Sababu nne(4) za msingi kwanini siwezi kutumia simu za Samsung (scumsung)

Wengine flagship wanazionaga kwenye picha tu mtandaonišŸ˜‚
Hilo si tatizo, mradi tu ushajijua bajeti yako inaishia wapi, unakubali ukweli wa maisha tu.

Siyo bajeti yako ndogo, halafu hukubali ukweli wa maisha unailaumu Samsung badala ya kujiuliza kwa nini huwezi kumudu kununua Samsung flagship.
 
Samsung wana business model yao.

Wewe huna haki ya kuwapangia Samsung business model yao iweje.

Hilo tatizo ulilolitaja ni suala la business model ya Samsung, si tatizo ka Samsung kuwa na simu zisizo na ubora, kwa sababu Samsung ina simu zenye ubora ila hazipo kwenye bei unayitaka wewe tu.

Unajipa umuhimu usio nao kwenye biashara za watu.

Samsung si serikali ya kijamaa useme kwamba inakujali sana wewe mtumiaji kuliko inavyojali kutengeneza faida.

Inawezekana kabisa Samsung business model yao hawataki watu wa kajamba nani wengi wanataka watu wa flagship, wewe wa kajamba nani unalazimisha Samsung wawe na simu nzuri za kajamba nani wakati wao hawataki.
 
Scumsung!!

SomeThug

ScumBag

ScreamSung

...

simu ni itel tu!

mimi na itel ya milioni 8 ina ram 8gb na storage 512gb camera 72megapixel na betri 9200mAh.

Inakaa na chaji siku 8
Kanyagia kwenye tumbo bado anapumua huyo. Wuwaa😃
 
Hilo si tatizo, mradi tu ushajijua bajeti yako inaishia wapi, unakubali ukweli wa maisha tu.

Siyo bajeti yako ndogo, halafu hukubali ukweli wa maisha unailaumu Samsung badala ya kujiuliza kwa nini huwezi kumudu kununua Samsung flagship.
Bajeti ikiwa ndogo unanunua simu ambayo inafaa zaidi kwa bei hiyo ndio maana kuna reviews za simu. Mbona kuna makampuni mengi tu yanaweka specs nzuri kwa bei ya kati.
Kutaka kila mtu anunue flagship ni drama ambazo haziwezi kuja in real life. Hata huko Korea, Uingereza nk sio kila mtu anatumia flagship.
Kama una laki 8 unapaswa kupata simu inayoendana na laki 8, sio simu ambayo specs zake wenzako wanauza kwa laki 5 halafu wewe unauza laki 8 kwa kuwa tu una flagship nzuri. Realme mbona wana flagship nzuri ila hata midrange zao wanaziwekea telephoto cam, thin bezels na SoC za kueleweka. Hardware ya maana, angalia uwezo wa Poco X6 Pro na bei yake uone, ika chukua Samsung inayouzwa sawa na Poco X6 pro

A series sio mbaya ila zimekuwa priced horribly, A55 ilitakiwa iwe laki 7 kabisa sio hata laki 9 au milioni 1
 

Unataka kulazimisha Samsung wajali watu wasionunua flagship wakati kampuni ya Samsung si yako na wao hawajali watu wasionunua simu zao za flagship?

Samsung si kampuni yako, huipatii ruzuku, lakini unataka kuipangia jinsi ya kutengeneza simu na wauze bei gani?

Kwa nini usianzishe kampuni yako ya simu utoe simu nzuri zisizo flagship na wewe sasa?

Unataka kuwapangia watu wenye kampuni zao jinsi ya kufanya biashara zao?
 
Mimi biashara za watu siwezi kuingilia, kwani nimewapigia Samsung au kuwafuata kwenye email zao kuwaambia wabadilishe business model yao?
Kungekuwa hamna maana ya phone reviews kwa stahili hiyo unayoenda nayo. Kama kuna kampuni zinatengeneza simu nzuri kushinda Samsung kwenye midrange segment tusiseme?

Mbona nyinyi humu JF ndio vinara wa kuponda Tecno na Infinix? Kwani na yenyewe si ni kampuni na ina business model yake? Mbona hamuiheshimu? Au mpaka mtu akosoe Samsung ndio mnaona umuhimu wa hicho kitu unachoita business model? Inafurahisha sana jinsi binadamu tulivyo aisee..
 
Achen ku compare samsung na uchufuwenu Tecno 🚮🚮🚮
 
Ukishaanza kuwa bash Samsung kwa kusema simu hii walitakiwa kuiuza bei hii tayari unewapangia biashara.

Wewe kama hupendi bei kanunue brand nyingine tu, hujalazimishwa.

Kwani lazima utumie Samsung?
 
Wewe unaipatia ruzuku hiyo Samsung? Au una kiwanda cha simu?
 
Moja imenifikia sitaki hata kuzisikia
 
Ukishaanza kuwa bash Samsung kwa kusema simu hii walitakiwa kuiuza bei hii tayari unewapangia biashara.

Wewe kama hupendi bei kanunue brand nyingine tu, hujalazimishwa.

Kwani lazima utumie Samsung?
Huko sio kuwapangia biashara, usichanganye concepts.
Smartphone market ina simu nyingi, na mimi nazifuatilia kama mtu anayependa tech na huna haki ya kunizuia mimi kutoa opinion zangu
Samsung A series ziko horribly priced compared to other midranges (performance to price ratio) . Hicho ndio ninachosema. Unachofanya wewe ni kumwambia mtu anayesema "Harmonize hajui kuimba" basi aende akaimbe yeye. Nini maana ya artists na fans? Au nini maana ya producers na consumers? Hata haihusiani na suala la kulazimishwa kununua Samsung. Ni vile tu midrange zao hazipo vizuri sana. Period.
 
