Sababu za Marrian Girls ya Bagamoyo Kung'aa!.


Mimi nadhani hayo makabila yanachanamkia fursa. Yanawaandaa watoto wao kuweza kukabiliana na demand ya Marian Sec School. Ndiyo maelezo ninayoweza kuyapata. Na sidhani wazazi wengi wana mwamko huo!
 

Umesema kweli. Mimi nilisoma Maua 1982-1988 - tulikuwa tunachukua masomo 12 na kila somo kila mwanafunzi alikuwa na vitabu vyake muhimu na maabala ilikuwa well equipped. Ratiba yetu ilikuwa mwisho wa masomo usiku saa 9, kisha manual work, michezo na mwisho wa kujisomosea saa 4 usiku na asubuhi kama mtu anataka kuamka ni kuanzia saa 12. Pamoja na hayo, tulihimizwa sana kufanya kazi (manual work), michezo na social events kama English debate na shule zingine mkoani Kilimanjaro + kila mwaka wanafunzi wa Kidato wa IV walikuwa na study tours kutembelea mashamba ya ngano, mifugo kule West Kilimanjaro maana shule yetu ilkuwa inachukua mchepuo wa Kilimo (Kilimo + mifugo).

Tuliweza pia kutembelea kila mwaka bandari ya Mombasa kujifunza jinsi meli zinavyotua, kupakia mizigo nk na Kiwanda cha Korosho Bamburi na pia kujifunza kuhusu 'land reclamation'. Hapo Bamburi zamani ilikuwa nusu jangwa lakini mwekezaji mmoja aliweza kubadilisha na kuifanya fertile land kwa kuweka majongoo aliyoyakuwa akiyakusanya kutoka visiwa vya Bahari ya Hindi na yalipooza yalitengeneza udongo na kuanza kuotesha mimea na kufuga wanyama mbalimbali. Mambo mengine tuliyoyafanya nje ya masomo ni kujifunza music [kusoma notes, kucheza flute, kinanda, gitar, piano, kodiani (sijui nimepatia spellling), kupiga ngoma, kuigiza], kutengeneza matofali, ku'service machine' mfano trekta etc, kufuga nyuki, kufanya survey (kama wanavyofanya wapima barabara), grafting, sauna bath, kuogelea etc.

Hivyo, mtu akimaliza Maua alikuwa na elimu karibu ya kila kitu na kila kitu mwanafunzi anajifunza kwa kuona mfano kwa somo la geografia kuhusu erosion inayosababishwa na mto tulikuwa tunaenda kwenye mto kuona inafanyika namna gani. Pia tulikuwa tunatembelea bwawa la Nyumba ya Mungu, Crater Lake (Ziwa Jipe) na kupanda mlima Kilimanjaro maana Maua ilikuwa inatoa huduma kwa wale wanaopanda mlima Kilimanjaro kama huduma ya nguo za baridi, groves na viatu vyake. Ila ukitoka kwenye mazingira kama haya uende sehemu ambayo inabidi uibie mitihani, umhonge mwalimu, kupata maksi mpaka ujikombe kwa mwalimu wa somo nk, of course, utafeli tena sana!

Msingi huu umefanya elimu ya kilimo, utunzaji wa mazingira, ujenzi, carpentry, ufugaji nk ibaki kwenye damu yangu hadi leo.
 

Hawa watoto wa kishua wanaosoma katika shule hizi, mwisho wao wa kuwakilisha unaishiaga katika Vyuo Vikuu. Tulianza nao pale Muhimbili, wengi waliliwa vichwa katika Semister ya kwanza tu, na wengine wengi walikimbilia mzumbe! tukabaki sisi watoto wa uswazi tuliotokea Kibaha, Mzumbe, Ilboru na Pugu boyz. Ni mbwembwe tu! whatzup nyingi!
 

hv ratio zpo sawa???? wanaoingia chuo na kufeli kutoka vipaji na saint.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…