Sababu za kuacha kutazama video za utupu

Sababu za kuacha kutazama video za utupu

Gelion Kayombo

Senior Member
Joined
Feb 17, 2018
Posts
149
Reaction score
199
Katika kipindi hiki; kipindi cha mtandao wa intaneti mambo yamebadilika sana kiasi kwamba mtu akiwa na simu au kompyuta yake anaweza kuingia mtandaoni kwenye kila tovuti na kurasa kupitia simu yake au kompyuta yake. Hali ambayo sasa hivi upatikanaji wa taarifa umerahisishwa sana. Mtu anaweza kuingia mtandaoni na kutafuta chochote anachokitaka yeye na kwa muda anaotaka yeye.

Tembelea blog yangu kwa kutafuta Google kwa jina hili Gelion Kayombo kujifunza zaidi makala bora.

Kulingana na urahisi huo wa kupata taarifa kwa urahisi kwenye viganja vya mtumiaji, intaneti imekuja na changamoto zake kwani kwenye intaneti kunapatikana taarifa zote. Ziwe taarifa mbaya; za kubomoa au taarifa nzuri za kujenga.

Ni kutokana na hali
hiyo leo nimeamua kuja na chapisho linalohusu hasara za mtumiaji wa intaneti kama atatumia mtandao wa intaneti vibaya. Ieleweke kuwa ubaya au uzuri wa utumiaji wa mtandao wa intaneti upo mikononi mwa mtumiaji. Kama mtumiaji atatumia vibaya mtandao wa intaneti basi ataharibikiwa na kama atautumia vizuri basi atajengeka.

Ni kutokana na hali hizi mbili za ubaya wa intaneti na uzuri wa intaneti leo nimeamua kuja na chapisho la hasara ya kutumia mtandao wa intaneti vibaya hususani katika eneo la kuangalia picha za utupu(ngono) kwani watu wengi wanaoangalia picha za utupu wanatumia aidha simu zao na kompyuta, na wanatumia kupitia intaneti.

“Kuangalia picha za utupu kuna faida katika malengo ya muda mfupi lakini kwa malengo ya muda mrefu kuna hasara kubwa”. Gelion Kayombo

Watu wengi wanaoangalia picha za utupu na wale waliowahi kuangalia picha za utupu na kufanikisha kuacha kuangalia picha hizo, wakiulizwa swali “Kuangalia picha za utupu kuna madhara”? Wengi watajibu kuwa “Ndiyo kuangalia picha za utupu kuna madhara makubwa”, na wachache watajibu “Hapana kuangalia picha za utupu hakuna madhara”.

Wengi ya watakaojibu kuwa kuangalia picha za utupu kuna madhara ni wale ambao tayari wamekumbana na madhara hayo au walikumbana na madhara hayo na aidha wanaendelea kuangalia picha hizo za utupu au waliacha kuangalia picha hizo.

Na wale watakaosema hakuna madhara ya kuangalia picha za utupu ni wale ambao aidha bado wanaendelea kuangalia picha hizo au wameacha kuangalia. Wanasema hakuna madhara kwa sababu aidha bado wapo kwenye hatua za mwanzo za kuangalia picha hizo hivyo madhara yanakuwa bado hayajaanza kujijenga akilini mwao. Na kama wamefanikisha kuacha mapema kuangalia picha hizo za utupu bila kugundua madhara waliyoyapata basi jua kuwa wanakuwa hawajajichunguza kwa umakini kuangalia madhara waliyoyapata.

Nijuacho mimi kwenye kila kitu unachokifanya lazima kuna matokeo utayapata hata kama ni matokeo madogo. Yawe matokeo mazuri au matokeo mabaya, yawe matokeo makubwa au matokeo madogo. Wakati mwingine ni ngumu kugundua matokeo mapema kwa sababu ya udogo wake, lakini matokeo lazima yatakuwepo ni vile tu hujawa makini kuchunguza kwa umakini kujua matokeo hayo.

Ni mtu pekee aliyewahi kuangalia picha hizo na kupelekea kufanya vitendo vya kujichua ndiye anayeweza kuelezea kwa usahihi madhara yake. Madhara ya kuangalia picha za utupu yanatokea baada ya hatua anazochukua mtu baada ya kuangalia au hatua anazochukua wakati anaendelea kuangalia picha hizo. Watu wengi mara kadhaa wamenieleza madhara waliyoyapata kwa kuangalia picha hizo na hatua walizochukua baada ya kuangalia picha hizo. Yafutayo ni madhara ya kuangalia picha za utupu.

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kujichua(masturbation)

Kuangalia picha za utupu hupelekea akili ya mtu kukosa makali(sharpness) na nguvu

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kukosa nguvu za mwili

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kukosa hali ya kujiamini

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kukosa nidhamu binafsi

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kukwepwa na watu wa jinsia tofauti

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kuwa na msongo wa mawazo

Kuangalia picha za utupu hupelekea mtu kuwa na afya dhaifu


Haya ni baadhi ya madhara ya kuangalia picha za utupu. Na madhara halisi hujitokeza baada ya hatua anazochukua mtu baada ya kuangalia picha hizo. Madhara niliyotaja hapo juu yanatokea baada ya mtu kuanza kuchukua hatua za kujichua nk. Na kama mtu huwa anaangalia picha hizo kujichua ni lazima atajichua. Haya ni baadhi ya madhara ya kuangalia picha za utupu. Kuna madhara mengi ila haya ni baadhi tu. Nimetaja kwa ufupi ila kwenye chapisho lijalo nitaeleza kwa kina kila aina ya madhara ya kujichua niliyo yaandika hapa.

Asante kwa kusoma chapisho hili mpaka mwisho. Nakuomba ndugu msomaji jiunga kwa email na kuruhusu tuwe tunakutumia ujumbe kila tunapoweka chapisho kwenye blog hii.

Gelion Kayombo

Iringa Tanzania.
 
Huo wa huko juu ulishafika na kuuona?
Sijauona ila umetajwa kwenye karibia kila dini. Pia mkuu, tambua kuwa kuna aina mbili za kufanya rejea hapa dunia. Aina ya kwanza unafanya rejea kwa kupitia dini(theology) na aina ya pili ni kupitia Sayansi.
 
Sijauona ila umetajwa kwenye karibia kila dini. Pia mkuu, tambua kuwa kuna aina mbili za kufanya rejea hapa dunia. Aina ya kwanza unafanya rejea kwa kupitia dini(theology) na aina ya pili ni kupitia Sayansi.
Kwenye sayansi ni wapi pameongelewa moto baada ya kifo?
 
Back
Top Bottom