PreGE2025 Sababu za CHADEMA Kuwatengua Mwita na Catherine zafahamika: Wamesaini waraka wa kupinga ajenda ya ‘No Reform no Election’

PreGE2025 Sababu za CHADEMA Kuwatengua Mwita na Catherine zafahamika: Wamesaini waraka wa kupinga ajenda ya ‘No Reform no Election’

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kuna utofauti sana kati ya CCM na vyama vingine vya upinzani kwenye kudeal na hoja tata ndani ya vyama.

Miaka ya 1992 - 1995 liliibuka kundi ndani ya CCM likijiita G55 likiongozwa na Njelu Kasaka na Philip Malmo. Agenda ya kubwa ilikuwa Serikali Tatu kwa maana ya kuitaka Serikali ya Tanganyika.

Hawa G55 wa CCM waliitwa kwenye vikao vya chama na Mwl. Nyerere alikuwa mmoja wa watoa mada ya kwanini Serikali mbili na si tatu. G55 hawakuelewa Somo. Maamuzi ikawa viongozi wao waingizwe kwenye mifumo ya uongozi ili waelewe vizuri maana ya Serikali Mbili. Njelu Kasaka akawa Naibu Waziri na Philip Malmo akawa Naibu Spika na hoja ya G55 ya CCM ikafia hapo! Kwa kifupi CCM ilitumia mbinu ya "Keep your enemy closer"!!!

Kwa upande wa Chadema, wao wameamua G55 wao kuwashughulikia kwa kuwavua vyeo na mchakato wa kuwafukuza uwanachama unaendelea. Halafu wanajiita chama Cha Kidemokrasia. Chama ambacho hakipo tayari kupata changamoto ndani yake. Mbowe asingelikuwa mvumulivu, basi leo Lissu si tu asingelikuwa Mwenyekiti wa Chadema, bali angelikuwa si Mwana Chadema.

Hapo ndipo unaona utofauti wa ukomavu wa kisiasa kati ya CCM na vyama vingine vya upinzani!
 
Ccm hata siku moja haivumili uasi ( dissent) ndani ya chama! Uasi wa aina yeyote ile adhabu yake ni kufukuzwa!
Yule mchungaji wa Kilimanjaro aliyehoji uhalali wa Samia kuteuliwa kugombea Urais bila mpinzani ndani ya ccm, alifukuzwa chamani bila kusita !😳😳
 
Hebu tuomeshe mahali John mrema akiwa kwenye maandamano😂. Mbona mnalilia na m23 wenu... Wachukueni wapambanaji wawasidie kuiaua chadema .
Anafukuza wapambanaji anataka kubaki na kenge wa mtandaoni wasiopiga kura hata akiwaita kuandamana wanajifunika shuka!
 
Kwa upande wa Chadema, wao wameamua G55 wao kuwashughulikia kwa kuwavua vyeo na mchakato wa kuwafukuza uwanachama unaendelea. Halafu wanajiita chama Cha Kidemokrasia. Chama ambacho hakipo tayari kupata changamoto ndani yake. Mbowe asingelikuwa mvumulivu, basi leo Lissu si tu asingelikuwa Mwenyekiti wa Chadema, bali angelikuwa si Mwana Chadema.

Kwani neno "demokrasia" maana yake nini?
Maana yake: mawazo ya wengi yatekelezwe, mawazo ya wachache yawekwe pembeni.
Hii G55 ya kina Mrema inapinga kanuni hii muhimu katika demokrasia.
John Mrema na msomi mwenye shahada ya kwanza katika sayansi ya siasa.
Alikuwa kwenye vikao vilivyopitisha maamuzi haya kwa mujibu wa kanuni ya wengi.
Baada ya kushindwa kupinga ndani ya vikao anakuja kupinga nje ya vikao.
Huo ni utovu wa nidhamu dhidi ya maamuzi halali ya vikao.
Bado wewe unaandika kuunga mkono upotofu wao huo.
Naishangaa sana "thought process" yako!
Totally illogical, fanciful and absurd.
 
Kuna utofauti sana kati ya CCM na vyama vingine vya upinzani kwenye kudeal na hoja tata ndani ya vyama.

Miaka ya 1992 - 1995 liliibuka kundi ndani ya CCM likijiita G55 likiongozwa na Njelu Kasaka na Philip Malmo. Agenda ya kubwa ilikuwa Serikali Tatu kwa maana ya kuitaka Serikali ya Tanganyika.

Hawa G55 wa CCM waliitwa kwenye vikao vya chama na Mwl. Nyerere alikuwa mmoja wa watoa mada ya kwanini Serikali mbili na si tatu. G55 hawakuelewa Somo. Maamuzi ikawa viongozi wao waingizwe kwenye mifumo ya uongozi ili waelewe vizuri maana ya Serikali Mbili. Njelu Kasaka akawa Naibu Waziri na Philip Malmo akawa Naibu Spika na hoja ya G55 ya CCM ikafia hapo! Kwa kifupi CCM ilitumia mbinu ya "Keep your enemy closer"!!!

