GWAPISYETO
New Member
- Dec 18, 2024
- 3
- 13
Hamjambo Watanzania!
Ni dhahiri joto la uchaguzi ndani ya chama cha upinzani cha CHADEMA limepamba moto na katika ufuatiliaji wangu kwenye mitandao ya kijamii hususani Youtube,X na Instagram nimeona maoni ya wananchi na wanachama wengi wa kawaida wanamhitaji Lissu kuliko Mbowe. Kwa usanisi wangu nimegundua hoja 5 zinazowekwa mezani.
HOJA YA 1: KURUDISHA DEMOKRASIA NDANI YA CHAMA
Wakati ambapo jina la chama linatanabaishwa kuwa na msingi mkubwa wa demokrasia lakini kuna wingu zito la udikteta liliingizwa chamani na Mhe. Mbowe kwa kuondosha ukomo wa madaraka.
Hii inafanya kufifisha harakati za kupigania demokrasia hata nje ya chama. Watu wanahoji inakuwaje CHADEMA waliounga mkono rasimu ya katiba ya Warioba iliyosheheni vifungu vya ukomo wa madaraka kwa viongozi wa umma lakini ndani ya chama chenyewe hawataki ukomo wa madaraka?
Kwa mantiki hiyo Mhe.Lissu au mtu mwingine apewe fursa ya uenyekiti wa chama na kanuni ya ukomo wa madaraka kwa viongozi wa chama itizamwe upya.
HOJA YA PILI: MISIMAMO YA KISIASA
Kwa siku za hivi karibuni Mhe.Mbowe ameonekana kushuka morali ya kusimamia maslahi ya chama. Ukiacha tuzo aliyoandaa na kumpa Mama huku akitahadharishwa na Lissu lakini bado ameonekana kutokujenga taswira ya chama kinataka nini?
Awali tulidhani katiba mpya na tume huru ya uchaguzi lakini ukiacha kukosekana kwa nuru ya hivyo vyote kupatikana bado Mwenyekiti alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha chama kinashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa bila kuwepo kwa tume huru wala katiba bora.
Hii inaonyesha ombwe la uongozi hivyo CHADEMA inahitaji mtu atakayeonyesha njia ya aidha katiba mpya ipiganiwe ili ilete tume huru na uchaguzi huru na haki ili upinzani ujipenyeze kwa haki kukamata dola vinginevyo itakuwa kama kushiriki siasa za ruzuku.
HOJA YA TATU: KUKOMESHA UKABILA NA UKANDA NDANI YA CHAMA
Hoja hii haipendwi na mara zote ikiibuliwa wahafidhina wa Mwenyekiti Mbowe hujibu kwa ukali sana lakini kwa mwenendo wa uchaguzi wa ndani ya chama toka enzi za kina Chacha Wangwe, Zitto Kabwe na hata sasa Kamanda Lissu anagombea kuna watu mfano Henry Kilewo ambaye ni mwenyekiti wa BAVICHA Dar anatoa hoja za kumtetea Mhe.Mbowe abaki madarakani bila kujali maslahi ya chama. Mfano, hakuna kikao chochote cha BAVICHA mkoa wa Dar es salaam kilichoketi kumuidhinisha Mbowe lakini machawa hususani wanufaika wa mfumo wa Mbowe au wanaotoka ukanda ule wamekuwa wakali na wanamtetea bila kujali maisha baada ya uchaguzi.
Inashangaza, mtu anasema hajali hata Mbowe akiongoza milele lakini anajali kwanini CCM isiongoze milele. Ili kuondosha ombwe hili tunahitaji dira ya mwenyekiti mpya.
HOJA YA NNE: KUSHINDWA KUPAMBANA NA MFUMO WA CCM YA SASA
Wakati ambapo CCM wakiwapa vijana exposure na kuwalea katika misingi ya uongozi bora hali imekuwa tofauti kwa CHADEMA. Kati ya mwaka 2010 mpaka 2018 kulikuwa na harakati nyingi za chama hususani mpango wa CHADEMA NI MSINGI ambapo lenho kubwa lilikuwa kufika mashinani kuimarisha chama hususani vijijini na kuwavutia vijana wengi wa vyuo vikuu kupitia CHASO lakini mipango yote hiyo imebuma na msisimko wa vijana wengi kwa chama umeshuka vibaya mno hivyo chama kinahitaji mwenyekiti mpya atakayetengeneza safu ya utendaji bora na kutekeleza maazimio ya chama yatakayopelekea kuendana na mfumo wa siasa za sasa za CCM wanaoimarisha Chipukizi, mabaraza ya vijana, wazee na wanawake huku wakisajili wanachama wengi kwa mfumo wa kidigitali.
HOJA YA TANO: KUONGOZA CHAMA KWA KUZINGATIA ITIKADI BADALA YA BUSARA
Duniani kote hakuna chama cha upinzani kinachokamata dola kwasababu eti kiongozi mkuu ana busara kama kipo nitajieni.
Chama lazima kiende kwa itikadi na falsafa zitakazokaa katika fikra za wanachama na wananchi. Katika nyakati tofauti tumeona chama kikipoteza mwelekeo kwa kutokusimamia itikadi. Mfano chama kiliingizwa kwenye fungate la 4R pasipokugundua kwamba ni karata ya chama tawala hivyo kujikuta baadae kimeachwa solemba. Watu wanauawa, watu wanatekwa, rasilimali za nchi zinaibiwa, uhuru wa kujieleza unakandamizwa, uchaguzi unaingiliwa kinyume na utaratibu, uwakilishi wa wananchi unadumazwa.
SAUTI YA MWENYEKITI WA CHAMA HAITOSHI ANAHITAJIKA MWINGINE.
Tubishane kwa hoja sasa✅