Sababu za CCM kutoanguka tangu Uhuru hadi sasa

Siyo kweli.

Chama chenye nguvu kiasi hicho. KitaibaJe kura ?!.

Uwe na nguvu ukatae tume huru ?!. Uwe na nguvu ukatae katiba mpya ya wananchi iliyo fair ?!
 
CCM ni chama cha ukombozi, na vyama vingi vilivyopigania Uhuru wa nchi zao havipo tena madarakani lakini CCM bado ipo tu.
Yafuatayo ni baadhi ya michango iliyosababisha CCM iendelee kubaki madarakani:
Nyingine ni ujinga na uoga wawananchi wa kutojua haki zao
 
Kwani unailinganisha serikali ya CCM na serikali gani nyingine iliyowahi kuwepo Tanzania? unaposema haina ubaguzi mkubwa kwa wananchi, ni serikali gani imewahi kuwa na ubaguza kwa wananchi Tanzania?

Serikali ya CCM Zanzibar ndiyo iliyozidi kwa ubaguzi
 
Hapa ndo uwaga ninajisemea,ikiwa ni lazima kuwa na chama ni bora tuu niwe CCM,
hata Mbowe mwenyewe ni CCM.
 
Kianguke Mara ngapi ndio ujue?Chama ambacho kinakimbia uchaguzi na kuwategemea akina Kingai Mahita na Goodluck ndio Chama hai?
Mbona kinaendelea kuiongoza nchi?
 
Haianguki kwa kuwa ni chama makini chama cha mioyo ya watu kisicho na longolongo
Vyama vyenye asili ya kisosholist, kuanguka ngumu sana, cheki cuba, china venezuela etc,, sababu viko kwa ajili ya watu,,
Sasa hivi vyama vingine vinafanya siasa kufurahisha wazungu
 
Nitakusema kwa Nabii Lema, akuombee urudi mbinguni mkuu.. [emoji23]
 
Elimu Tz ni duni sana. Haiwezi kubadili fikra kwenye ubongo.
 
Umejiuliza baada ya vizazi vilivyozaliwa na kukulia katika mfumo wa chama kimoja kufariki kitatokea nini?
 
Hii sababu ya uholela inaibeba CCM kwa asilimia 50.

Kuweka mifumo dunifu ya elimu ni sababu ya muhimu pia.
 
Hapa ndo uwaga ninajisemea,ikiwa ni lazima kuwa na chama ni bora tuu niwe CCM,
hata Mbowe mwenyewe ni CCM.

Sasa kwa nini hutumika nguvu Za vyombo vya dola kulazimisha ushindi badala ya kuwaachia Hao wananchi wakaichagua hiyo CCM wanayoipenda?
 
Sasa kwa nini hutumika nguvu Za vyombo vya dola kulazimisha ushindi badala ya kuwaachia Hao wananchi wakaichagua hiyo CCM wanayoipenda?
Mkuu mimi sijui..ila shida iko hivi,

Ni chama kipi unaweza kufikiri kinaweza kupewa dola ?...

Sisi raia tuna hamu ya ukombozi kutoka CCM lkn viongozi wa upinzani hawako hivyo...wanachumia tumbo.
 
Hii sababu ya uholela inaibeba CCM kwa asilimia 50.

Kuweka mifumo dunifu ya elimu ni sababu ya muhimu pia.
Yuko Waziri mkuu alishasemaga hadharani kuwaambia watu na wafanyabiashara kuwa kama wanataka biashara na mambo yao yaende sawa bila kubughuziwa waichague CCM. Kauli ilimaanisha kuwa wakwepa kodi, wauza dawa za kulevya, wafanyabiashara bila leseni, wawindaji, wavuvi na wachimbaji haramu hawatabughuziwa kama wataichangia na kuichagua CCM. Hakuna mtu asiyetaka Uhuru kwenye mambo yake. Uholela ndiyo kete muhimu kwa CCM kuendelea kubaki, na hata Rais Maguli alilijuwa hilo, ndio maana alikuwa akisisitiza machinga wasibughuziwe hata kama wanaharibu mazingira, hawalipi kodi, wanazuia njia za wenzao wanaokwenda kwa miguu; na wafugaji waachwe wazurure na makundi ya mifugo yao kila pahala, wachimbaji waachwe wafukue mashimo kila pahala, mama ntilie waachwe wauze hata barabarani, masokoni na popote pale; kila nyumba ina flemu za maduka na kila duka kunauzwa chochote hata pombe, sumu za kuulia wadudu nk.; kila mtaa una glosary ya kuuza pombe, madaladala yanajaza abiria kupita kiasi na kusimama popote kubeba na kushusha abiria.
Hii haiko duniani kote, kama Siku akitokea kiongozi wa CCM akauziba uholela huu CCM itakiona cha moto.

Kete ya pili kuu ya CCM ni uwepo wa ardhi kubwa ya wazi. Ardhi kubwa ndio mapafu ya kupulia ya serikali ya CCM yanayosababisha CCM kuishi hadi leo. Watanzania wengi wenye hali mbaya ya kiuchumi wanakimbilia kwenye ardhi za wazi kujenga vijumba, kufuga, kulima bustani, kufungua garage, kupiga matofali, kulima mazao ya chakula na biashara, kujenga viwanda vidogovidogo, nk kwakuwa ardhi ipo bado. Siku maeneo yote ya wazi yakiisha mapafu haya yatajaa mavumbi, watu wataanza kujitambua na kuiluza maswali ya aina mbalimbali CCM na serikali yake.
 
Sasa kwa nini hutumika nguvu Za vyombo vya dola kulazimisha ushindi badala ya kuwaachia Hao wananchi wakaichagua hiyo CCM wanayoipenda?
Hata huko kuiba kura (kama kupo) ni jambo la muda tu, iko siku wananchi hawatakubali hata kura yao moja iibiwe na yeyote. Sasa hivi hawajali wizi wa kura kwakuwa bado kuna uholela katika maisha yao, uwepo wa ardhi ya wazi ya kupumulia na vyama vya upinzani kuwa dhaifu sana na vya kiganga njaa zaidi . Siku uholela ukiisha, ardhi ya wazi hakuna na vyama vya upinzani kuwa stronger hawatakubali kura yao iibiwe hata moja.
 
kuondoa Ukabila na dini ni sawa, lakini sio sababu kubwa kivileeee!!. Somalia ni dini na kabila moja lakini wanatifuana. Sudani, Yemen, Syria, Zambia, Marekani, Ualya wengi ni wakristo tu lakini vyama vinaangushwa vinaondolewa madarakani.
 
Mkuu mimi sijui..ila shida iko hivi,

Ni chama kipi unaweza kufikiri kinaweza kupewa dola ?...

Sisi raia tuna hamu ya ukombozi kutoka CCM lkn viongozi wa upinzani hawako hivyo...wanachumia tumbo.

Wananchi wenyewe wataamua kupitia sanduku la kura Na sio JWTZ, au Kamanda Sirro Na Mafia zake au TISS kupiga kambi Govt Press Na kuamua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…