Kwa upande wa Chadema, wao wameamua G55 wao kuwashughulikia kwa kuwavua vyeo na mchakato wa kuwafukuza uwanachama unaendelea. Halafu wanajiita chama Cha Kidemokrasia. Chama ambacho hakipo tayari kupata changamoto ndani yake. Mbowe asingelikuwa mvumulivu, basi leo Lissu si tu asingelikuwa Mwenyekiti wa Chadema, bali angelikuwa si Mwana Chadema.

Hapo ndipo unaona utofauti wa ukomavu wa kisiasa kati ya CCM na vyama vingine vya upinzani!
Maelezo mengi hata maana!!, Tumewauliza kwanini walishindwa kulikataa kwenye mkutano mkuu?. Au hawakuwa sehemu ya maamzi?.
 
Demokrasia ilikuwa wakati wa mikutano iliyopitisha wazo... Naamini kulitolewa nafasi ya wenye wazo mbadala. Wazo likishapitishwa na chama halipingwi ni utekelezaji....
 
Hebu tuomeshe mahali John mrema akiwa kwenye maandamano😂. Mbona mnalilia na m23 wenu... Wachukueni wapambanaji wawasidie kuiaua chadema .
Kenge za mtandaoni ni shida sana mna midomo!
 
Kenge za mtandaoni ni shida sana mna midomo!
Wachukueni hao wapambanaji basi 😂, m23 hawana nafasi tena ndani ya chama kilichozaliwa upya tena chama cha kizalendo chini ya Lissu na Heche. Nikukabia juu tu😊.
 
Ukisoma hoja zilizo ndani ya waraka wao unabaini G55 ni realists, ambao wanataka political leader na sio cult leader.

Watia nia ni wanachama ambao wanajua siri iliyo wazi ambayo watanzania wengi tayari tunaijua. Hakuna hao watanzania committed wa kuzuia uchaguzi mbele ya maji washa, virungu na mabomu ya machozi.

Kwa mtazamo wao ’no reform, no election’ ni kuchezea slim chances walizonazo kwenye viti vya ubunge na udiwani.

Head you loose, tail you loose (hiyo ndio situation ya CDM) ‘no reforms, no reforms’ chances za kufanikiwa ni 0.01% na wakiingia kwenye uchaguzi CCM itafanya yake.

Walau kwa kushiriki CDM wanaweza ambulia 5%-10% ya viti vya ubunge na udiwani kwa njia ya uchaguzi, jumlisha viti maalum na kupata ruzuku ya kuendeshea chama.

Kitu ambacho watia nią wamefanya ni risk assessment na ‘no reforms, no election’ presents a greater loss kwa CDM.

Mind you bila ya Mbowe baada ya kushindwa uchaguzi na kuamua kutoa hela zake tsh 50 million, vinginevyo BAWACHA mwaka huu wasingefanikisha sherehe zao za kila mwaka siku ya wanawake dunia. Uongozi wa CDM ulishawatamkia chama hakina hela za kuandaa sherehe zao.

Sasa bila ya ruzuku huko mbele hiko chama kitaendeshwaje.

No reforms, no elections ni agenda ya watu wasioelewa changamoto za kuendesha taasisi; utachangiwa kila mwezi ili uendeshe chama. Huyo Lissu atabaki Tanzania kwa miaka mitano akikosa uraisi na kusaidia hela za kuendesha chama kutoka mfukoni kwake.

CDM kwa sasa ina cult leader, na wachache waliobaki na akili humo wanajaribu kuokoa jahazi na kutaka kuachana na hadithi za ‘abunuwasi’ wanazouza uongozi uliopo na kuraka warudi kwenye dunia ya uhalisia.

Sikio la kufa uwa, alisikii dawa

Halafu we mleta mada unatuwekea maandishi ya njano sijui orange hujui wengine vision ni tia maji-tia maji humu; bila ya miwani kusoma mtihani; unaenda kutuongezea ugumu wa kusoma post kwa kuweka mirangi rangi ya ajabu.
 
Mrema na wenzake ni kenge kwenye msafara wa mamba
 
Mtaalam wa masuala ya utawala na uongozi, wa Chuo Kikuu cha Munich, Ujerumani, Profesa Dagobert Pinochet, anasema kuwa, tabia ya baadhi ya viongozi walioko kwenye ngazi za utendaji kupinga kichini chini maamuzi ambayo wanapaswa kuyasimamia, ni sumu kwa uhai wa taasisi.

Pinocheti anasema kuwa tabia hiyo huweza kusababisha taasisi husika kupoteza dira, yaani kuanguka kwenye mtaro wa "mission creep,".

Anasema kuwa hili ni jambo ambalo hatimaye huyumbisha taasisi hiyo kwa kuzalisha maagizo yanayokinzana kwenda kwa viongozi ambao ni watendaji wa ngazi za chini, yaani "antinomic delegation."

