Sababu nne(4) za msingi kwanini siwezi kutumia simu za Samsung (scumsung)

Sababu nne(4) za msingi kwanini siwezi kutumia simu za Samsung (scumsung)

Naomba mnielewe hapa sizungumzii samsung flagships kama s24,s24 ultra no. Mostly "A" series.

Zifuatazo ni sababu kwanini siwezi kutumia samsung mid rangers.

1.Design mbovu : hawa jamaa ubunifu sifuri wanatengeneza simu zenye muonekano wa mwaka 1990 hata tecno anawazidi.

¤Bezels nene(ufito wa pembeni wa simu)mfano A15,A25,A34:simu nyingi za sasa hivi ni less bezels au bezel less kabisa.

¤Mwaka 2023/2024 kutengeneza simu yenye water drop notch kama A16 ni uongo simu nyingi sasa hivi zina punch hole.

¤Simu nene(8.2mm) : sasa hivi makampuni mengi yanatengeneza simu nyembamba(7.7mm au 7.8mm)

2. Storage ndogo : amini usiamini hawa jamaa mwaka huu 2024 wametoa simu inaitwa A16 ina ram 4gb.hata wachovu Tecno mwaka huu base smartphone yao ina 8gb ram na 256gb rom.

3. Betri ndogo : hawa jamaa ni kawaida tu kutengeneza simu yenye betri 3900mahz halafu hyo simu wakaiuza milioni 2.

4. Screen resolution ndogo 1080×2340: hawa jamaa simu zao zote zinazouzwa chini ya milioni screen resolution ni moja
Endelea kufurahia kitochi chako,waache wenye brand yao waendelee kupiga hela
 
Nimekuja kufanya ubabe hapa lakini naona umeanza kwa kuomba msamaha kwa kuzitoa simu zangu za Samsung kwenye hii habari.

Siku nyingine andika kwenye heading kabisa nisisumbuke kuingia.
Samsung ni samsung tu. Hata A series pia ni samsung.
 
Samsung ni samsung tu. Hata A series pia ni samsung.
Yeah, lakini si ninayotumia mimi.

Hapo ni sawa umwambie mtu anayetumia Mercedes Benz S Class matatizo ya Mercedes Benz C Class. Hayamhusu.
 
REDMI au XIAOMI tena zile zenye chip.. Snapdragon 🔥🔥🔥 ukimiliki aina hii ya simu wala huta jutia na kampuni zingine utona ni kelele na michosho.
Kama ni mpenzi wa hizi simu just give a⭐
Kwenye hizi simu sitoki hadi naenda mbinguni.
specs-header02.png
Screenshot_2024-11-12-11-44-48-133_com.google.android.googlequicksearchbox.jpg
Screenshot_2024-11-12-11-42-54-728_com.google.android.googlequicksearchbox.jpg
 
Storage ndogo: Amini usiamini hawa jamaa mwaka huu 2024 wametoa simu inaitwa A16 ina ram 4gb.hata wachovu Tecno mwaka huu base smartphone yao ina 8gb ram na 256gb rom.
Storage ya kweli ila Ram na Camera Pixel ukiondoa sumsang wengjne waongo tu
 
Acha nikanunue Made in Tanzania kwanza ina uwezo.kuliko hata iphone
 
Back
Top Bottom