Sababu za Sabaya kukifunga kiwanda cha Daren Fabrics Industries Ltd

Sababu za Sabaya kukifunga kiwanda cha Daren Fabrics Industries Ltd

Pole mrs Saa mbaya pambana baby wako atoke
Hatuko tayari kuona wazalendo wa nchi yetu wakinyanyaswa na wauza madawa ya kulevya.

Tunaanza kampeni rasmi ya kumchangia na kumuwekea wakili Sabaya kwenye kesi yake. Kama msaliti wa nchi mzee wa MIGA aliweza kuchangiwa ,sisi kama watanzania wazalendo hatuwezi kushindwa kumchangia Sabaya ambaye kwa uzalendo wake aliitoa wilaya ya Hai kutoka ya 63 kwenye ulipaji kodi hadi ikawa ya 4 kitaifa.
Hatuwezi kuhukumu watu kwa kusikiliza upande mmoja wa wanafiki chadema ambao hawana jema kwa nchi yetu.

Chadema kila kitu wanapinga na kuponda, walipinga ndege, bwawa la umeme, elimu bure, ujenzi wa viwanda kila kitu wao ni kupinga tu, Ndege zilipokamatwa walishangilia.
Ndiyo tuwasikilize? Hapana.

#Justice for SABAYA
#Free SABAYA
 
Prison jazz band ,wanafanya yao tunaweza shuhudia MTU Akitembea miguu imetanuka ,kutokana na showkali
 
Kumtetea mtu muovu ni laana ambayo itakutafuna wewe pamoja na kizazi chako[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Video haijajibu tuhuma, mleta mada alisema kabisa kuwa TRA walikanusha, Wizara ikaingilia kati, akaweka na evidence, sasa wewe unakuja na clip ya sekunde kadhaa unatufanya watoto?

Jibu hoja zike, he TRA hawajawahi kumsafisha jamaa? Je mamlaka zilizotajwa mle hazijawahi kumsafisha huyo jamaa? Je Sabaya hajawahi kuomba hio pesa?? What if wakiweka na docs zaidi utaendelea kubisha??
Mkuu tusaidie clip au chochote kinachoonyesha TRA wakimsafisha speshoz
 
Kama umeumia mpelekee kesho uji na maandazi ya Bakhresa.Kichwa Kama koleo jipya wewe.
 
Hatuko tayari kuona wazalendo wa nchi yetu wakinyanyaswa na wauza madawa ya kulevya.

Tunaanza kampeni rasmi ya kumchangia na kumuwekea wakili Sabaya kwenye kesi yake. Kama msaliti wa nchi mzee wa MIGA aliweza kuchangiwa ,sisi kama watanzania wazalendo hatuwezi kushindwa kumchangia Sabaya ambaye kwa uzalendo wake aliitoa wilaya ya Hai kutoka ya 63 kwenye ulipaji kodi hadi ikawa ya 4 kitaifa.
Hatuwezi kuhukumu watu kwa kusikiliza upande mmoja wa wanafiki chadema ambao hawana jema kwa nchi yetu.

Chadema kila kitu wanapinga na kuponda, walipinga ndege, bwawa la umeme, elimu bure, ujenzi wa viwanda kila kitu wao ni kupinga tu, Ndege zilipokamatwa walishangilia.
Ndiyo tuwasikilize? Hapana.

#Justice for SABAYA
#Free SABAYA
Nipo tayari

#Justice for SABAYA
 
kama huyo Sabaya bado ana marinda basi vijana wa magereza waongezewa kifungo
 
Acha sheria ichukue mkondo wake! Mahakama itatoa uamzi,kama hana hatia ataachiwa huru na nadhani (ingawa mimi si mwamnasheria) kama atashinda kesi anayo haki ya kuishitaki Jamhuri kwa kumsingizia makosa ambayo hakufanya.
 
Uchagani ni tatizo watu wanadhani eti walionewa saaana! Huyu Sabaya anawezakuwa na ubaya wake lakini kikubwa ni Mbowe hawamuoni ktk siasa. Wako tayari kuchanga na kuhonga ili tu ushahidi wa uongo utengenezwe. Huyo Malisa ni bonge la ignorant, sasa naye kawa thinker wa kuaminiwa. Kila siku ni ukabila tu!

Ni mkoa ambao wanaamini wako peke yao waachwe wao kwa wao, ingawa wao wanakwenda mikoa ya wengine sana! Nilisikia Samia akisema hata Mgwila walimpa taabu. Huko Nyuma alikuwepo Gama naye walimpa taabu sana!
Hiki ndo nina uhakika nacho 100%.
 
Haya mambo msiandike humu jamani...muende kumtetea huko alipo humu hamumsadii kitu na hayo maandiko
 
Uchagani ni tatizo watu wanadhani eti walionewa saaana! Huyu Sabaya anawezakuwa na ubaya wake lakini kikubwa ni Mbowe hawamuoni ktk siasa. Wako tayari kuchanga na kuhonga ili tu ushahidi wa uongo utengenezwe. Huyo Malisa ni bonge la ignorant, sasa naye kawa thinker wa kuaminiwa. Kila siku ni ukabila tu!

