale wa Wayahudi ndio maana nikakuambia wewe bado unasafari ndefu ya kujifunza mambo haya.

Ni Sawa na mkristo aambiwe ataje manabii wakubwa watano WA Kikristo alafu amtaje Musa au DAUDI au Suleiman, Wakati hao walikuwa ni mayahudi, dini Yao ni yakiyahudi na hawaujui ukrukri
 
King Cyrus The messiah, isaya 45:1.
Screenshot_20230121-140022.png
 
Kwa nini unarukaruka kwenye hoja babu!!?..nimekuonesha Ibrahim,Musa nk ni manabii wa Allah kwa mujibu wa Qur'an,umerukia nguzo za uislam

Wewe ndio hujui maswali yangu yanalenga nini.

Nilikuambia Unitajie manabii wa Dini wakiyahudi, ukanitajia. Nikakuambia VIZURI.

Sasa nilipokuambia unitajie manabii WA dini ya Kiislam naona unarudia walewale wa Wayahudi ndio maana nikakuambia wewe bado unasafari ndefu ya kujifunza mambo haya.

Ni Sawa na mkristo aambiwe ataje manabii wakubwa watano WA Kikristo alafu amtaje Musa au DAUDI au Suleiman, Wakati hao walikuwa ni mayahudi, dini Yao ni yakiyahudi.

Waislam
 
Uwe unaruhusu vitu vipya kuingia fuvu lako tofauti na uelewa wako wa awali,nilikujibu uislam ni dini iliyoanza tangu nabii Adam yaani dini ya awali mpaka Ibrahim na Muhammad,nijasema wayahudi wao walikubali baadhi ya manabii na kukataa baadhi wakiwemo yesu na Muhammad,maana yake wayahudi wanachagua miongoni mwa manabii hivyo katika orosha ya manabii wa wayahudi watatokea manabii wa Allah
 
Unaumwa wewe!
Iraq wapo waarabu?😂😂
Tangu lini wamedi/wairaq wakawa waarabu?
Au tangu lini waajemi/wairani wakawa waarabu?
Waarabu asili yao saudi arabia, yemen,,
Iraq, misri, palestine, moroco, etc, walikua arabised,, waliadopt
 
Dini ya kiyahudi imeanza miaka 3500 iliyopita,ikianza na Ibrahim,manabii watano kati ya 48 wa uyahudi ni Ibrahim,suleimani,daudi,Musa,harun,mungu wao ana majina mengi yehova,hosana nk
Hapa unaenda kinyume na uislamu hao Manabii hawakuwa wayahudi hata Qu'ran imesema wazi kuwa Nabii Ibrahimu hakuwa myahudi uyahudi ni dini wala sio Taifa Musa ,Haruni,Suleimani na Daudi wote amani iwe juu yao walikuwa Wana wa Israeli na sio wayahudi.
 
Waarabu asili yao saudi arabia, yemen,,
Iraq, misri, palestine, moroco, etc, walikua arabised,, waliadopt
Hili linathibitishwa vipi!?..historical time lines kwenye lugha na race Mara nyingi ni dhana tu, Saudi Arabia ipi!?..maana Saudi Arabia ya Leo imewekwa na muingereza huko nyuma ilikua city states,Makkah na Madina zikiwa nchi mbili tofauti, Oman,Kuwait, UAE inamaana walikua arabises!!?..na nani!?..mionekano yao inatofautiana!?
 
Uwe unaruhusu vitu vipya kuingia fuvu lako tofauti na uelewa wako wa awali,nilikujibu uislam ni dini iliyoanza tangu nabii Adam yaani dini ya awali mpaka Ibrahim na Muhammad,nijasema wayahudi wao walikubali baadhi ya manabii na kukataa baadhi wakiwemo yesu na Muhammad,maana yake wayahudi wanachagua miongoni mwa manabii hivyo katika orosha ya manabii wa wayahudi watatokea manabii wa Allah

Ndio nikakuuliza Ili MTU awe muislam lazima ashike nguzo tano si ndio?
Sasa zitaje nguzo tano za uislam alafu eleza Kwa ushahidi Musa, DAUDI, Suleiman walizishika nguzo hizo.

Maana wewe mwenye umewataja manabii WA Wayahudi alafu ajabu inawataja haohao kama manabii WA uislam, huoni kama unapotosha?
 
Hapa unaenda kinyume na uislamu hao Manabii hawakuwa wayahudi hata Qu'ran imesema wazi kuwa Nabii Ibrahimu hakuwa myahudi uyahudi ni dini wala sio Taifa Musa ,Haruni,Suleimani na Daudi wote amani iwe juu yao walikuwa Wana wa Israeli na sio wayahudi.
Nimeenda kihistoria anavyotaka yeye
 
Hapa unaenda kinyume na uislamu hao Manabii hawakuwa wayahudi hata Qu'ran imesema wazi kuwa Nabii Ibrahimu hakuwa myahudi uyahudi ni dini wala sio Taifa Musa ,Haruni,Suleimani na Daudi wote amani iwe juu yao walikuwa Wana wa Israeli na sio wayahudi.

Musa ndio aliyeanzisha uyahudi.

Ukisema Musa alikuwa Muislam nitakuuliza maswali ambayo mwenyewe utaona kabisa Musa hakuwa Muislam Ila alikuwa Myahudi
 
Ndio nikakuuliza Ili MTU awe muislam lazima ashike nguzo tano si ndio?
Sasa zitaje nguzo tano za uislam alafu eleza Kwa ushahidi Musa, DAUDI, Suleiman walizishika nguzo hizo.

Maana wewe mwenye umewataja manabii WA Wayahudi alafu ajabu inawataja haohao kama manabii WA uislam, huoni kama unapotosha?
Ili mtu awe muislam yampasa aamini mungu mmoja muumba wa kila kitu na kwamba alitumia manabii kuufikisha muongozo wake kwa binaadam,acha kurukaruka
 
Kihistoria
Kisayansi
Na kiimani manabii wote uliowataja hawakuwa waislam isipokuwa Huyo Muhammad tuu
Sayansi inathibitishaje unabii wa mtu,nikikupa Aya ya Qur'an 19:41-50 kuonesha Musa,Ibrahim nk ni manabii wa Allah
 
Ili mtu awe muislam yampasa aamini mungu mmoja muumba wa kila kitu na kwamba alitumia manabii kuufikisha muongozo wake kwa binaadam,acha kurukaruka

Kwa hiyo uislam unanguzo moja?😂😂😂

Dini nyingi zinaamini Mungu ni MMOJA ukiwepo dini ya kiyahudi.

Ukijadili vitu jadili kwa logic, itasaidia kuwafundisha wanaofuatilia mjadala na wanaopenda Kutumia Akili na logic
 
Hakuna nguzo za uislam zilizotajwa kwenye Qur'an,Ila mtua anayeamini mungu mmoja,manabii tangu Adam mpaka Muhammad,anaamini maisha baada ya kifo na malipo(akhera) huyo ni muislam
 
Back
Top Bottom