Sina pa kwenda
Senior Member
- Nov 18, 2010
- 113
- 15
Habari wanajamvi jamani hivi inawezekana mama mjamzito wa miezi minne kutokwa na damu? Na kama ndio inatokana na nini?
Msaada please
=========
Similar Cases
========
Ushauri:
Kutokwa damu kipindi cha ujauzito ni hali hatarishi, inawezekana ni dalili ya kutaka kuharibika kwa mimba au complications za mimba tu. Mama aidha hutokwa damu kwa kiasi kidogo(matone) au kiasi kikubwa, haswa kipindi cha miezi 3 ya kwanza ya mimba (first trimester) mpaka miezi 3 ya mwisho( third trimester). Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 25 ya wamama wajawazito wanatokwa na damu kipindi cha miezi 3 yao ya mwanzo (first trimester).
Mama anapotokwa damu huambatana na maumivu chini ya tumbo, kizunguzungu, kushindwa kuona vizuri na kuishiwa nguvu.
Mimba inapotungwa inapofika wiki ya 4 yai linakuwa fertilized na kushikilia uterine wall, hiyo hali inaweza msababishia mama kupata damu nyepesi kwa muda na baadae itakata(implantation bleeding). Implantation bleeding inakuwa damu nyepesi.
Damu inapotoka kiasi kidogo cha matone (spotting) hapo inaweza matatizo kama ya infection au dalili ya kuharibika kwa mimba ila damu inapotoka kwa wingi hiyo inakuwa hali nyingine kabisa.
Complication nyingine zinazoweza sababisha mama kubleed damu kwa wingi ni:-
1. Kuharibika kwa mimba. Mjamzito anapotokwa damu kwa wingi yenye madonge makubwa au madogo kidogo hiyo ni ishara kubwa ya kuharibika kwa mimba.
2. Kuharibika kwa placenta(kondo) kunachangia mama kutokwa damu.
3. Yai kutungwa nje ya mji wa mimba (ectopic preganancy). Mimba inapotungwa nje ya mfuko wa uzazi na badala yake inakuja kutungwa kwenye mirija ya uzazi(fallopian tube) hapo nafasi ya kulea mimba na kukuzia mpaka miezi 9 ni ndogo, hiyo hali inamletea mama kupata damu kwa wingi. Ndio mana Wizara ya Afya inashauri mama unapopata mimba toa taarifa kituo cha afya usisubirie ikue miezi 4-5 ndio uanze clinic.
4. Kondo(placenta) kuwa na matatizo kwenye ukuta wa uzazi.
5. Mabadiliko ya mwili yanachochewa na homoni(hormonal changes), inasababisha mama kutokwa damu matone madogo madogo (spotting).
6. Kushiriki tendo la ndoa uume akigonga kwenye mlango wa uzazi kunaweza msababisha mama kutokwa damu kidogo (matone). Mama akiona iyo hali ni vizuri kuacha kushiriki tendo la ndoa muda kwanza.
7. Maambukizi yanapompata kupitia ukeni au cervix kama U.T.I, kaswende, gonorea n.k ni rahisi kutokwa damu kipindi cha miezi 3 ya kwanza (first trimester). Mama mwenye infections anatakiwa kuwahi hospital ili kuokoa maisha yake na mtoto, infetions husababisha watoto kuzaliwa na ulemavu (kuona,kusikia n.k)
8. Mama anapofanyiwa vipimo na mkunga au daktari na kuwekea kidole ndani ya uke kunaweza msababishia kutokwa damu matone.
9. Mama anapojifungua kabla ya week 37(preterm labor) atasikia kutanuka kwa uke kunakoweza ambatana na damu, kuhara, maumivu ya mgongo na mvuto kwenye nyonga.
Muhimu:
Unapoona damu inakutoka haijalishi kidogo au nyingi, wahi hospital sababu hujui nini kimesababisha na inaweza kuwa dalili ya kuharibika kwa mimba. Kwa matibabu utafanyiwa ultra sound na vipimo vingine vya ukeni na tumboni n.k kujua tatizo ni nini.
Msaada please
=========
Similar Cases
Mjamzito anatokwa na damu. Rangi ni brown, inatoka kidogo tu, sio kama ya period, tumbo haliumi kabisa. Umri ni 29 ni mimba ya kwanza, sijawahi kuugua ugonjwa wa zinaa. Kama UTI ni ugonjwa wa zinaa niliugua mwaka jana mwezi kama wa sita hivi.
Kazi ngumu hapo ndio sielewagi ni zipi maana kazini na kuishia kwa kiti na kazi za kawaida. Sijawahi ugua homa muda mrefu sana, safari ndefu hapana, stress za kawaida sana hizi ugomvi wa hapa na pale.
Nilienda hospital Dr. akaniambia nikacheki kwanza Ultra sound nikaenda check ikaonekana hamna shida akanipa dawa zinaitwa Duphaston basi ndio naendelea kumeza ila sasa sijaelewa maana sasa imetokea mara ya pili thats why nimekuja kuuliza kabla sijarudi tena hospital maana appointment na Dr. Jumamosi ya 24/03/2013
Msaada wadau,
Mwanamke anapokuwa mjamzito na anatokwa na damu mara moja moja na wakati mwingine maji anakuwa na tatizo gani?
Wasalaam,
Kuna dada ana mimba ina miezi 3 na wiki mbili na hili amelijua siku chache zilizopita kuwa ana mimba na sababu ya kutokujua hadi inafika umri huo ni kwamba na alikua anapata hedhi kama kawaida japo anadai damu ilikuwa inatoka kdogo sio nyingi kama ilivyo kawaida na mpaka sasa hivi hali bado iko hivyo.
Hospitali kaenda kaelekezwa akanunue dawa ya kukata na mimba bado ipo.
Naomba kujua inawezekana mwanamke ana mimba na bado akatokwa damu? Na nini sababu yake na madhara yake pia kama damu itaendelea kutoka.
Naombeni msaada wa ushauri kwenu wataalam.
Wenye taaluma au uzoefu mnisaidie ni dalili ya nini? Siku za kujifungua alizoandika nesi zimepita kama wiki moja, but maumivu ya kiuno na nyonga na tumbo yanakuja na kutoweka, then damu kidogo na whitish mucus inafuata.What is that? Msaada pls...