Sababu za msingi zinazopelekea 'afande' wa ulawiti asikamatwe ni hizi?

Ilikuwa ni kusababisha au kuhamasisha mkuu. Wewe unadhani kusababisha na kuua ni sawa? Ndio maana nimesema kusababisha, kumtuma muuaji au kuhamasisha mauaji sio kosa kisheria. Isipokuwa yule anayehusika kuua moja kwa moja ndiye mwenye makosa.
Futa Uzi mpuuuzi huna unalojua zombe na mke wa msuya walipona kutokana na kukosekana ushahidi usio acha Shaka. Na sio kwa sheria hizo za ujinga ujinga unazo sema wewe
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka,
Kama sheria haitambui mtu aliyetuma watu kutekeleza uhalifu inakuaje wale wanaotuma watu kufanya maandamano au kukusanya watu kwa namna moja ama nyingine kwa lengo flani la kuandamana wanakamatwa .?

Je, anayechochea (mchochezi) jambo kwa wanachokiita ni kinyume na sheria na anayemtuma mtu kufanya uhalifu kunatofauti gani?
 
Soma vizuri nilichoandika
 
Hapo kikubwa case iishe tu, yule mtoto aliutaka na hilo liwe fundisho kwake.

Familia zinalala njaa watoto hawasomeshwi, Mama zao wanatelekezwa sababu ya hawa malaya chipukiz wa elfu mbili wanajiita GenZ wa tz.

Binafsi naona hatia ipo kwa waliotekeleza ubakaji hasa yule mwamba wa kutifua mtaro, bj na Camera man. Mama wa watu hana hatia kabisa alitoa hukumu ya haki.
 
Alitakiwa kukamatwa na hao wafiraji wengine na wote wawe sehemu ya kesi hiyo hadi mahakama itakapotamka vinginevyo.
Kumbuka:
hukumu hutolewa na mahakama na sio mapolisi!
 
Sio kweli boss!
Kimsingi kesi ulizotaja kama mfano ni tofauti na kesi ya binti! Katika kesi zako za mfano hakuna ambayo victim ali survive hivyo hakuna testimony from the victim.

Katika kesi ya binti, victim yupo hai and she is a competent witness to testify! Na kumbuka kuwa katika kesi za ubakaji ushahidi wa victim is the best evidence mahakamani.

Tofauti na kesi zako za mfano, kwenye kesi hii kuna kitu kinaitwa ACCESSORY TO/BEFORE THE EVENT, huyo mama mtumaji anaingia vizuri tu. Vipi kuhusu CONSPIRACY?

Changamoto ninayoiona ni uvivu au njama za waendesha mashtaka kuandaa charges mbovu ambazo zinaacha counts nyingi za kum pin mtuhumiwa!
Ukitaka uone moto, kesi hii wapewe mawakili wa kujitegea, waandae kuanzia mashtaka hadi prosecution mahakamani dhidi ya watuhumiwa, hachomoki mtu hapo! Hiyo sio kesi ya kupeleka charges mbili tu mahakamani!
 
Mimi sio mwanasheria lakini nafahamu mambo ya kisheria kidogo mkuu
Hata kama Kuna legal loopholes ya kumtia hatiani 'afande' kiu ya watu ni kama kwa Zombe aonekane hadharani na mahakama ya umma iatamuhukumu .
Pili kwani hawezi kushitakiwa kijeshi na kuhukumiwa kwa uvunjaji mkubwa wa maadili na at least afukuzwe kazi?
 
Arguments nzuri lakini precedents ulizoweka haziko consistent.

Kikubwa ni kupata ushahidi kwamba kweli walitumwa, mara nyingi anaetoa contract au kuwatuma anarekodiwa. Wanaachiwa pale ambapo kunakuwa hakuna ushahidi mahili kwamba walitoa maagizo. Huyo afande alituma watu wakabake, akisema si kweli, kuna ushahidi gani kwamba aliwatuma? Haiwezi kuwa suala la their word against her word, lazima kuwe na kitu kinaitwa substantiating evidence kwamba aliwatuma, mfano malipo, au walimrekodi nk. La sivyo huwezi kumfungulia mashitaka.

Nyerere alimuuliza mwandishi wa habari Nairobi, tu akikuambia mimi ni baba yako, kwamba nilitembea na mama yako ndio ukazaliwa, utamuamini kwa kuwa tu amesema hivyo?
 
Mkuu umetoa ufafanuzi uliojitosheleza. Mtoa hoja huenda ana maslahi na kesi hii. Huenda ana ujamaa na huyo afande mtuhumiwa. Kwani hata akipelekwa mahakamani na kwa bahati akachoomoka, polisi watapata hasara gani. Huwa wanawambabikiza kesi viongozi wa upinzani kwa makesi ya kijinga ambayo huwa hayana mashiko mahakamani.
 
Mkuu nikusahihishe kidogo sheria yetu inatambua kwamba hata aliyetuma nae ametenda kosa sawa na waliofanya under penal code ndio maana zombe na mama msuya walikutwa na hatia
Ila kilichowaokoa ni mahakama ya rufaa, na mahakama ya rufaa haiangalii facts ila makosa ya kisheria kwenye kuwatua hatiani au kutoa hukumu
Case zote mbili ulizotaja polisi walivuruga kwenye kuunganisha ushahidi na hilo ni kosa kisheria na hukumu inakuwa batili ,na sio kwamba sheria haitambui aliowatuma kama ulivyoiweka wewe
 
Siyo kweli kwamba "Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni."❌❌❌

Aliyehusika kufyatua risasi ni Saad ambaye alifariki wakati kesi inaendelea.

Kwa kuwa marehemu Saad ndiye ndiye mtenda kosa mkuu, hao wengine, akiwemo Zombe hawakuweza kutiwa hatiani Kwa sababu katika kesi za makosa ya ushirika, mhalifu mtenda kosa namba moja asipopatikana mahakamani au asipopatikana na kosa, basi wengine wote wanaachiwa.

Sababu ya kuachiwa ni kwamba huwezi kusema washirika Wana makosa wakati muongoza uhalifu hajapatikana na hatia.

Kwenye jinai, kama umeshiriki Kwa namna yeyote ile sheria inakutia matatani. No excuse!
 
KINDEENA na wewe acha UONGO,aliyefyatua Risasi kuwaua wale wafanyabiashara wote na dreva wao ni Koplo Saad Ally na hakuwahi kupatikana mpaka leo. Aliyefia Mahabusu wakati Kesi inaendelea ni Koplo Rashid Lema.
Bahati nzuri hao wote nawafahamu maana nilifanya nao kazi
 
Zombe kafa lini?
 
Kwa maana hiyo, kufadhil ugaidi sio, kufadhili mauaji sio kosa, kufadhili uhaini siyo kosa au
Huyo Afande anapaswa kuunganishwa kwenye Kesi hii kwa sababu ni accessory for the crime.
Kuhusishwa kwa namna yoyote ile kwenye shughuli au matukio ya njama za kupanga Uhalifu, unakuwa sehemu mojawapo ya Uhalifu huo. Aunganishwe kwenye Kesi hii ili aende akajitetee yeye mwenyewe huko Mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…