Wewe unaipatia ruzuku hiyo Samsung? Au una kiwanda cha simu?
Mimi sijalalamikia ubora wa Samsung, natumia flagship. Hivyo swali hilo halinihusu. Sijataka kuipangia bei Samsung. Sijaji mwambafy kwamba Samsung ifanye hivi, isifanye vile kwenye bei za simu.

Swali hilo ni kwa watu wanaojimwambafy kuipangia Samsung bei kama wewe.

Inaonekana umeshindwa hata kufuatilia mantiki ya swali, una changamoto ya kusoma kwa ufahamu na kufuatilia mantiki.

Watanzania acheni fikra za kijamaa jamaa za kufikiri haya makampuni ya kibepari yapo pale kuwasaidia nyie masikini msiotaka kulipa bei kubwa mpate simu za ubora wa hali ya juu.

Kampuni hizi zina uwezo wa kuamua business model zinazotaka, na nyie mna uhuru wa kuzigomea mnunue brand zenu za kujali watu wa kajambanani.

Usimlazimishe tajiri afanye biashara vipi.

Tafuta sehemu ambapo bajeti yako itakupa kitu unachokitaka.
 
Brand ya Samsung si brand sahihi kwako. Inajali flagship kuliko hizo simu za chini.

By design. Ndiyo business model yao.

Acha kulialia kulilia vitu vya kampuni zisizokujali.

Tafuta brand inayojali simu za chini kuliko flagship.

Usiwafundishe watu jinsi ya kufanya biashara zao wanazozijua kukuzidi wewe.

Kwani ni lazima ununue Samsung?

Usipotumia Samsung utakufa?
 
Kwanza kabisa unanikera unavyoniita masikini kila muda, na ndio kwanza niko university sijaanza hata maisha yangu na hata hujui hatma yangu, na every time unaniita masikini. Hivi huwezi kuongea hoja bila kukejeli?
Pia Samsung kuwa kampuni tajiri haibadilishi kitu kuwa kuna kampuni nyingine zina midrange bora kuliko hizo Samsung. Hata wewe unachofanya ni kutoa hoja yako sio kwamba Samsung watakuja wakupe hela au ubalozi kisa unawatetea JF.
Mimi kama consumer kama Samsung inatengeneza simu za uwezo wa chini kwa bei sawa na simu za uwezo wa juu zaidi, usiseme hainiaffect. Pengine nina laki 9 na ninapenda software ya Samsung ila hardware zao wanazingua (A55 inatumia Exynos 1480) kwa nini nisiumie? Kwa hiyo hata kama unapenda One UI itabidi uachane nayo tu kwa sababu unaweza kupata hardware bora zaidi kwingine.

We hao jamaa usiwatetee, midrange zao wanaboronga. Wenzao wanatumia Qualcomm Snapdragon 8s Gen 3 kwenye simu ya laki 8 wao wanaweka Exynos 1480 au 1380 ambazo zinapitwa hata na Qualcomm Snapdragon 7+ Gen 2 kwenye simu za laki 5 na nusu. Mi naona unatetea upuuzi
 
Wabongo wengi kama wewe mnapenda sana kupangia matumizi hela za watu.

Kifupi hiki ndicho unachofanya hapa.
 
Wabongo wengi kama wewe mnapenda sana kupangia matumizi hela za watu.

Kifupi hiki ndicho unachofanya hapa.
Mi najua wabongo wengi mkinunua flagship mnahisi mmetajirika hata kama kazi yako ni kuingia Insta tu kuangalia reels.
Mkikosa cha kufanya mnakuja kukejeli watu mitandaoni. Ndo unachofanya wewe hapa
 
Mi najua wabongo wengi mkinunua flagship mnahisi mmetajirika hata kama kazi yako ni kuingia Insta tu kuangalia reels.
Mkikosa cha kufanya mnakuja kukejeli watu mitandaoni. Ndo unachofanya wewe hapa
Mimi nahesabu nyumba Marekani mkuu, sihesabu simu.

I just bought like maybe my 30th Samsung/Lenovo tablet if you are into that shyt.

Lakini sipangii Samsung iuze bei gani simu zake.

Wewe unaipangia Samsung iuze bei gani simu zake.

Huijui dunia.
 
Scumsung!!

SomeThug

ScumBag

ScreamSung

...

simu ni itel tu!

mimi na itel ya milioni 8 ina ram 8gb na storage 512gb camera 72megapixel na betri 9200mAh.

Inakaa na chaji siku 8
Mae..!
 
Mimi nahesabu nyumba Marekani mkuu, sihesabu simu.

I just bought like maybe my 30th Samsung/Lenovo tablet if you are into that shyt.

Lakini sipangii Samsung iuze bei gani simu zake.

Wewe unaipangia Samsung iuze bei gani simu zake.

Huijui dunia.
Wewe unayeijua dunia unasupport horrible specs kwa high prices? Nini maana ya kujua dunia sasa kama unasupport hizo anti-consumer moves?
Unaweza ukawa Marekani na bado usiijue dunia kwa sababu Marekani sio dunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…