Ni mkoa ambao wanaamini wako peke yao waachwe wao kwa wao, ingawa wao wanakwenda mikoa ya wengine sana! Nilisikia Samia akisema hata Mgwila walimpa taabu. Huko Nyuma alikuwepo Gama naye walimpa taabu sana!
"Sabaya anaweza kuwa na ubaya wake"
this statement ina prove kuwa maybe ana mazuri.. lakin pia ana madudu yake.

"watu wanadhan walionewa sana" tuambie ww.. tofauti ya kuonewa sana na kuonewa kidogo, je kuna kunazuia watu wasiseme?

na hayo madudu hayawez kuachwa eti kisa alifanya mazuri fulani fulani.
Sheria haifanyi kazi hivyo. sheria haifanyi kazi kishkaji

oh tatizo ni mbowe. wakati yote yanatendeka mbowe alikaa kimya. mpaka leo yupo kimya.

mpaka sabaya anafika hapo alipofika mbowe anahusikaje?

mbowe ndio kafungua kesi? ndio kashtaki takukuru? au mbowe ndio kasema kwa mhe rais?
but either way what his involvement in this case?
 
Chadema hawa hawa wanaokatazwa kufanya siasa , wanaoibiwa kura na CCM wanaonyanyaswa na police kutwa kucha?

Chadema sasa inamiliki TAKUKURU? CHADEMA ina MAHAKAMA? CHADEMA ina POLICE? Inamaana nchi inaongozwa na CHADEMA au CCM? hoja zingine haziingii akilini kabisa
Kila siku wanadai CDM imekufa waulize imefufuka lini?
 
Chadema hawa hawa wanaokatazwa kufanya siasa , wanaoibiwa kura na CCM wanaonyanyaswa na police kutwa kucha?

Chadema sasa inamiliki TAKUKURU? CHADEMA ina MAHAKAMA? CHADEMA ina POLICE? Inamaana nchi inaongozwa na CHADEMA au CCM? hoja zingine haziingii akilini kabisa
Siku moja utajua maana ya propaganda na kupika ushahidi feki.

Hivi ujiulizi sasa hivi watu maarufu wengi wanakufa na hakuna story za corona! Kafariki Mzindakaya, Songoro wa Songoro marine na wengine wengi kwa muda mfupi lakini hakuna hata ukelele wa korona inatumaliza! Imagine angekuwepo Magufuli! Magazeti, BBC, DW story zingekuwa corona Tanzania! Hakuna kingine Kungekuwa kinajadiliwa sasa hivi.

Kumbe vinara wa propaganda lengo lilikuwa kumchafua Magu kwa sababu zao za ubinafsi wao, na wengine sababu hamfikirishi akili zenu mnakubali kucheza ngoma msiyoijua!

Sababu ni propaganda. Wapiga propaganda wanajua kushawihi hasa akili za wasiojitambua (na wako wengi sana) wanaibua mijadala na watu wanajikuta hao wako ndani pulizo! Wanaelekea wajanja wanakotaka waelekee!
 
Jifunze kutofautisha btn reality and illusions.
Propaganda ni illusion.. but serikal haifanyi kazi kwa kusikiliza propaganda.
ndio maana ina idara na vyombo husika vya kufanya task za uchunguzi.

Chadema haina power ya kuishawish serikal imkamate sabaya. serikal imeona yenyewe tu kuwa kuna haja ya kulifanyia kazi.
 
JPM aliyapenda haya! eti kwa kuwa alimuandaa kumng'oa Mbowe .
 
Mwaka jana mwishoni mfanyabiashara na mbunifu wa mavazi Jeffery Mmbungu maarufu kama @Speshoz alifungua kiwanda cha vinywaji vikali, wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro. Kiwanda hicho kinaitwa Daren Fabrics Industries Ltd kinazalisha kinywaji chenye jina Faru John.

Mwezi February mwaka huu, aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya alimpigia Jeff na kumwambia kuwa CCM itafanya maadhimisho ya miaka 44 tangu kuanzishwa, na yeye ni miongoni mwa wanakamati wanaoandaa maadhimisho hayo.

Akataka kiwanda hicho kichangie TZS 10M kufanikisha maadhimisho hayo. Jeff akamwambia hana uwezo wa kuchangia 10M, lakini akaahidi kuchangia 1M. Sabaya akamnanga kwamba serikali ya CCM ndiyo iliyomuwekea mazingira mazuri ya kibiashara hadi akaweza kufungua kiwanda, kwahiyo kuchangia 1M ni dharau kwa chama, anatakiwa achangie kiasi kisichopungua 10M.

