Sababu za msingi zinazopelekea 'afande' wa ulawiti asikamatwe ni hizi?

Polisi wanapaswa kujua kwamba Amri yoyote inatolewa na kiongozi wake wa kazi haijalishi ana cheo gani ya KUUA/KUBAKA/KULAWITI/KUTEKA Raia wa TANZANIA ni AMRI BATILI.

Na msalad ukibumburuka utadakwa wewe ulitekeleza hio amri sio aliyeitoa.

Yeye atahamishwa tu kutoka ofisi Moja kwenda nyingine.

Wewe utaenda kunyea DEBE/MTONDOO.

So kabla ya kutekeleza amri za kikatlli fikiria kwanza.

Ni heri ukufuzwe kazini Kwa kutotii amri BATILI kuliko ugeuzwe status kuitwa mfungwa/mtuhumiwa/muuaji na hatis haitokuacha ikiwa utamwaga damu ya watu.

HATA POLISI WANAPASWA TAMBUA KUWA HAWAPO SALAMA ANYTIME MSALA UTAKUPATA WATZ WAKIAMUA

utaicha familia kitaa Raia wanakusaidia mkeo.

Usiwe baba au mama mpumbavu.
Watakuelewa basi... Na wakati wao wakifanya hayo maukatili yao ndo wanajiona miamba kumbe wapuuzi tu 😂
 
Mtoa mada pengine umesahau kipindi kesi ya zombe kuna mashahidi muhimu waliuawa ili kuficha ushahidi, bila baadhi ya mashahidi kufa ni vigumu sana kuchomoka ndiyo maana watu tunataka huyo afande apande kizimbani haijalishi atachomoka au anafungwa.
Hata huyo zombe hakuishi Kwa Amani Hadi anakufa Kwa kifupi ni kama alikuwa jela tu
Ili haki ionekane imetendeka lazima Afande aliyefadhili hiyo show naye afikishwe Mahakamani, huko ndiyo Mahakama ikamsafishe na kumpulizia manukato kabisa kuwa ni mtu safi lakini asipoguswa kabisa itakuwa uonevu tu.
 
Mkuu usiwe buh lawyer. Unafikiri kwanini Zombe na mke wa Msuya au wahalifu waliotumwa na mke wa Msuya (na fingerprints zao zikapatikana kwenye visu vilivyotekeleza mauaji) hawakutiwa hatiani?
Kutiwa hatiani hasa kwenye criminal cases inahitaji mtu ku prove beyond reasonable doubt.

Kesi ya mke wa Msuya hakuna ushahidi usioacha shaka kwamba aliwatuma ndiyo maana akaachiwa huru.

Lakini endapo jamhuri ingethibitisha pasipo kuacha shaka kwamba alishiriki kwa namna moja ama nyingine kwenye mauaji lazima angekuwa criminally liable.

Hivi ni kweli hata kwa akili ya kawaida tu hujui hata mtu aliyeshiriki tu kula njama za kutenda uhalifu hata kama yeye hakwenda eneo la tukio kisheria ni mmoja wa wahusika wa uhalifu?

Sasa wewe panga njama za tukio la ujambazi wape vijana silaha na vitu vya kuwawezesha kutenda ujambazi halalfu wewe kaa nyumbani then kwenye ushahidi ukatajwa kama mfadhili mkuu wa uwezeshaji wa kutendeka kosa la ujambazi kama hujakwenda na maji as far as ushahidi uwe concrete na usioacha shaka.
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.

Jambo la kushangaza na ambalo watanzania wengi wanashindwa kupata majibu ni kwanini 'afande' aliyewatuma wale wahuni (na ambaye alisikika akiombwa msamaha na binti aliyekuwa akibakwa na kulawitiwa mubashara) hakamatwi? Swali la pili ni je, wale watuhumiwa 2 wa ulawiti waliobaki ni akina nani na kwanini hawakamatwi? Je, wana uhusiano wowote na huyo afande asiyekamatika? Hiki ndicho kitendawili ambacho watanzania wangependa kupata majibu yake.

