Sababu mbalimbali zinazopelekea Mjamzito kutokwa damu ukeni

Sababu mbalimbali zinazopelekea Mjamzito kutokwa damu ukeni

Habari za asubuhi wanajamvini nilienda clinic wakanicheck Dr. akaniambia inabidi nichukue Bed Rest ndio nimeanza hvy! Nawashukuru wote kwa ushauri wenu, barikiweni saaana
 
Kama alivyojibu The secretary - hiyo ni dalili ya kuwa ujauzito wako upo hatarini sana - Katika hali ya kawaida damu yaweza kutoka kutokana na sababu mbalimbali lakini The worst case scenario yawezekana umepatwa na PPROM - Preterm Premature Rapture Of Membrane - Tiba ya hili tatizo mara nyingi huwa ni "bed rest" hadi utakapojifungua kwa wanaobahatika kujifungua...!

Hiyo kitaalamu tunaita antepartum haemorrhage (APH). Ikitokea ni kweli inamaanisha ujauzito upo hatarini. Sababu kubwa huwa ni kushika kwa kondo sehenu isiyo sahihi(placenta praevia). Na hili tatizo linahitaji bedrest!
 
Last edited by a moderator:
Msaada wadau,

Mwanamke anapokuwa mjamzito na anatokwa na damu mara moja moja na wakati mwingine maji anakuwa na tatizo gani?
 
Ndio, sometime huwa hivyo hasa mwanzoni, ukienda hospitalini watakwambia ujauzito unatishia kutoka...
But nothing serious.
 
Wasalaam,

Kuna dada ana mimba ina miezi 3 na wiki mbili na hili amelijua siku chache zilizopita kuwa ana mimba na sababu ya kutokujua hadi inafika umri huo ni kwamba na alikua anapata hedhi kama kawaida japo anadai damu ilikuwa inatoka kdogo sio nyingi kama ilivyo kawaida na mpaka sasa hivi hali bado iko hivyo.

Hospitali kaenda kaelekezwa akanunue dawa ya kukata na mimba bado ipo.

Naomba kujua inawezekana mwanamke ana mimba na bado akatokwa damu? Na nini sababu yake na madhara yake pia kama damu itaendelea kutoka.

Naombeni msaada wa ushauri kwenu wataalam.
 
Awahi mapema sana hosp hizo zaweza kuwa dalili za mimba kutoka (miscarriage)! Yaani mimba haikujishikiza vyema
 
Awahi mapema sana hosp hizo zaweza kuwa dalili za mimba kutoka (miscarriage)! Yaani mimba haikujishikiza vyema
Hospital ameenda kaandikiwa akanunue dawa za kukata damu isiendelee kutoka
 
Implantation bleeding ni Mwezi mmoja so aende hospital ni kama inatishia kutoka esp Kama anapata damu yenye vibonge
 
Wakuu kuna mwanamke ana ujauzito wa mwezi mmoja anatokwa na maji mepesi ukeni na mara chache vitone vya damu ukeni. Msaada kwa anaejua situation hii na solution yake.
 
mimba haiwezi kukaa, hiyo imemtokea mtu wangu wa karibu
 
Wahi hostpitali wanaweza kukushona na ukapata bed rest miguu juu mpaka hali itakapotengemaa.
 
Anaweza kusaidiwa ila sio hapa, hio tunaita threat for abortion, awahi hospital iliyo karibu atapata clinical help plz!!
 
Back
Top Bottom