Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Hivi karibuni, wajumbe kutoka vyama vya siasa vya vya nchi mbalimbali walifanya ziara hapa Beijing, ambapo walitembelea majumba ya makumbusho ya historia ya Chama cha Kikomunisti cha China.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Nepal, Madhav Kumar Nepal, amesema falsafa ya rais wa China Xi Jinping kuhusu ujenzi wa chama “imejibu vizuri swali ambalo hakuna chama cha siasa kinaweza kulikwepa, lakini ni vyama vichache sana vimewahi kulijibu kwa dhati.”
Swali lenyewe ni lipi? Kwa ufupi ni kwamba, je, chama tawala kinawezaje kuhakikisha hakidhoofiki, hakipotezi mshikamano wake, na hakijitengi na wananchi?
Kuhusu swali hilo, Mkutano wa Tano wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uliofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba ulitoa jibu la kipekee la China. Mkutano huo ulipitisha azimio lililojikita katika dhana moja kuu: “kushughulikia mambo ya Chama kwa nidhamu kali katika pande zote”. Ingawa hii inaweza kusikika kama lugha kavu ya kisiasa, lakini umuhimu wake unahusika na maisha ya kila mtu wa kawaida. Basi CPC kimefanya nini ili kujibu vizuri swali hilo?
Kwanza ni mapambano dhidi ya rushwa. Tangu Mkutano wa 18 wa Wajumbe Wote wa CPC ulipofanyika, vyombo vya ukaguzi na usimamizi wa nidhamu vya CPC kote nchini China vimefungua kesi milioni 8.105 za ufisadi, na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanachama milioni 7.922 wa CPC, idadi ambayo ni karibu sawa na jumla ya watu wote katika nchi yenye ukubwa wa katikati. Ufisadi ni changamoto sugu kwa vyama vyote vya siasa duniani kote. Badala ya kuikwepa, CPC imetengeneza njia inayounganisha malengo matatu: kuhakikisha viongozi “hawathubutu” kujihusisha na rushwa, “hawawezi” kujihusisha na rushwa, na “hawana hamu” ya kujihusisha na rushwa.
Pili ni kukamilisha mifumo. Watu wengi wanaweza kudhani kuwa mifumo ya chama haina uhusiano mkubwa na maisha yao ya kila siku. Lakini fikiria hili: ikiwa chama cha kisiasa hakina sheria na nidhamu kali za ndani, je, sera zinazotungwa na chama hicho zinaweza kuaminika kweli? Kwa miaka mingi, moja ya kazi muhimu ya CPC imekuwa ni kuweka na kusimamia kwa ukali kanuni za ndani za Chama. Profesa Hisham Shaili wa Chuo Kikuu cha Khartoum nchini Sudan anaona kuwa, nchi za Afrika zinaweza kujifunza kutoka kwa uzoefu wa China, kwani kanuni inayosema “nidhamu kali huimarisha imani ya umma” ni ya kweli mahali popote.
Hatimaye, lengo la kimsingi la kazi zote ni kwa ajili ya watu. Taarifa zilizotolewa na mkutano huo zinasisitiza mara nyingi juu ya “kudumisha uhusiano wa karibu kati ya Chama na watu” na “kukuza kwa kina dhamira ya kuhudumia umma”. Hizi si kauli tupu tu. Utafiti uliofanywa mwaka jana na Idara Kuu ya Takwimu ya China ulibaini kuwa asilimia 95.5 ya waliohojiwa wanaunga mkono utekelezaji wa “Nidhamu Nane” (zinazohusu kuboresha mwenendo wa Chama na serikali), huku asilimia 92.2 wakiamini kuwa mabadiliko chanya katika mwenendo wa Chama na serikali yamechangia katika uboreshaji wa jumla wa maadili ya kijamii. Katibu Mkuu wa Chama cha Kisoshalisti cha Misri Ahmed Shaaban amesema, Rais wa China Xi Jinping daima anawajali watu, na CPC inafuata falsafa inayoweka watu katikati.
Hii ndiyo sababu ya msingi inayofanya Chama cha Kikomunisti cha China kuendelea kuaminiwa na kupata ushindi.