Sasa ni wazi kwamba kwa kuzingatia ukweli huu, leo tarehe 05 Aprili 2025, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Antipas Lissu, ameamua kutengua uteuzi wa Catherine Ruge kutoka kwenye nafasi ya Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema. Ruge alikuwa anakitumikia Chama kwenye Sekretarieti kama Mtaalaam wa Dawati la Jinsia.

View attachment 3294351

Catherine Ruge ni kiongozi wa pili kutenguliwa ndani ya siku mbili, wa kwanza akiwa ni Julius Mwita, aliyekuwa Katibu wa Sekretarieti ya Chadema.

Mwita amekuwa anapinga msimamo wa Chadema kuhusu ajenda ya “No reforms, no election” na amekuwa akiwahamasisha viongozi wengine kupinga ajenda hiyo.

Ajenda hii inalenga kuishinikiza Serikali kufanya mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi ili kuleta usawa na haki.

Kwa mujibu wa kauli ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu, aliyoitoa tarehe 03 Aprili 2025 wakati anaongea na watia nia wa Ubunge na Udiwani, "No reform No Election" ni ajenda yenye Baraka rasmi za Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chadema na inatekelezwa kwa kutumia "constitutionally protected tools of protest".

Mara tu baada ya kutenguliwa Mwita aliongea na waandishi wa habari na kuthibitisha tuhumhidhidi yake.

Tarehe 03 Aprili 2025, John Mrema na wenzake 55 walijibatiza jina la G55 kisha kuandika, kusaini na kusambaza “Waraka Maalum” wenye kubeba kilichotajwa kama “Ushauri kwa Chama” cha Chadema.

Katika waraka huu kina Mrema wanadai kwamba Chadema itenganishe madai ya mabadiliko ya kimfumo yatakayoleta chaguzi huru na zenye kuaminika (reforms) na ajenda ya kuzuia uchaguzi kwa kusogeza ajenda ya mabadiliko katika kipindi baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025;

Julius Mwita na Catherine Ruge ni miongoni mwa watu waliosaini waraka huo, wenye kupinga msimamo wa chama.

Hivyo, uamuzi wa kuwaweka pembeni kina Mwita na Ruge ni hatua mwafaka, na hasa kama tukitumia ubovu wa hoja zao zilizomo kwenye waraka wao, ulioambatanishwa hapa chini, baada ya kufupishwa na kuhakikiwa.

Sababu za Kina Mrema kuunga mkono uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025

Waandishi wa Waraka wanadai kwamba wanapinga mpango wa Chadema wa kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kabla ya mabadiliko ya kimfumo kwa sababu zifuatazo:
  1. Ajenda ya "No Reforms, No Elections" iliyoasisiwa na vikao vya Chadema haijumuishi kipengele cha kuzuia uchaguzi mkuu;
  2. Haiwezekani kuzuia uchaguzi wakati Chadema iko nje ya uchaguzi;
  3. Hakuna uwezekano wa kutekeleza ajenda hii kwa ufanisi katika muda mfupi uliobaki kabla ya Oktoba 2025;
  4. Tumekwishafeli kuzuia uchaguzi maana tayari mchakato wa kutekeleza uchaguzi umeshaanza na uandikishaji wapiga kura pamoja na kugawanya majimbo;
  5. Katiba ya Chadema inakitaka chama kushiriki uchaguzi mkuu kama njia ya kutafuta uhalali wa kuongoza nchi;
  6. Kuzuia uchaguzi kwa kuusogeza mbele baada ya Oktoba 2025 ni kuvunja haki za kikatiba za wanachama wa Chadema wanaotaka kugombea;
  7. Mpaka sasa vyama vyote vya siasa na madhehebu ya dini yenye waumini wengi hawaungi mkono ajenda ya kuzuia uchaguzi mkuu; na
  8. Ajenda ya kuzuia uchaguzi haiwezi kutekelezwa kwa kutumia mbinu ambazo hazivunji katiba na sheria za nchi.
Tathmini na majibu kwa hoja za waraka wa Kina Mrema

Hoja zote za Kina Mrema zimeshajibiwa na Lissu, hasa kupitia mkutano na watia nia uliofanyika makao makuu ya Chadema tarehe 03 Aprili 2025.