Kabla ya kutoa majibu na kueleza kwanini afande hakamatiki, naomba nirejee kesi 2 zinazofanana na hii ya afande zilizowahi kufikishwa mahakamani na kugonga mwamba.

Kesi ya kwanza ni ile ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa Dar es Salaam, ndugu Abdallah Zombe ambaye aliwatuma askari polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora mamilioni ya fedha. Kwa ufupi, kesi ilipotinga mahakamani, wale askari waliotumwa kuua walijitetea kuwa walifanya mauaji yale kwa kutii amri ya mkubwa wao wa kazi, ndugu Zombe. Baada ya kesi kuunguruma kwa muda mrefu, huku wananchi wakidhani Zombe hachomoki kwenye kesi ile, hatimaye aliachiwa huru. Wale askari waliohusika na mchakato wa mauaji wakahuhumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa. Lakini baadaye askari wale walikata rufaa na baadhi yao kufanikiwa kujichomoa. Aliyekutwa na hatia ni mmoja wao anayeitwa Bageni, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Katika kesi hii kuna facts mbili za kisheria zilizotumika. Fact ya kwanza ni ile ya mtu mzima mwenye akili timamu kutumwa na mtu mwingine kutekeleza uhalifu. Sheria haimhukumu aliyetuma bali humhukumu mtumwaji, hata kama mtumaji anajulikana na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli aliwatuma. Ndio maana Zombe aliachiwa huru bila shuruti.

Fact ya pili katika kesi hii ni uhusika wa mtu binafsi katika kutenda uhalifu. Baadhi ya askari waliachiwa huru kwa kuwa hawakuhusika kuwapiga risasi wafanyabiashara. Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni. Ndio maana askari wengine waliachiwa huru, akahukumiwa Bageni tu.

Turejee kwenye kesi ya pili iliyomhusu mke wa Bilionea Msuya kuwatuma watu kumuua wifi yake (mdogo wake bilionea Msuya). Mahakamani ilithibitika kweli mke wa bilionea Msuya aliwatuma watu kufanya uhalifu. Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?

Sasa turejee kwenye hoja yetu ya msingi. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii (sio JF) imemtaja na kumuonesha hadharani afande aliyewatuma wale wafiraji kumdhulumu binti wa watu haki yake ya msingi. Pia haiwezekani binti aliyedhulumiwa amuombe afande msamaha hadharani halafu polisi wasimuombe awapeleke nyumbani kwa afande ili wamkamate. Haiwezekani.

Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti. Kwa hiyo, polisi wanaona hata kama wakiamua kumpeleka afande mahakamani wataambulia patupu. Illmradi wahalifu wamekamatwa, hakuna haja tena ya kusumbuka na afande kwa kuwa hata akipelekwa mahakamani, hana kesi ya kujibu.

Sheria inatambua kwamba mtu mzima unapotumwa kutenda uhalifu nawe ukakubali kufanya hivyo, sheria itakuangukia wewe uliyetenda uhalifu na wala sio mtu aliyekutuma. Kwa hiyo, watanzania, hasa wale msiojua sheria, tulizeni mumkari na muendelee kuwa watulivu wakati wabakaji na wafiraji waliohusika kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Nawasilisha.
Kwani zile Kesi zinazosema Watuhumiwa wote Kwa pamoja walikula njama za kutenda Uhalifu wa kudhilumu binti kimapenzi hazipo?
Yule Mama alikula njama ya Kurgans ze kundi la wahalifu ili kutekeleza kosa la ubakaji, hivyo ashtakiwe Kwa kuunda genge la kutekeleza uhalifu
 
Mkuu usiwe buh lawyer. Unafikiri kwanini Zombe na mke wa Msuya au wahalifu waliotumwa na mke wa Msuya (na fingerprints zao zikapatikana kwenye visu vilivyotekeleza mauaji) hawakutiwa hatiani?
Kama upo kwenye profession ya sheria jisomee sana case laws na sheria mbalimbali utagundua hiki ninachokwambia.

