Sababu za ndege kumwaga mafuta angani

Sababu za ndege kumwaga mafuta angani

Hapa Africa hakuna mtu ashawahi ona rocket. Hakuna range ya rocket kabisa na ndo maana tangu ajari za rockets zitokee hujawahi sikia eti limedondoka au debris zake zimedondoka kwenye makazi ya watu. Nchi zenye rockets ni U.S, Russia, China, India, Japan, Europe hawa wana shirika la pamoja nchi kadhaa, Ukraine sijui kama bado wataendelea, na Iran hivi karibuni. Sijui kama nimeacha nchi zaidi ya tatu. Hakuna range ya rocket kuonekana huku Africa.
Rocket zinanyanyuka direct vertically zikiwa zimelala nyuzi kidogo.

Kwenye mafuta ya ndege. Fuel dumping hufanyika karibu na airport/base na mara nyingi katika kuzunguka. Kumbuka ndege inakuwa katika hali mbaya hivyo itatua hivi karibuni.
Pia kingine mleta mada hajaongeza, kumwaga mafuta husaidia kupunguza moto endapo ndege itaungua ikipata ajari katika kutua.
Kwa hiyo rocket ikinyenyuka mwendo wa wima haiendi haibadirishi kwenda ulalo
 
Daaah cjui nani alitutengenez huu uvumi kwamba zile zinazopita juu. Na kuacha trails ni rockets..zile ni ndege za kawaida..though zinapita anga la juu sana ambalo kama wadau walivosema kuna mgandamizo mkubwa...rockets.kwa africa kwa kweli amna nchi inayoeza kufanya project hyo.ko hazipo..jaman nani anakumbuka kuna watu walikua wanasema eti zile rocket zinatuaga south Africa tu..hahahaha...utoto bna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kutudanganya mkuu. Nimesoma topic ya physics ya advance ya rocket propulsion

Embu google hapo rocket propulsion utaelewa kitu kingine tofauti na cha mtoa mada. Hiyo topic nimeisoma advance naielewa kuliko mtoa mada. Rocket huwa zinatoa moshi mwingi nyuma kwenye mawingu ya juu yale sio mafuta.

Force of rocket = (dm/dt) X velocity
dm/dt inaendana sanjali na mafuta yanayo unguzwa na moshi unaotolewa nyuma ya rocket hivyo ndivyo speed yake huongezeka.
Ka mtoa mada make generalize kitu ambacho sio kweli.
Mkuu nafikiri umekurupuka hizo physics siyo ww tuu uliyesoma alichokieleza mtoa mada na unachokisema ni vitu viwili tofauti.

Nafikiri muda mwingine jitahidi kuwa makini katika kuelewa .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
I am today years old ndiyo nimejua wakati wa utotoni zile ndege tulizokua tunaita
Ndege kumwaga mafuta angani kitaalamu #FuelDump au #Jetsoning ni utaratibu wa dharura unaofanywa na rubani kutoa mafuta nje ya tanki za ndege ikiwa angani.

Mara nyingi ndege kubwa na za kati zina uwezo wa kumwaga mafuta angani kupitia tundu maalumu '#Nozel' zilizopo nyuma ya mbawa endapo itapatwa na dharura inayohitaji kutua haraka hasa pale muda mfupi baada ya kupaa.

Kwanini muda mfupi baada ya kupaa?
Kwasababu mafuta yanakuwa bado ni mengi hivyo ndege kuwa na uzito mkubwa unaopitiliza mipaka ya usalama wake kwenye kutua.

Ndege nyingi huwa zina uwezo wa kupaa na uzito mkubwa kuliko uzito wa kutua kwakuwa mkandamizo au 'stress' za ndege wakati wa kutua ni kubwa kuliko wakati wa kupaa.

Pia mafuta hujazwa mengi kwasababu ya masafa (hasa marefu) kule inapoelekea hivyo huitaji,
>Mafuta ya safari husika,
>Mafuta ya kuzunguka angani kusubiri kama kuna dharura,
>Mafuta ya kwenda kutua uwanja wa ndege mwengine endapo kuna dharura katika uwanja uliopangwa kutua awali n.k

Kwahiyo ndege husika inapopata dharura muda mfupi baada kupaa rubani analazimika kupunguza mafuta angani katika eneo salama atakaloona au kuelekezwa na waongoza ndege ili kurudi kutua na uzito salama kuepuka hatari kama kupasuka tairi, kuharibu miundombini ya barabara #runways, kutosimama mapema au kupitiliza nje ya barabara yake 'runway', kutua kwanguvu #hardLanding, kuipa udhaifu/'#stress, kupinda au kuvunja maungio ya kiwiliwili cha ndege husika au kusababisha ajali kabisa.