Majibu ya Lissu yako hivi:
  1. Ajenda ya "No Reforms, No Elections" iliyoasisiwa na vikao vya Chadema tangu enzi za Mwenyekiti Mbowe inajumuishi kipengele cha kuzuia uchaguzi mkuu na ushahidi wa video upo;
  2. Inawezekana kuzuia uchaguzi wakati Chadema iko nje ya uchaguzi huo kwani dhana ya kuwa nje ya uchaguzi kwa kiwango kinachomzuia mhusika kufanya kazi ya kuzuia uchaguzi inawahusu watu walioko nje ya Tanzania na sio vinginevyo.
  3. Hakuna uwezekano wa kutekeleza ajenda hii kwa ufanisi katika muda mfupi uliobaki kabla ya Oktoba 2025 lakini kuna uwezekano wa kusogeza mbele ratiba ya uchaguzi hadi baada ya mabadiliko kufanyika;
  4. Tumekwishafeli kuzuia uchaguzi maana tayari mchakato wa kutekeleza uchaguzi umeshaanza kwa njia ya uandikishaji wapiga kura pamoja na kugawanya majimbo lakini hatua zilizobaki za uchaguzi bado zinaweza kuzuiwa kwa ufanisi katika wakati mwafaka;
  5. Katiba ya Chadema inakitaka chama kushiriki uchaguzi mkuu ulio huru na haki lakini sio kushiriki uchaguzi wa kiinimacho;
  6. Kuzuia uchaguzi wa Oktoba 2025 kwa kuusogeza mbele sio kuvunja haki za kikatiba za wanachama wa Chadema wanaotaka kugombea bali kuandaa mazingira bira zaidi ya kulinda haki hizo;
  7. Sio kweli kwamba Mpaka sasa vyama vyote vya siasa na madhehebu ya dini yenye waumini wengi hawaungi mkono ajenda ya kuzuia uchaguzi mkuu maana hakuna ushahidi uliotolewa na mwandishi wa waraka; na
  8. Ajenda ya kuzuia uchaguzi inaweza kutekelezwa kwa kutumia mbinu ambazo hazivunji katiba na sheria za nchi mfano maandamano ya amani, mikutano ya hadhara kwa ajili ya kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa umma mpana, kufungua kesi mahakamani, na kujenga na kusambaza hoja kwa wadau wote, ndani na nje ya nchi, kwa njia mbalimbali halali.
Kwa ujumla, njia bora ya kuonyesha ubovu wa hoja ya akina Mrema ni kuiweka kwenye muktadha wa vigezo muhimu vya uchaguzi unaoweza kuleta ushindi kwa vyama vya upinzani.

Uwezekano wa kushinda uchaguzi hutegemea vigezo (determinants) sita, yaani: (1) mgombea bora, (2) ajenda bora, (3) mtandao wa rasilimali watu wenye kuongea lugha moja kabla na wakati wa kampeni, (4) rasilimali fedha za kutosheleza mahitaji ya kibajeti, (5) wapiga kura wenye kiu ya haki na amani na (6) mfumo wa uchaguzi ulio rafiki kwa wadai wote.

Vibadilika hivi sita, vinayo michango yenye uzito tofauti katika kufanikisha ushindi.

Kwa mujibu wa tunayoyajua kuhusu chaguzi za Tanzania tangu 2015 hadi 2024, michango hiyo, katika asilimia zilizo kwenye mabano, ni kama ifuatavyo:

Mgombea bora (5%), ajenda bora (5%), mtandao mpana wa rasilimali watu wenye kuongea lugha moja kabla na wakati wa kampeni (5%), rasilimali fedha na rasilimali vitu za kutosheleza bajeti ya kampeni ya angalau dola moja kwa kila mpiga kura (5%), wapiga kura wenye kiu ya haki na amani (5%), na mfumo wa uchaguzi rafiki (75%).

Kwa hiyo, ni ndoto za mchana kufikiria kwamba, mfumo wa uchaguzi unaoweza kubatilisha ushindi kwa yamkini ya 75%, unairuhusu Chadema kwenda kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba ikiwa na matumaini ya ikaambulia kitu chochote.

John Mrema, ni msomi mwenye shahada ya Chuo Kikuu katika sayansi ya siasa, na hivyo anapaswa kuelewa vizuri zaidi ukweli huu. Lakini bado anajitoa ufahamu.

==KIAMBATANISHO==

View attachment 3294686
John Mrema, Mwandishi wa "Waraka Maalum"

WARAKA MAALUM: USHAURI KWA CHAMA CHA CHADEMA​

KUTOKA KWA: John Mrema, Kwa Niaba ya Watiania 55 wa Chadema wa 2025 na Baadhi ya Viongozi wa Juu wa Chadema.

KWENDA KWA: Katibu Mkuu, Chadema Taifa, S.L.P 31191, Dar-es-Salaam.

TAREHE: 3 Aprili 2025.

I. UTANGULIZI

Kichwa cha Waraka hapo juu chahusika.

Pia rejea wito uliotolewa na Ofisi yako kwa tuliokuwa wagombea ubunge wa CHADEMA 2020 na watia nia wa ubunge 2025, ukitutaka kushiriki kikao maalum pamoja na viongozi wakuu wa Chama, kilichopangwa kufanyika tarehe 3 April, 2025, kujadili hali ya kisiasa na mwenendo wa Chama katika kudai chaguzi huru na zenye kuaminika (No Reforms, No Elections)

II. MADHUMUNI YA WARAKA HUU

Pamoja na kupokea wito wa kushiriki mkutano huo maalum, sisi, wagombea ubunge wa 2020 na watiania wa ubunge wa 2025, tumeona kuna viashiria vya kutopewa au kutopata nafasi ya kutosha kusikilizwa katika mkutano huo maalum, na kwa hiyo, tumeamua kukuandikia Waraka huu, kwa sababu zifuatazo:

1. Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe Tundu Lissu, akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Iringa ametamka wazi kuwa, wote wanaoona, "No Reforms, No Elections" haiwezekani ni wana-CCM pamoja na vibaraka wao.

