Sababu ni ipi jiji la Mbeya kukosa show za wasanii?

Sababu ni ipi jiji la Mbeya kukosa show za wasanii?

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370
Yani inafika siku kama ijumaa ma jumamosi usiku namna cha msanii yeyote aliekuja kupiga show unaishia kuwaona tu YouTube na instagram ukiwa mkazo wa hili jiji,

sio hivyo tu hata clubs za kwenda kucheza mziki hili jiji wapo nyuma sana, zamani zilikuwpo royal pamodzi na Livingstone ila kwa sasa ni sawa na hakuna.

Unakuta wasanii hadi sumbawanga wanafika, hata mkoa wa karibu Iringa idadi yao ya show inaridhisha.

Mbeya nakumbuka msanii wa mwisho kuja alikuwa ni Mbosso kwenye ile Miss mbeya miezi kama minne hivi iliyopita, tangu hio show sijasikia tena kuna msanii mkubwa kaja kupiga show.

Zamani kidogo walisingizia vyuo vinavyichochea wasanii waje ni vichache ila kwa sasa kumekuwa na vyuo vingi hapa mjini kuanzia Saut pale mafiati, Tia hapo hapo mafiati, Mzumbe eneo la forest, Teku pande za block T, na vyuo vingine kama cbe na adem vilivyopo hapa town. Must sijaiweka kwasababu vijana kila muda wanaopiga misuli mizito.

Sasa najiuliza hivi ni kwanini wasanii hawatafutwi na mapromota au kujiandalia show Mbeya?????
 
Mbeya ni jiji la mungu ni kama Nazareth au Bethlehem,watu ni ibada sana so wasanii wa gospel mbeya ndio kwa kupigia Show na pesa.
 
Mbeya hamna club? Japo sio mpenzi wa club je city pub?? Maeneo ya wazi ya starehe mbeya canivo vp mbeya pazuri nasoma marafiki au Ulitaka nini. Mambo ya kuenda kuona vibongo fleva ni ya zamani na ya kishamba sana
 
E bhana vipi Mbeya,ile kitu ya kuitwa Kadansana bado ipo?
 
Mbeya hamna club? Japo sio mpenzi wa club je city pub?? Maeneo ya wazi ya starehe mbeya canivo vp mbeya pazuri nasoma marafiki au Ulitaka nini. Mambo ya kuenda kuona vibongo fleva ni ya zamani na ya kishamba sana
acha kulinganisha hizo bar na club mkuu, wanalazimisha zifanane na night clubs ila kiukweli hizi ni bar kwa kiasi kikubwa, huwezi linganisha hata na club D ya arusha
 
Ukweli ni kwamba wakifanya show Mbeya kama fiesta wanaambulia hasara kutokana na usela mavi wa masela na masista duu wa Mbeya wao hawalipi kiingilio wanapita njia za panya uwanja unajaa pesa dry
 
NASIKIA MBEYA NALO NI JIJI MKUU, INAWEZEKANA MBEYA WATU WAKE MABAHIRI SANA
Ni jiji ambalo limepata lift yake kwanza ya kupandia ghorofani mwaka 2014 na lift hio ilizinduliwa na mkuu wa mkoa hahah.
 
Mbeya ni jiji la mungu ni kama Nazareth au Bethlehem,watu ni ibada sana so wasanii wa gospel mbeya ndio kwa kupigia Show na pesa.
Jiji la Mungu siku hizi wameacha kuchuna ngozi za watu?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mbeya jiji letu
 
To be honest mbeya hakuna club ya maana..unaweza kupita kwenye pub au bar mbili tatu mwisho wa siku woote mnakuja kukutana city pub lounge
 
Yani inafika siku kama ijumaa ma jumamosi usiku namna cha msanii yeyote aliekuja kupiga show unaishia kuwaona tu YouTube na instagram ukiwa mkazo wa hili jiji,

sio hivyo tu hata clubs za kwenda kucheza mziki hili jiji wapo nyuma sana, zamani zilikuwpo royal pamodzi na Livingstone ila kwa sasa ni sawa na hakuna.

Unakuta wasanii hadi sumbawanga wanafika, hata mkoa wa karibu Iringa idadi yao ya show inaridhisha.

Mbeya nakumbuka msanii wa mwisho kuja alikuwa ni Mbosso kwenye ile Miss mbeya miezi kama minne hivi iliyopita, tangu hio show sijasikia tena kuna msanii mkubwa kaja kupiga show.

Zamani kidogo walisingizia vyuo vinavyichochea wasanii waje ni vichache ila kwa sasa kumekuwa na vyuo vingi hapa mjini kuanzia Saut pale mafiati, Tia hapo hapo mafiati, Mzumbe eneo la forest, Teku pande za block T, na vyuo vingine kama cbe na adem vilivyopo hapa town. Must sijaiweka kwasababu vijana kila muda wanaopiga misuli mizito.

Sasa najiuliza hivi ni kwanini wasanii hawatafutwi na mapromota au kujiandalia show Mbeya?????
RC wa mbeya pia ni kikwazo,hakawii kiamrisha wanaohudhiria matamasha ni halali wauwawe,,,,,mtazamo wangu tu washkaji msijenge chuki
 
Hivi kweli mtu mzima unaacha usingizi wako unaenda mwona hamorapa. Au bongo fleva kajiremba kama dada yake huku anaimba kama dada. Na kumbuka mbeya mji wa upinzani halisi hawa vijana wengi ni kijani je mnataka tukasikilize show za kishindo cha fulani. Mbeya aliepaweza ni Christian bela kila bada miezi mitatu yupo apa na raia wanajaa
 
Sio Mbeya tu mkuu, mimi nina takribani mwaka niko Njombe sijawahi kuona msanii wa maana wala Club cha maana hapa mjini!

Sijui shida ni nini!
 
Mbeya starehe zetu ni tofauti, usitake kulazimisha tulingane na maeneo mengine. Ukija Mbeya uliza tunachofanya usituletee astaarabu wako. Mbeya tunapenda zaidi pickn8ck na tour kuliko kwenda club. Kwa wapenda Club za maana wengi huvuka mpka kwenda Zambia, we like to keep that way.
Wakati vijana wa maeneo mengi nchini wakisukumizana kwa wingi kwenda Dar, idadi ya watu waliotoka Mbeya kwenda maeneo yote nchini haifikii hata nuxu ya idadi ya vijana toka mkoani Mbeya wanaokwenda nchi za nje kwenda kutafuta maisha.
Bakini na ustaarabu wenu tuacheni na wa kwetu.
 
Back
Top Bottom