Umwagaji mafuta mara nyingi ufanyika katika umbali maalumu kwenda juu na nje ya makazi ya watu au baharini.

Umbali wa kwenda juu kidogo husaidia mafuta hayo kutawanyika hewani na kupotea na upepo au kufika chini kama mvuke hafifu usio na madhara sana.

Kumbuka usifananishe kwani umwagaji mafuta huu pia unaacha mistari ya mvuke isiyodumu nyuma inayotaka kufanana kidogo na ile hali michirizi ya wingu inayoganda na baridi (#condensation) pale ndege inakuwa kimo cha juu sana ambayo wengi huita roketi kimakosa.
View attachment 1456396
Ongera kwa kuwapa shule madogo na hii ndio sababu jamiiforum imekuwa sehemu muafaka kujifunza ila naomba nikukosoe maana kuna watu wanachanganya mambo sio kila ndege inayotoa mosh angan inamwaga mafuta no JET ENGINE ya ndege hufanya kaz kwa principle kuu mbili moja pressure na temperature
Sasa hii principle ya temperature hiko hv engine hufyoza cold air in large opening kisha hutoa hot air in narrow opening sasa io hot air ndio huo moshi na lengo ni kuzalisha thrust japo kuna ndege zinamfumo wa kuhakikisha hazitoi mosh mwing
 
Em subilini Kwanza
Inamaana zile Ni ndege....
Na ule Moshi unaoonekana nyuma Ni mgandamizo,?
Maana Kama inamwaga mafuta inafikaje Sasa
Inamaana sijawahi kuona locket !?[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Ahsante mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Em subilini Kwanza
Inamaana zile Ni ndege....
Na ule Moshi unaoonekana nyuma Ni mgandamizo,?
Maana Kama inamwaga mafuta inafikaje Sasa
Inamaana sijawahi kuona locket !?[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Ahsante mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ule moshi ni maji yaliyo ganda kikawaida mafuta yanapo ungua hutoa by product ambazo ni maji na carbon dioxide.
Sasa kwa kuwa ndege zinakuwa zipo katika anga la juu sana ambapo temperature ni ndogo hivyo hupelekea maji ( vapour) , kuganda (kutengeneza kama wingu) na kuacha alama( trails).



Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
Enzi za utoto roket ikipita angani kiangazi tu inatutengenezea mvua na yale mawingu mweupe.

Sasa leo unasema zilikuwa zinamwaga mafuta kulaleki, hii haingii akilini dah
Screenshot_20200522-190219.jpg
Screenshot_20200522-190235.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa Mada Upo sahihi kabisa [emoji28]
Wale tunaoita zile Rockets ni iko hivi

Ni Reaction Kati ya HOT HUMID AIR From JET ENGINE na AIR MOLUCULES then inatengeza VAPOUR, ile VAPOUR ina condesnce ina'turn' into GAS kama Mawingu hivi na Ndio kile kinacho,onekana pale zinaitwa CONTRAILS
Na sio Rockets(Rocket Anga la Africa??)
Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ufafanuzi nilikuwa nausubiri nilikuwa sahihi utotoni na bado niko sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina hata miezi mitatu nilimdanganya mtoto Wa jirani, maana ndege ilipita hivyo ulivyoelezea ahaaa asante mleta Mada
 
Ambacho napenda kufahamu ni kwamba ni altitude gani hasa hizi ndege tulizokuwa tunaziita rockets huwa zinasafiri. Na kama huwa ndege za abiria au. Maana zinakuwaga juu sana.
Kumbuka usifananishe kwani umwagaji mafuta huu pia unaacha mistari ya mvuke isiyodumu nyuma inayotaka kufanana kidogo na ile hali michirizi ya wingu inayoganda na baridi (#condensation) pale ndege inakuwa kimo cha juu sana ambayo wengi huita roketi kimakosa.

Ulikuwa sahihi utotoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah cjui nani alitutengenez huu uvumi kwamba zile zinazopita juu. Na kuacha trails ni rockets..zile ni ndege za kawaida..though zinapita anga la juu sana ambalo kama wadau walivosema kuna mgandamizo mkubwa...rockets.kwa africa kwa kweli amna nchi inayoeza kufanya project hyo.ko hazipo..jaman nani anakumbuka kuna watu walikua wanasema eti zile rocket zinatuaga south Africa tu..hahahaha...utoto bna

Sent using Jamii Forums mobile app
Mstari wa mwisho umenikamata mkuu. Mpaka leo ndio nimefahamu kuwa Africa haijawahi kuona rocket.

Halafu kuna swali hapo juu, tunaomba kujua, rocket huwa zinasafiri na abiria? Kazi yake haswa ni ipi na husafiri kwa muda gani. Tuliosoma civics na stadi za kazi tunaomba ufafanuzi zaidi.
 
Back
Top Bottom