Kauli hii ya Mwenyekiti tayari imezuia uhuru wetu wa kutoa maoni au ushauri mbadala dhidi ya "No Reforms, No Elections", kwani, kwa mujibu wa Mwenyekiti wetu, watu wa namna hiyo ni wana-CCM au vibaraka wao.

2. Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Chama ya kuchangisha fedha kwa ajili ya "No Reforms, No Elections", Mhe Godbless Lema, akihutubia mkutano jijini Arusha, amenukuliwa akisema kwamba wote wanaotaka ubunge au udiwani bila reforms waondoke CHADEMA.

Kauli hii ya Mhe Lema ya kufukuza watu wenye maoni mbadala ndani ya Chama, haijakanushwa na Chama, na inazidi kuondoa mantiki ya mkutano huo maalum wa kujadili mwenendo wa No Reforms, No Elections, kwani tayari washiriki tumewekewa mipaka na vitisho katika kujadili suala hilo.

3. Hivi karibuni, Mwanaharakati, Maria Sarungi, aliandika katika ukurasa wake wa "X" akikitaka Chama kiyaweke hadharani majina ya wote wanaotaka ubunge kwa udi na ubani bila reforms, na akatuhumu kuwa watu hao wanataka kufanya "blackmail" (kutishia) eti watahama chama.

Pia, Maria Sarungi, bila kujali mamlaka ya Ofisi yako, ametaka ajulishwe ni nani amewaita watiania kwenye mkutano huo maalum maana uongozi mzima upo field. Na akataka Chama kisiwahusishe watiania (do not engage them), bali waachwe waende CCM.

Kauli hizi za Maria Sarungi, ambaye si mwana Chadema, zinafanana na kauli za Mhe Lissu na Mhe Lema. Aidha, kauli hizi zinaingilia mamlaka ya ndani ya Chama, na Ofisi yako imezinyamazia kimya, huku kukiwa na taarifa kuwa Mwanaharakati huyo ana mgongano wa kimaslahi wa kutaka Chama kisishiriki uchaguzi wa mwaka huu kwa maslahi yake binafsi.

Kauli za Maria ambaye ni swahiba wa karibu wa baadhi ya viongozi wetu wakuu zinazidi kuongeza vitisho na kufinya uhuru wa maoni kuelekea katika kikao hicho maalum.

Kwa msingi huo, tunawasilisha mchango wetu wa mawazo kwa njia ya maandishi kama ifuatavyo:

III. TUNAUNGA MKONO MADAI YA MABADILIKO (REFORMS)

Tunaunga mkono na tupo tayari kuongeza nguvu zaidi katika jitihada zote za Chama za kudai mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi (reforms) ili kuwa na chaguzi huru na zinazoaminika.

IV. MAONI MBADALA DHIDI YA MPANGO WA KUZUIA UCHAGUZI

Tunasita kuamini katika mpango wa Chama wa kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa 2025 (iwapo mabadiliko hayatopatikana), tukiwa na sababu kuu zifuatazo:

1. Tunaona kuwa haiwezekani kuzuia uchaguzi kwa kuwa nje ya uchaguzi. Kujaribu kuzuia uchaguzi huku tukiwa nje ya uchaguzi itakuwa ni sawa na kufanya jinai.

Uwezekano pekee wa kuzuia uchaguzi ni kushiriki uchaguzi wenyewe kwa kuhakikisha tunaingiza wagombea katika uchaguzi.

Ni rahisi kwa wagombea kuhamasisha na kuongoza wananchi kuzuia uchaguzi katika vituo mahsusi vya uchaguzi, katika kata au majimbo yanayoelekea kufanyiwa hujuma kuliko kujaribu kuzuia uchaguzi wote huku tukiwa nje kabisa ya uchaguzi wenyewe.

2. Dhana ya "No Reforms, No Elections", ilianza kama kampeni mnamo mwezi Januari mwaka 2020 baada ya "retreat" ya Kamati Kuu iliyofanyika Makueni, nchini Kenya, na haikuwa na tafsiri ya kuzuia uchaguzi bali ilikuwa inalenga kuhamasisha uungwaji mkono wa kudai reforms.

3. Kwa muda mfupi uliosalia, hatuoni uwezekano wa kutekeleza kwa ufanisi mkakati wowote madhubuti wa kuzuia uchaguzi.

Tayari, uchaguzi wenyewe umeshaanza kupitia zoezi la uandikishaji wapiga kura ambalo limeshafanyika kwenye mikoa mingi nchini na mchakato wa uchaguzi unaendelea kwa hatua ya mgawanyo wa majimbo ya uchaguzi.

4. Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, ibara ya 4 inayohusu madhumuni ya Chama, dhumuni kuu la Chama ni kuongoza dola na kutekeleza madhumuni mahsusi ya kisiasa kama yalivyoainishwa katika kifungu cha 4.1, madhumuni ya kiuchumi yaliyopo kwenye kifungu 4.2 pamoja na madhumuni ya kijamii kama yalivyoainishwa katika kifungu 4.3. Kwa hiyo, kushiriki uchaguzi ili kuongoza dola ni sharti la kimsingi la kikatiba.

5. Ibara ya 5.2.2 ya Katiba ya Chama imetamka haki ya mwanachama wa CHADEMA kuwa ni pamoja na kuchaguliwa kuongoza na kuwakilisha Chama katika ngazi yoyote kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa ya sifa za uongozi.

Mpango wa kuzuia uchaguzi unaweza kukosa uhalali wa kutosha kikatiba kwa kuathiri haki za wanachama wa CHADEMA wanaotaka kugombea.

6. Ukiondoa chama chetu, mpaka sasa hakuna chama kingine hata kimoja cha siasa kinachounga mkono mpango wa kuzuia uchaguzi ikiwa reforms hazitopatikana.

Kinyume chake, kuna Chama kimoja tu cha upinzani ambacho kinapigania "reforms" lakini huku kikiendelea kujipanga kushiriki uchaguzi. Vyama vingine hususani vile vyenye kawaida ya kutumika na CCM, vimeendelea kutangaza nia zao za kushiriki uchaguzi.

7. Viongozi wa dini na madhehebu yenye waumini wengi hapa nchini, tayari wamehimiza na wanaendelea kuelimisha na kuhamasisha waumini wao kwenda kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi.

Hali hii inaashiria kuwa ama Chama chetu kimechelewa au tayari kimekwama kupata uungwaji mkono wa wadau muhimu katika mpango wa kuepuka uchaguzi usio na reforms.

8. Uchunguzi na uchambuzi wetu unaonesha kuwa wadau wengi wa demokrasia wanaunga mkono madai yetu ya "reforms", lakini wanasita kuunga mkono mpango kamili wa Chama chetu wa kuzuia uchaguzi iwapo "reforms" hazitopatikana, kwani hali hiyo kwao inatafsiriwa kuwa ni karibu sawa na kufanya uasi au kuvunja katiba na sheria zilizopo licha ya ubaya wake.

Kwa maneno mengine, msisitizo wa kuzuia uchaguzi unaathiri au kupunguza kasi ya uungwaji mkono katika madai ya msingi ya reforms.

9. Kushindwa kuzuia uchaguzi katika dakika za mwisho (ikiwa jitihada za kupata reforms zitakwama), kunamaanisha kuwa Chama hakitokuwa tena na muda wa kujiandaa na hivyo hakitoshiriki kabisa uchaguzi huo.

10. Mhe Katibu Mkuu, matokeo ya kushindwa kuzuia uchaguzi yatakuwa ni kutoshiriki uchaguzi. Katika moja ya mahojiano yake na vyombo vya habari, Makamu Mwenyekiti wa Chama, Mhe John Heche, alithibitisha ukweli huu pale alipojibu swali la Chadema itafanyeje iwapo haitofanikiwa kuzuia uchaguzi.

Mhe Heche, aliweka bayana kuwa "ikiwa hivyo basi Chama hakitoshiriki uchaguzi".

V. ATHARI ZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI

Ni maoni yetu kuwa Chama kitafikwa na athari zifuatazo iwapo hakitoshiriki uchaguzi:

1. Chama kinaweza kuondokewa au kupoteza viongozi na wanachama wenye nia ya kuwania urais, ubunge, udiwani pamoja na nafasi za viti maalum vya ubunge na udiwani katika maeneo mbalimbali nchini.

2. Chama kitapoteza mvuto kwa umma, kitadhalilishwa kwa propaganda na hata kudhohofika.

Hadi sasa Chama kimekatika katika vipande viwili vinavyosigana kuhusu jambo hili.

Ikitokea tukashindwa kushiriki uchaguzi, mkatiko huu utakuwa ni wa wazi na athari zake zitakuwa mbaya zaidi.

3. Chama kitapoteza kabisa ruzuku baada ya uchaguzi na hivyo kuathiri uhai na uendelevu wa shughuli za Chama.

4. Ari na hamasa ya wanachama kukichangia Chama itazidi kushuka kwani wananchi hawatoona faida ya kukichangia Chama kisichoshiriki uchaguzi.

5. Kutoshiriki kampeni na uchaguzi kutakipotezea Chama fursa ya kujijenga zaidi maana haitokuwa rahisi kwa watiania kuwekeza kwenye Chama ambacho hakiingii kwenye uchaguzi maana hawatopata fursa ya kugombea.