Hata Penal Code yetu nadhani section 387 ama around hapo sina uhakika kuna mtu anaitwa accessory after the fact jinsi anvyohusika kama mhalifu ingawaje hakuwepo kabisa kwenye commission of an offence lakini ushiriki wake tu in connection with a criminal offence anakuwa criminally responsibility.
 
Leo umeandika fact sana mkuu. Umejitofautisha sana na wale wasiojua sheriabza nchi.

Kwa vile umeandika fact za kisheria naomba nikupe na picha ya jana ambayo nilitaka kuiandikia uzi mfupi kutoa watanzania tongotongo.

FB_IMG_1724140710802.jpg

Picha moja ila moja imefichwa sura na nyingine wazi
FB_IMG_1724140528134.jpg
 
We jamaa mbona nakumbuka tulisomaga kula njama ni kosa na lina hukumu kabisa?

Ile topiki ilikua inaitwa "conspiracy in criminal law in tz"
Hapo sasa ndipo unapaswa uchekeche kichwa zaidi ufahamu ni kwanini mke wa Msuya na Zombe waliaachiwa huru kwa sheria hizo hizo ulizosoma wewe.
 
Leo umeandika fact sana mkuu. Umejitofautisha sana na wale wasiojua sheriabza nchi.

Kwa vile umeandika fact za kisheria naomba nikupe na picha ya jana ambayo nilitaka kuiandikia uzi mfupi kutoa watanzania tongotongo.

View attachment 3074736
Picha moja ila moja imefichwa sura na nyingine wazi
View attachment 3074737
Asante sana kwa nondo hii muhimu sana mkuu. Ubarikiwe mno.
 
Daah! Inauma sana kwa
Leo umeandika fact sana mkuu. Umejitofautisha sana na wale wasiojua sheriabza nchi.

Kwa vile umeandika fact za kisheria naomba nikupe na picha ya jana ambayo nilitaka kuiandikia uzi mfupi kutoa watanzania tongotongo.

View attachment 3074736
Picha moja ila moja imefichwa sura na nyingine wazi
View attachment 3074737
Kuna kitu gani hapa kimejificha mkuu?
 
Muanzisha Uzi umeongea UONGO kwenye Kesi ya Zombe.Christopher Bageni(aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Oysterbay)alihukumiwa kunyongwa lakini sio yeye aliyefyatua Risasi kuwaua wale Wafanyabiashara. Aliyefyatua Risasi ni Askari alikuwa anaitwa Koplo Saad Ally na si Bageni.Na huyo aliyefyatua Risasi kuwaua wale wafanyabiashara Koplo Saad Ally hakuwahi kupatikana mpaka leo. Kilichofanya Bageni ahukumiwe kunyongwa ni kwamba yeye kama Mkuu wa Upelelezi alikuwepo mpaka eneo la tukio kule kwenye mauaji(msitu wa pande),hivyo alikuwa na uwezo wa kuzuia mchakato mzima. Kilichomuokoa Zombe ni kutokuwepo eneo la tukio. Lakini pia kukosekana mawasiliano ya kwenye Mtandao wa siku kuonyesha kwamba siku ya tukio alikuwa anampa maelekezo Bageni ya kuwaua wale wafanyabiashara(mawasiliano kutoka VODACOM yalikuwa yameshafutwa kwa mujibu wa Sharia baada ya kukaa miezi 6). Aliyefia Mahabusu alikuwa anaitwa Koplo Rashid Lema.
Jitahidi kufanya research kabla ya kuandika uongo
 
Kesi ya zombie ilikua ni kufanya mauji dhidi ya wafanyabiashara au kusababisha mauaji dhidi ya wafanyabiashara ?
Ilikuwa ni kusababisha au kuhamasisha mkuu. Wewe unadhani kusababisha na kuua ni sawa? Ndio maana nimesema kusababisha, kumtuma muuaji au kuhamasisha mauaji sio kosa kisheria. Isipokuwa yule anayehusika kuua moja kwa moja ndiye mwenye makosa.
 
Daah! Inauma sana kwa

Kuna kitu gani hapa kimejificha mkuu?
Ziangalie picha vizur
Picha moja imezibwa macho
Picha ya pili haijazibwa macho.

