Sababu mbalimbali zinazopelekea Mjamzito kutokwa damu ukeni

Sababu mbalimbali zinazopelekea Mjamzito kutokwa damu ukeni

Muwaishe hosp... Na utuambie pia ilikuaje ili na sisi tujifunze.
 
Wenye taaluma au uzoefu mnisaidie ni dalili ya nini? Siku za kujifungua alizoandika nesi zimepita kama wiki moja, but maumivu ya kiuno na nyonga na tumbo yanakuja na kutoweka, then damu kidogo na whitish mucus inafuata.What is that? Msaada pls...
 
Jamani wataalam njooni hapa mtoe ufafanuzi tafadhari
 
Nenda hospitali kwa msaada wa haraka na wa uhakika zaidi.
 
Na bado yuko nyumbani????
Hosptali kuna umbali gani kutoka hapo ulipo
 
Huo ndo uchungu wenyewe unaanza,wahi hosp,Leo au usiku lazima ajifungue.
 
Me nilizembea nusu niue mtoto eti navumilia uchungu home,ile kufika hospital tu kunicheck weee nilikimbizwa labor saa hiyo hiyo nikajifungua,but mtoto alikua amechoka.niligombezwa na manesi acha kabisa,so mpeleke akasubiri huko huko,na sababu kaanza na damu nenda hosp kubwa zenye madoc wazuri.
 
ndugu fanya uwahi hospital mapema, tarehe 5 ya mwezi huu mke wangu aliyekuwa na ujauzito wa miezi 6 alipata maumivu kiasi ya tumbo tukadharau tukihisi labda ni mabadiliko ya kawaida ila muda ulivoenda na maumivu yakaongezeka alipoenda kukojoa akaona damu kidogo ndipo tuliposhtuka na kwenda hospital tulifika mama akiwa na hali mbaya hata nikahisi nitampoteza ila kwa msaada wa madaktari wakamsaidia wakampa madawa ya kujifungua akajifungua kitoto cha kike ambacho kilikua kimeshafariki nashukuru mama anazidi kuimalika ila yuko so traumatic and we still trying to cope, usidharau chochote kinachomtokea mjamzito kwani athari zake ni kubwa!
 
Kwani mkienda clinic hamfundishwi lini uende hospital?
Dalili za kujifungua?
Dalili za hatari kwa mama mjamzito?
Mambo ya kujiandaa?
Siku zikipitiliza ufanye nini?

Tuache mchezo
Makosa yako
Kupitiliza siku n.a. kuendelea kukaa nyumbani kosa la kwanza
Kutokujua dalili za uchungu/hatari kosa la pili
Kupoteza muda kuandika huku wakati bado ako nyumbani hajafika kituo cha afya nne NB nilitegemea wakati unaomba ushauri huku awe ashafika hospital ndo tuwe tunapeana elimu nini cha kufanya kwa baada

Ushauri
Swala la afya ya uzazi ni keki sana kwa Sasa
Bab/mama kupata mtoto mwenye afya njema sio sport sport ongezeni speed ya kuhiraji kutafuta huduma za afya physically n.a. digitally kuepusha maafa
Matatizo mengine ya uzazi n.a. matokea yake tunajitakia wenyewe
Chagua uzazi salama watoto wenye afya
 
Kimbilia hospital haraka sana! Hongera!
 
Dr.mwanamke akiwa mjamzito halafu anatokwa Na damu nyepesi inaashiria nini?
 
Habari.., hizo si dalili nzuri hata kidogo kwa usalama wa mimba.., mara nyingi huishia kutoka zisipopatiwa ufumbuzi wa kitaalamu...!!!
USHAURI
Muda wowote kwa mjamzito akipata dalili yoyote ile isiyo ya kawaida kipindi cha ujauzito ni wakati muafaka kwenda hospitali bila kuchelewa..,nenda hospitali mara moja umalizapo kuisoma hii coment tafadhali kama una mpango wa kuendelea kuikuza hiyo mimba mpaka muda muafaka wa kujifungua ufike..!!!)))
 
Back
Top Bottom