..lakini Roketi haina mabawa mkuu! Na kama hizi tunazoona ni roketi, zingepaswa kuwa na mchirizi mmoja tu wa moshi unaotoka kwa nyuma!
Ukiona michirizi minne fahamu kuwa ni ndege ya masafu marefu yenye injini Nne, mbili kila Bawa!
Na mara nyingi moshi ule hautokani na kumwaga mafuta kwa dharura, maana ingekuwa hivyo basi usafiri wa ndege ni dharura maana kumbuka wewe mwenyewe kwenye siku moja tu ya kawaida utaona ndege ngapi zinazoacha moshi zikikata anga! Dharura?
Nimependa maelezo ya Mkuu mmoja ambayo ametoa hapo kuhusu ule moshi ambao sio moshi kwa maana halisi bali ni aina ya mvuke tu unaotokana na baridi kali iliyopo hukoo juu inayotokana na joto kali linaloachwa nyuma na injini za ndege hizo...na ametoa mfano mzuri wa wewe mwenyewe kutoka nje siku ya baridi kali na kupumua kwa kutumia mdomo, uone mvuke mweupe unaotoka mdomoni mwako!!!