Sababu za ndege kumwaga mafuta angani

Mr pianoman

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2019
Posts
2,595
Reaction score
6,264
Ndege kumwaga mafuta angani kitaalamu #FuelDump au #Jetsoning ni utaratibu wa dharura unaofanywa na rubani kutoa mafuta nje ya tanki za ndege ikiwa angani.

Mara nyingi ndege kubwa na za kati zina uwezo wa kumwaga mafuta angani kupitia tundu maalumu '#Nozel' zilizopo nyuma ya mbawa endapo itapatwa na dharura inayohitaji kutua haraka hasa pale muda mfupi baada ya kupaa.

Kwanini muda mfupi baada ya kupaa?
Kwasababu mafuta yanakuwa bado ni mengi hivyo ndege kuwa na uzito mkubwa unaopitiliza mipaka ya usalama wake kwenye kutua.

Ndege nyingi huwa zina uwezo wa kupaa na uzito mkubwa kuliko uzito wa kutua kwakuwa mkandamizo au 'stress' za ndege wakati wa kutua ni kubwa kuliko wakati wa kupaa.

Pia mafuta hujazwa mengi kwasababu ya masafa (hasa marefu) kule inapoelekea hivyo huitaji,
>Mafuta ya safari husika,
>Mafuta ya kuzunguka angani kusubiri kama kuna dharura,
>Mafuta ya kwenda kutua uwanja wa ndege mwengine endapo kuna dharura katika uwanja uliopangwa kutua awali n.k

Kwahiyo ndege husika inapopata dharura muda mfupi baada kupaa rubani analazimika kupunguza mafuta angani katika eneo salama atakaloona au kuelekezwa na waongoza ndege ili kurudi kutua na uzito salama kuepuka hatari kama kupasuka tairi, kuharibu miundombini ya barabara #runways, kutosimama mapema au kupitiliza nje ya barabara yake 'runway', kutua kwanguvu #hardLanding, kuipa udhaifu/'#stress, kupinda au kuvunja maungio ya kiwiliwili cha ndege husika au kusababisha ajali kabisa.

Umwagaji mafuta mara nyingi ufanyika katika umbali maalumu kwenda juu na nje ya makazi ya watu au baharini.

Umbali wa kwenda juu kidogo husaidia mafuta hayo kutawanyika hewani na kupotea na upepo au kufika chini kama mvuke hafifu usio na madhara sana.

Kumbuka usifananishe kwani umwagaji mafuta huu pia unaacha mistari ya mvuke isiyodumu nyuma inayotaka kufanana kidogo na ile hali michirizi ya wingu inayoganda na baridi (#condensation) pale ndege inakuwa kimo cha juu sana ambayo wengi huita roketi kimakosa.
 
I am today years old ndiyo nimejua wakati wa utotoni zile ndege tulizokua tunaita ndege za Urusi actually ni ndege zinakua zinamwaga mafuta.

This just made me hungry.
Kumbuka usifananishe kwani umwagaji mafuta huu pia unaacha mistari ya mvuke isiyodumu nyuma inayotaka kufanana kidogo na ile hali michirizi ya wingu inayoganda na baridi (#condensation) pale ndege inakuwa kimo cha juu sana ambayo wengi huita roketi kimakosa.

Ulikuwa sahihi utotoni.
 
Kwahiyo mkuu zile sio rocket zinachana mawinguni?

Sijui mwanangu akiona hii post atanichukuriaje[emoji30][emoji30][emoji30]. Maana anajua ni rockets
[emoji23][emoji23] Kawaida tu hiyo mkuu mbona hata sisi kipindi tunakuwa tukimkuta mama kajifungua mtoto mchanga ukimuuliza anakwambia ame mnunua dukani [emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23] Kawaida tu hiyo mkuu mbona hata sisi kipindi tunakuwa tukimkuta mama kajifungua mtoto mchanga ukimuuliza anakwambia ame mnunua dukani [emoji23][emoji23]
Ila anaweza kuona kilaza au hujui.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
aiseee!since nimezaliwa leo ndo najua hili jambo πŸ˜‚salaaalee! watu tulishazoea kusema ni rockets kumbe ni mafuta yanayo mwagwa kutoka kwenye ndege...πŸ˜‚πŸ˜‚ Shukran mkuu kwa taarifa...
 
Kwahiyo mkuu zile sio rocket zinachana mawinguni?

Sijui mwanangu akiona hii post atanichukuriaje[emoji30][emoji30][emoji30]. Maana anajua ni rockets
Hahaha ataona ana dingi kilaza.

God save us
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…