PreGE2025 Sababu za CHADEMA Kuwatengua Mwita na Catherine zafahamika: Wamesaini waraka wa kupinga ajenda ya ‘No Reform no Election’

PreGE2025 Sababu za CHADEMA Kuwatengua Mwita na Catherine zafahamika: Wamesaini waraka wa kupinga ajenda ya ‘No Reform no Election’

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Nani alifukuzwa kwenye G55? Mzee Omulangira Leopard Lwizandekwe alichukua fomu ya kugombea Urais na Mlw. Nyerere mwaka 1964! Hakufukizwa na mpaka mwaka jana kaadhimisha miaka 95 ya kuzaliwa akiwa amevaa kofia ya CCM!!
Je mwalimu aliyeulizia uhalali wa Samia kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais kupitia ccm bila kupingwa ; kinyume na Katiba yenu hajafukuzwa ccm?
Ccm ya jana sio ya leo iliyojaa mafisadi na chawa!
 
Anafukuza wapambanaji anataka kubaki na kenge wa mtandaoni wasiopiga kura hata akiwaita kuandamana wanajifunika shuka!
Mbona kwenye maandamano ya kudai watu wanaotekwa wakiwemo wana Chadema hao G55 hata mmoja hakupeleka komwe lake..!!
Aliachiwa mbowe peke yake wote walikula njoro..!!

Hiko kipara uanze kukiotesha nywele uenda ukafanikisha msemo wa “Akili ni nywele”
 
Kuna utofauti sana kati ya CCM na vyama vingine vya upinzani kwenye kudeal na hoja tata ndani ya vyama.

Miaka ya 1992 - 1995 liliibuka kundi ndani ya CCM likijiita G55 likiongozwa na Njelu Kasaka na Philip Malmo. Agenda ya kubwa ilikuwa Serikali Tatu kwa maana ya kuitaka Serikali ya Tanganyika.

Hawa G55 wa CCM waliitwa kwenye vikao vya chama na Mwl. Nyerere alikuwa mmoja wa watoa mada ya kwanini Serikali mbili na si tatu. G55 hawakuelewa Somo. Maamuzi ikawa viongozi wao waingizwe kwenye mifumo ya uongozi ili waelewe vizuri maana ya Serikali Mbili. Njelu Kasaka akawa Naibu Waziri na Philip Malmo akawa Naibu Spika na hoja ya G55 ya CCM ikafia hapo! Kwa kifupi CCM ilitumia mbinu ya "Keep your enemy closer"!!!

Kwa upande wa Chadema, wao wameamua G55 wao kuwashughulikia kwa kuwavua vyeo na mchakato wa kuwafukuza uwanachama unaendelea. Halafu wanajiita chama Cha Kidemokrasia. Chama ambacho hakipo tayari kupata changamoto ndani yake. Mbowe asingelikuwa mvumulivu, basi leo Lissu si tu asingelikuwa Mwenyekiti wa Chadema, bali angelikuwa si Mwana Chadema.

Hapo ndipo unaona utofauti wa ukomavu wa kisiasa kati ya CCM na vyama vingine vya upinzani!
Mkuu yaani unatoa mifano miwili tofauti kabisa,Ile ya Kina Njelu miaka ile,Walianzisha wenyewe kakikundi hako na mpango wa Muungano wa serekali mbili wenhgi waliikuta tayari upo kazini.Lakini hawa wahuni wa Mbowe walikuwepo mwanzo mwisho wakati wa Agenda ya NoRENE na walipiga makofi mingi sana wakati Bwana wao akipitisha.Imekuwaje leo wakati wa uongozi wa Lissu watu walewale waone ni Agenda ngeni?
 
Umeisoma Waraka wao vizuri? Nakushauri uurudie kuusoma.
 
Mbona kwenye maandamano ya kudai watu wanaotekwa wakiwemo wana Chadema hao G55 hata mmoja hakupeleka komwe lake..!!
Aliachiwa mbowe peke yake wote walikula njoro..!!

Hiko kipara uanze kukiotesha nywele uenda ukafanikisha msemo wa “Akili ni nywele”
Wewe ulikuwepo..
 
Mgombea bora (5%), ajenda bora (5%), mtandao mpana wa rasilimali watu wenye kuongea lugha moja kabla na wakati wa kampeni (5%), rasilimali fedha na rasilimali vitu za kutosheleza bajeti ya kampeni ya angalau dola moja kwa kila mpiga kura (5%), wapiga kura wenye kiu ya haki na amani (5%), na mfumo wa uchaguzi rafiki (75%).
Good Analysisi.....Well Done My Fellow Learned Dr
 
Ni kweli but ukiwa kiongozi inabidi kuwa mjanja, sometimes usitumie hata madaraka yako ili lengo litimie, mfano tunagombana na CCM sababu ya udikteta wa viongozi wake, ukifanya kitu kilekile hata kama uko sahihi unaleta hisia nyingine ambazo hazihitajiki..ni mpasuko juu ya mpasuko.
Mwaka huu pesa za ccm mtazikula kwa shida sana
 
Back
Top Bottom