kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Bunge la Jamhuri ya Tanzania mwaka huu linatarajia kujadili na kupitisha mkataba wa Kiserikali kati ya Tanzania na Dubai kuhusu kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam, Hili litaweka mazingira ya kufanyika kwa taratibu nyingine, ikiwamo mkataba wa makubaliano, kabla ya kuanza kwa sura mpya ya ushirikiano kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na DP World.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa anasema sababu ya serikali kupendekeza kampuni ya DP World kufanya kazi na Mamlaka ya bandari ni uwezo wa kampuni hiyo katika kukabiliana na vikwazo vya kimataifa vya kibiashara vinavyosaidia kukuza biashara za kimataifa na kuongeza mapato.
Inakadiriwa, kampuni hiyo itakapoanza kufanya kazi katika bandari ya Dar es Salaam inatarajia kuongeza ukusanyaji wa mapato kupitia bandari hiyo kwa asilimia 233.7 katika miaka kumi ijayo. Huku lengo likiwa ni kuongeza kiasi cha mapato yanayokusanywa bandarini kutoka Sh7.79 trilioni kwa mwaka hadi Sh26 trilioni katika muongo ujao.
DP World ina teknolojia za kisasa, vifaa vya hali ya juu na wafanyikazi wenye ujuzi ambavyo vitawezesha bandari kushughulikia mizigo zaidi, kupunguza msongamano, na kuharakisha nyakati za ugeuzaji wa meli, na hivyo kupunguza gharama kwa wateja wa mwisho.
Kampuni hiyo ina rekodi iliyothibitishwa ya kusimamia, kuendesha na kuwekeza katika miundombinu ya biashara barani Afrika kwa zaidi ya miaka 20 kwa viwango vya juu zaidi vya kimataifa.