6. Kwa ujumla, kutoshiriki uchaguzi kutasababisha Chama kupoteza uhusika na umuhimu wake kwa umma (relevance), hali inayoweza kufuatiwa na kuporomoka kisiasa na hatimaye kudhohofika kabisa.

VI: USHAURI WETU: TUJIANDAE KWA UCHAGUZI

Kwa kuzingatia msingi wote huo, sisi tuliokuwa wagombea ubunge 2020 na watiania wa ubunge 2025, tunakishauri Chama chetu (CHADEMA) kwamba tuendelee na tuongeze kasi na nguvu ya kudai mabadiliko yatakayoleta chaguzi huru na zenye kuaminika (reforms), lakini bila kuchanganya madai hayo na ajenda ya kuzuia uchaguzi.

Badala yake, Chama kiruhusu kuanza mara moja kwa maandalizi ya chini kwa chini ya kujipanga kwa ajili ya kushiriki uchaguzi hata kama “reforms” zitakuwa zimekawia kupatikana.

Tunatoa ushauri huu tukiwa ni wana Chadema makini, wenye mapenzi mema na uaminifu wa hali ya juu kwa Chama chetu, huku tukisukumwa na maslahi mapana na endelevu ya Chama na nchi yetu. Katika ushauri wetu huu, tumetilia maanani masuala ya msingi yafuatayo:

1. Upo uwezekano wa kushinda uchaguzi wa 2025 na kutangazwa katikati ya vikwazo vingi vya kikatiba, kisheria na utamaduni mbaya wa CCM wa kubaka demokrasia.

Pamoja na hujuma na uonevu wote tuliofanyiwa katika chaguzi zilizopita, bado yapo madhaifu ya ndani ya kirasilimali na kimkakati yanayoweza kuondolewa na hivyo kukifanya Chama kiingie katika uchaguzi huu kikiwa na nguvu mpya na mikakati madhubuti ya kukabiliana na hujuma za CCM na serikali yake kwa kiasi kikubwa.

Zipo nchi nyingi duniani na ndani ya Bara la Afrika ambazo vyama vya upinzani viliweza kupambana na kushinda chaguzi katikati ya mazingira onevu na kandamizi ya katiba na sheria za uchaguzi.

Wakati tukipigania reforms, tuchukue vile vile wajibu wa kuandaa mkakati kabambe wa kuikabili CCM katika mazingira magumu ikiwa reforms hazitopatikana kwa wakati.

2. Tukijipanga vizuri kimkakati, kushiriki uchaguzi kutatupatia fursa kubwa na nzuri zaidi ya kuuzuia uchaguzi kirahisi kwenye vituo na maeneo mahsusi yanayoelekea kufanyiwa hujuma.

Tunasisitiza kuwa ni ngumu na kwa kweli haiwezekani kuuzuia uchaguzi huku tukiwa nje ya uchaguzi.

3. Kushiriki uchaguzi kutatupatia fursa ya ziada ya kuyatumia madhila ya uchaguzi katika kuwaunganisha, kuwachochea na kuwaongoza wananchi kuendeleza vuguvugu la kudai reforms kwa kishindo kikubwa zaidi.

4. Kushiriki uchaguzi kutasaidia kuimarisha na kuendeleza umoja na mshikamano wa Chama, wanachama na wananchi, kutahuisha uhai na kuendeleza nguvu, hamasa na harakati za Chama (mabadiliko ni mchakato)

5. Ikumbukwe kwamba, pamoja na mapungufu makubwa ya katiba na sheria za uchaguzi, bado si hujuma zote tunazofanyiwa katika chaguzi zimetamkwa au zimehalalishwa katika kisheria.

Vitendo vya mawakala wetu kutoapishwa, mawakala wetu kuzuiwa kuingia vituoni, wagombea wetu kunyang'anywa fomu, wasimamizi kukimbia ofisi ili kukwepa kupokea fomu za wagombea wetu na kura feki kuingizwa vituoni, si matendo ambayo yamehalalishwa na katiba wala sheria bali ni uhuni tu unaofanywa na CCM na serikali yake na ambao upo kinyume pia na sheria zilizopo.

Kwa hiyo, mbali na kupigania reforms kwaajili ya kuleta chaguzi huru na zenye kuaminika, kushiriki uchaguzi kutatupatia fursa ya kuja na mikakati madhubuti ya kukabiliana moja kwa moja na vitendo vya kihuni vilivyo kinyume kabisa na sheria zilizopo.

VII. HITIMISHO

Mheshimiwa Katibu Mkuu, tunaomba uzingatie kuwa tumetoa maoni na ushauri wetu huo baada ya Ofisi yako kutualika kujadili ajenda ihusuyo hali ya kisiasa na mwenendo wa Chama katika kudai chaguzi huru na zenye kuaminika.

Kwa muhtasari, maoni na ushauri wetu, vimejikita katika kuunga mkono madai ya reforms lakini wakati huo huo tukikisihi Chama chetu kione haja ya kujiandaa na hatimaye kushiriki uchaguzi mkuu wa 2025 hata kama “reforms” hazitopatikana kwa wakati.