Jeff akamwambia hana pesa hiyo. Sabaya akamwambia nimepitia transaction zako TRA najua unafanya mauzo ya mamilioni ya shilingi. Jeff akamwambia bado kiwanda ni kichanga na hakijaanza kujiendesha kwa faida kiasi cha kumpa Sabaya 10M.

Mwezi May mwaka huu Sabaya akavamia kiwanda hicho akiwa na mabaunsa wake. Wakawa-harass sana wafanyakazi waliokuwepo. Sabaya akiongozana na waandishi wa vyombo 11 vya habari akatangaza kukifunga kiwanda hicho kwa madai kinajiendesha bila vibali.

Vyombo vya habari vikaripoti kuwa kiwanda hicho kimefungwa kwa kufanya uzalishaji wa vinywaji vikali bila kuwa na kibali. Jeff akashangaa kwa sababu alikua na vibali vyote.

Ana leseni ya BRELA nambari 142255766 iliyotolewa July mwaka 2020. Ana leseni ya TRA nambari 142255766 iliyolewa July 2020. Ana leseni ya biashara nambari 03356294 iliyotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Hai tarehe 25 September 2020.

Ana Leseni ya mkemia mkuu wa serikali nambari B002C000255 iliyotolewa October mwaka 2020, pia ana Leseni ya TBS nambari 3082 iliyotolewa December 2020. Pia kabla ya kuanza uzalishaji alipewa barua ya ruhusa kutoka TBS yenye Kumbukumbu nambari QA/QCCA/3215/17.

Sasa akashangaa imekuaje kiwanda kifungwe kwa kukosa vibali wakati vibali vyote anavyo? Akampigia Sabaya kumuuliza. Akamwambia aende ofisini.

Alipofika ofisini, wakaongea na akamuonesha nakala za vibali. Sabaya akatoka ofisini na kumuacha ndani. Aliporudi akamnyang'anya simu zote, na kumuamuru akae chini. Akaita mabaunsa wake, wakamvua viatu na mkanda na kumpeleka rumande.

Taarifa za kukamatwa kwake zikafika kwa viongozi mbalimbali wa serikali. Wizara ya ya viwanda na biashara ikatoa tamko kuwa kiwanda hicho kinajiendesha kwa mujibu wa sheria. Wizara ya uwekezaje, ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali, Shirika la viwango (TBS), pamoja na ofisi ya BRELA wakaingilia kati na kueleza kuwa kiwanda hicho kinajiendesha kihalali.

Kesho yake Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro akafanya press na kutoa ufafanuzi kuwa kiwanda hicho kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Taarifa hiyo ikaeleza kuwa mwezi April kiwanda hicho kilipewa stika za 200M na kiliweza kuhuisha stika za 93M. Pia kwa siku chache za mwezi May (kabla hakijafungwa) kilikua kimehuisha stika za 13M.

Taarifa ya TRA ikaeleza kuwa kiwanda hicho hakijawahi kuwa na mgogoro wowote na serikali wala hakijawahi kujiendesha bila kuwa na vibali. Ikatangaza kukifungulia kiwanda hicho na kukiruhusu kiendelee na uzalishaji.

Media zote zilizoripoti kuwa kiwanda hicho kimefungwa zilialikwa kwenye Press ya TRA ili ziujulishe umma kwamba taarifa ya Sabaya haikua sahihi, na kwamba kiwanda hicho kimeruhusiwa kuendelea na uzalishaji.

Lakini Sabaya akazuia media hizo zisiripoti taarifa hiyo ya TRA. Ni ITV pekee walioamua kusimama katika misingi ya taaluma na kutoa ufafanuzi kwa umma. Media nyingine ziliamua kusimama na Sabaya. What a shame?

Tayari Jeff ameshaenda TAKUKURU kuwasilisha ushahidi wake. Pia atawasilisha malalamiko Baraza la habari nchini (MCT) ili media zilizomchafua na zikakataa kumsafisha zichukuliwe hatua, kwa sababu habari ya kiwanda hicho kufungwa imeathiri mauzo kwa kiasi kikubwa!
Dah KWA kweli jameni nimeshindwa kumtetea Sabaya KWA unyama huu
 
Hii habari ya kuruhusu uzalishaji wa hicho kiwanda cha vileo, habari ITV waliirusha kweli nakumbuka.
Ila kwa mwendo huu hakuna rangi Sabaya atashindwa kuiona. Kila uchao yanaibuka mapya. Hakuna kwa kuegemea safari hii.
 
Halafu mkikaa hapa mnamsifia jiwe eti alikuwa mzalendo.

Do yoy think haya hakuyaona au kusikia?
Aliyajua fika,maanake alikuwa akisema waziwazi,kwamba aliwaelewa vyema wateule wake kiasi hata kujua sms wakizokuwa wakitumiana.
Alienda mbali zaidi hadi kudukua simu zao.
 
Back
Top Bottom