Aloziba macho amechukua tahadhari maana bado walengwa ni watuhumiwa wa kosa tajwa
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
View attachment 3074754
Watuhumiwa 4 waliombaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakiwa mahakamani

Jambo la kushangaza na ambalo watanzania wengi wanashindwa kupata majibu ni kwanini 'afande' aliyewatuma wale wahuni (na ambaye alisikika akiombwa msamaha na binti aliyekuwa akibakwa na kulawitiwa mubashara) hakamatwi? Swali la pili ni je, wale watuhumiwa 2 wa ulawiti waliobaki ni akina nani na kwanini hawakamatwi? Je, wana uhusiano wowote na huyo afande asiyekamatika? Hiki ndicho kitendawili ambacho watanzania wangependa kupata majibu yake.

Kabla ya kutoa majibu na kueleza kwanini afande hakamatiki, naomba nirejee kesi 2 zinazofanana na hii ya afande zilizowahi kufikishwa mahakamani na kugonga mwamba.

Kesi ya kwanza ni ile ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa Dar es Salaam, ndugu Abdallah Zombe ambaye aliwatuma askari polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora mamilioni ya fedha. Kwa ufupi, kesi ilipotinga mahakamani, wale askari waliotumwa kuua walijitetea kuwa walifanya mauaji yale kwa kutii amri ya mkubwa wao wa kazi, ndugu Zombe. Baada ya kesi kuunguruma kwa muda mrefu, huku wananchi wakidhani Zombe hachomoki kwenye kesi ile, hatimaye aliachiwa huru. Wale askari waliohusika na mchakato wa mauaji wakahuhumiwa vifungo vya maisha na kunyongwa. Lakini baadaye askari wale walikata rufaa na baadhi yao kufanikiwa kujichomoa. Aliyekutwa na hatia ni mmoja wao anayeitwa Bageni, ambaye alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Katika kesi hii kuna facts mbili za kisheria zilizotumika. Fact ya kwanza ni ile ya mtu mzima mwenye akili timamu kutumwa na mtu mwingine kutekeleza uhalifu. Sheria haimhukumu aliyetuma bali humhukumu mtumwaji, hata kama mtumaji anajulikana na yeye mwenyewe kukiri kuwa kweli aliwatuma. Ndio maana Zombe aliachiwa huru bila shuruti.

Fact ya pili katika kesi hii ni uhusika wa mtu binafsi katika kutenda uhalifu. Baadhi ya askari waliachiwa huru kwa kuwa hawakuhusika kuwapiga risasi wafanyabiashara. Aliyehusika kufyatua risasi na kuua ni mmoja tu, naye ni Bageni. Ndio maana askari wengine waliachiwa huru, akahukumiwa Bageni tu.

Turejee kwenye kesi ya pili iliyomhusu mke wa Bilionea Msuya kuwatuma watu kumuua wifi yake (mdogo wake bilionea Msuya). Mahakamani ilithibitika kweli mke wa bilionea Msuya aliwatuma watu kufanya uhalifu. Na pia kisu kilichotumika kufanya mauaji kilipatikana na alama za vidole za wahalifu. Lakini mahakama ilitumia busara za kisheria kuwaachia huru watuhimiwa wote, akiwemo mke wa Msuya. Kwanini? Kwa sababu mtumaji hana kosa kisheria. Pia hata kama fingerprints za wahalifu zilionekana kwenye kisu, hakuna mtu mwenye uhakika kama kweli wao ndio waliua. Umeona eeh?

Sasa turejee kwenye hoja yetu ya msingi. Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii (sio JF) imemtaja na kumuonesha hadharani afande aliyewatuma wale wafiraji kumdhulumu binti wa watu haki yake ya msingi. Pia haiwezekani binti aliyedhulumiwa amuombe afande msamaha hadharani halafu polisi wasimuombe awapeleke nyumbani kwa afande ili wamkamate. Haiwezekani.