Kwamba, kushiriki uchaguzi kutatuepusha na athari nyingi na za muda mrefu za kudorora kwa Chama, huku tukiwa pia na uwekezakano wa kushinda au kuzuia uchaguzi kwenye maeneo au mazingira mahsusi ya kiuchaguzi yatakayoelekea kufanyiwa uhuni au hujuma dhidi ya demokrasia.

Tunaomba Chama kiyazingatie, kiyape kipaumbele katika tathmini na tafakari zake na kiyafanyie kazi maoni na ushauri wetu huo kwa kina, kikiongozwa na fikra chanya, maslahi mapana na endelevu ya Chama, pamoja na nafsi zilizojaa upendo, umoja na mshikamano kwa wanaChadema wote.

Tunapenda kusisitiza kuwa maoni na ushauri wetu huo si wa kupinga msimamo wa Chama, bali ni wa kupendekeza namna bora zaidi ya kuziendea reforms huku tukilinda ustawi endelevu wa Chama chenyewe chini ya imani kuwa "change is a process" (mabadiliko ni mchakato).

Tunapenda ieleweke kuwa iwapo Chama hakitakubaliana na maoni na ushauri wetu, basi tutaendelea kuheshimu msimamo na mwelekeo wa Chama kwa uaminifu na mapenzi yetu yote.

VIII. SAHIHI ZA UTHIBITISHO

Pamoja na salaam za "Stronger Together"

Mungu ibariki Chadema, Mungu ibariki Tanzania.

Tunaomba kuwasilisha.

Chama kinaongozwa na watu wasiokuwa na maarifa
 
Kuna utofauti sana kati ya CCM na vyama vingine vya upinzani kwenye kudeal na hoja tata ndani ya vyama.

Miaka ya 1992 - 1995 liliibuka kundi ndani ya CCM likijiita G55 likiongozwa na Njelu Kasaka na Philip Malmo. Agenda ya kubwa ilikuwa Serikali Tatu kwa maana ya kuitaka Serikali ya Tanganyika.

Hawa G55 wa CCM waliitwa kwenye vikao vya chama na Mwl. Nyerere alikuwa mmoja wa watoa mada ya kwanini Serikali mbili na si tatu. G55 hawakuelewa Somo. Maamuzi ikawa viongozi wao waingizwe kwenye mifumo ya uongozi ili waelewe vizuri maana ya Serikali Mbili. Njelu Kasaka akawa Naibu Waziri na Philip Malmo akawa Naibu Spika na hoja ya G55 ya CCM ikafia hapo! Kwa kifupi CCM ilitumia mbinu ya "Keep your enemy closer"!!!

Kwa upande wa Chadema, wao wameamua G55 wao kuwashughulikia kwa kuwavua vyeo na mchakato wa kuwafukuza uwanachama unaendelea. Halafu wanajiita chama Cha Kidemokrasia. Chama ambacho hakipo tayari kupata changamoto ndani yake. Mbowe asingelikuwa mvumulivu, basi leo Lissu si tu asingelikuwa Mwenyekiti wa Chadema, bali angelikuwa si Mwana Chadema.

Hapo ndipo unaona utofauti wa ukomavu wa kisiasa kati ya CCM na vyama vingine vya upinzani!
Hata kuwatimua ndio demokrasia yenyewe hiyo
 
Ccm hata siku moja haivumili uasi ( dissent) ndani ya chama! Uasi wa aina yeyote ile adhabu yake ni kufukuzwa!
Yule mchungaji wa Kilimanjaro aliyehoji uhalali wa Samia kuteuliwa kugombea Urais bila mpinzani ndani ya ccm, alifukuzwa chamani bila kusita !😳😳
Nani alifukuzwa kwenye G55? Mzee Omulangira Leopard Lwizandekwe alichukua fomu ya kugombea Urais na Mlw. Nyerere mwaka 1964! Hakufukizwa na mpaka mwaka jana kaadhimisha miaka 95 ya kuzaliwa akiwa amevaa kofia ya CCM!!
 
Kwani neno "demokrasia" maana yake nini?
Maana yake: mawazo ya wengi yatekelezwe, mawazo ya wachache yawekwe pembeni.
Hii G55 ya kina Mrema inapinga kanuni hii muhimu katika demokrasia.
John Mrema na msomi mwenye shahada ya kwanza katika sayansi ya siasa.
Alikuwa kwenye vikao vilivyopitisha maamuzi haya kwa mujibu wa kanuni ya wengi.
Baada ya kushindwa kupinga ndani ya vikao anakuja kupinga nje ya vikao.
Huo ni utovu wa nidhamu dhidi ya maamuzi halali ya vikao.
Bado wewe unaandika kuunga mkono upotofu wao huo.
Naishangaa sana "thought process" yako!
Totally illogical, fanciful and absurd.
Wafukuzeni tu. Nami nasisitiza, wafukuzwe!!
 
Back
Top Bottom