Sababu ya Dube kuomba kuondoka Azam

Sababu ya Dube kuomba kuondoka Azam

Yaani mtu mpaka kaandika barua na bado mnataka mseme kakurupuka??? Kwa hiyo hapo afanyeje??, fikra za baadhi ya wabongo anaeweza kuzielewa ni mtu asiejielewa kabisa

Yaani mtu kaandika barua kuijulisha klabu bado mtu anaona sio sawa, sa sijui kingine kipi huwa kinafanywa
Wewe ni miongoni mwa watu wachache wenye akili kubwa sana waliobakia hapa JF. Ulichokiandika ndio ukweli mtupu. Dube yuko sahihi, hajakurupuka na ndivyo utaratibu unavyotaka.
 
Shida huyo dogo ni "tripu" shamba "tripu" gereji lakini angekua hana majeraha ya mara kwa mara angekua anacheza kariakoo sasa hivi
 
Dube analeta utoto, kama unajua una mkataba na timu yako huwezi kukurupuka tu kutaka kuondoka, hizo ni bangi.

Hata kama anatakiwa na hiyo timu ya wafuga majini, awaambie viongozi wa wafuga majini waende kuongea na Azam wamalizane..

Hiki walichofanya kwa Dube ni kama wamemtuma kuvuruga mambo makusudi ili wapate mlango wa kuingilia..

Ili waanze kufanya mazungumzo na Azam, kwa kigezo mchezaji hana raha hapo alipo, kumbe wao ndio walimuagiza akose hiyo raha.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kulia alie tetere, akilia bundi uchuro!!
 
Dube amefuata utaratibu, na Azam wamefuata utaratibu. Iliyobaki ni Dube kukamilisha taratibu aruhusiwe. Hapa Azam ninawapongeza, maana hawajalazimisha akae nao mezani, wamemwambia tu leta mzigo tukupe ruhusa. Tena sio lazima kukutana, yeye Dube afanye deposit tu kwenye bank na atunze risiti
 
Itakua ni revenge ya Feisal, acha Azam nao wakomeshwe walishiriki sana kuharibu stability pale jangwani wakati team inapambana CAF
Mkuki kwa nguruwe kwa binadam mchungu... Kweli binadam mmeumbwa kusahau aiseee... Wakina Sureboy na Muda walisajiliwa vipi pale Uto?
 
Back
Top Bottom