Ni wazi kwamba afande anajulikana isipokuwa hata kama atakamatwa hatakuwa na kesi ya kujibu, kwa kuzingatia mfano wa kesi mbili nilizozitaja hapo juu ambazo watumaji waliachiwa huru bila shuruti. Kwa hiyo, polisi wanaona hata kama wakiamua kumpeleka afande mahakamani wataambulia patupu. Illmradi wahalifu wamekamatwa, hakuna haja tena ya kusumbuka na afande kwa kuwa hata akipelekwa mahakamani, hana kesi ya kujibu.

Sheria inatambua kwamba mtu mzima unapotumwa kutenda uhalifu nawe ukakubali kufanya hivyo, sheria itakuangukia wewe uliyetenda uhalifu na wala sio mtu aliyekutuma. Kwa hiyo, watanzania, hasa wale msiojua sheria, tulizeni mumkari na muendelee kuwa watulivu wakati wabakaji na wafiraji waliohusika kumdhalilisha binti wa Yombo Dovya wakishughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Nawasilisha.

Kesi za uhaini kwa nini hujumuisha waliotuma pia. Hiyo si ndio kupanga na kula njama. Hapa umetunoa sema labda sheria sio msumeno ukatao mbele na nyuma basi.
 
Tunafahamu hayo, tunafahamu hakuna uhakika wa kupatikana kwa ushahidi against “Afande” tunachotaka ni kila mhusika aliyehusika kwa namna moja au nyingine consequence imfikie.

Ukimshitaki mtu hata kama hukumu haitomtia hatiani kuna kitu unakuwa umempunguzia, ikiwemo reputation.

Usifikiri wanaopush hilo hawajui, Namna ya kupata haki haijanyooka, but in the end kila mtu aumizwe, tuumie wote ili tujifunze kutendeana kwa usahihi.

Tunaishi Africa.
 
Hili ndo nilikuwa nasema watu wanataka watu wapandishwe kizimbani kwa mihemko tu hawajui mahakamani ni ushahidi usio shaka ndo unasimama, kwa hiii kesi kumkuta na hatia huyu mama ni kazi sana maana inabidi ueleze kinaga ubaga chain yake na hao watu na uthibitishe kuwa yeye aliwatuma jambo ambalo si rahisi. Hii dunia ya mitando ni ngumu sana kwenda nayo maana kila mtu ni mtaalam na hisia ni bora zaidi kuliko ukweli
Atleast apelekwe mahakamani huko aonekane hana hatia.
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.

Nawasilisha.

Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
View attachment 3074754

Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Wiki hii tumeshuhudia vijana 4 kati ya 6 waliofanya uhalifu wa kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakifikishwa mbele za Pontio Pilato na kusomewa mashtaka, ijapokuwa walikana kuhusika na kitendo hicho kibaya.
View attachment 3074754
Watuhumiwa 4 waliombaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya wakiwa mahakamani
Sikubaliani na wewe kuwa mtu akikutuma mtu mzima ufanye uhalifu ni huyo aliyefanya tu ndo atawajibika na sio aliyekutuma. Section 22 (1) ya the Penal Code (Kanuni ya Adhabu)[CAP 16 R.E 2022] inaprovide kwa kitu kinaitwa principal offenders. Ukisoma sasa 22 (1) (d) Yeyote aliyecounsel au kuprocure naye anaweza kushtakiwa kwa kosa hilo lililotendeka au kwa kosa ya procuring au counseling.

Sasa kumwagiza mtu afanye uhalifa hiyo ni kuprocure na hivyo mtu anayeprocure naye anaingia kuwa mtendaji kosa. So inawezekana kabisa aliyeagiza kosa lifanyike akashtakiwa vizuri tu ingawa atakutwa na hatia au la ni suala la ushahidi. Ndio mana kilichomuokoa Zombe kwenye kesi hiyo ni kuwa muda wa kustore mawasiliano ya simu ulikuwa ushapita na hivya ikawa ngumu kumlink Zombe kama ni ndo yule aliyekuwa anatoa order. Pia kesi hii ya Zombe inatoa mwangaza juu ya hiyo section 22 ya Penal Code.
 
Back
Top Bottom