Sababu za Tanzania kupitwa kimaendeleo na nchi nyingine

Unatetea nini hapa YEHODAYA ?!.

Utajinasua lini hata utumie hicho kichwa kuleta la maana !!
 
Kingereza kisingeweza kuunganisha makabila zaidi ya 100 yaliyopo hapa Tanzania. Wengi wangerudia kuongea lugha za makabila yao maana kingereza ni kigumu na ni lugha ya kigeni. Na hicho kingeleta ukabila alioupiga vita Nyerere.
Akili ndogo kukariri upumbavu
 
Mfano wako wa Rwanda. Umeharibu point zako nzuri!
Rwanda kilicholeta maendeleo ni matumizi Bora ya ardhi ya Congo DRC, full stop!

Wamejua kuitumia DRC!
 
Kiingereza sio sababu ya kuwa maskini, tumekuwa nacho tangu uhuru lakini hakijatusaidia kuondokana na umaskini. Yatupasa sasa kuacha kufundisha watoto wetu kwa lugha hii
 
Kutumia kiingereza kufundisha watoto wetu ni moja ya sababu ya sisi kuwa maskini
 
Kutumia kiingereza kufundisha watoto wetu ni moja ya sababu ya sisi kuwa maskini
Mkuu ungefafanua kwasbb kiingereza chenyewe hatukijui, tuna ongea kiswahili nakujua kiswahili kwa 98% ila elimu bado duni ushindani wa kazi za kimatafa bado sana ugunduzi na ubunifu hamna ujuzi hamna, kwahiyo tatizo sio kiingereza tatizo ni kitu kingine kabisa.
 
kichwa cha habari jibu lake ni hili hapa!

ccm bado inatumia zana ikifanya maendeleo yote watakosa pengine kupigwa kula kama unavojua waziri kaenda kuzindua vyoo.
mabadiliko ya katiba na keki ya taifa.
Kweli eti kuzindua vyoo ,dah hiyo si kazi ya mwenye kiti wa mtaa sijui mkuu wa wilaya. Dah sisiem hoyeee
 
Hili nakubaliana na wewe,angalia nchi kama DRC walivyo na raslimali na bado ni maskini wa kutupwa
 
Kinacho takiwa ni change of "MINDSET" kwa kila mtu, maana utegemezi wa serikali ktk kutoa ajira ni too much. Ila kinachotakiwa ni exposure ya watu pia "HONESTY" Yani uwazi,ukweli nyani hapa bana tunafeli sisi temezidi yani "Upigaji" au "kurushana" ni kwingi, uwongo mwingi. Kwaiyo mpaka tubadilike hapo ndipo itakuwa rahisi
 
Huu ni uzwazwa wa watanzania kujidharau na kuona kila kitu cha nje ni bora kuliko chao. Hizo nchi zimeizidi Tanzania kwa lipi hasa? Umewahi kufika Senegal wewe au sababu unamuona Mane Liverpool basi unadhani nchi yao imeendelea?

Unasema watz wanashabika siasa, social media za Kenya na Uganda zimejaa siasa tu wapi wanashabikia siasa zaidi?
 
Yeye Nyerere alishindwa nini kuindeleza nchi iliyokuwa na raia milioni 9 tu huku akiwa ameachiwa na viwanda kabisa na wakoloni?.Badala ya kuwahimiza raia waliokuwa wapowapo tu kupambana kujitengenezea uchumi ili kuchangia katika maendeleo ya nchi kwa ujumla,yeye akalazimisha raia wachache kina mzee MWAMINDI waliokuwa wamejiongeza kwenye kilimo,wawagawie sehemu za mashamba yao raia wavivu ili hali mapori yalikuwa yamejaa.
Kwa upande wangu mimi Nyerere siyo mfano kabisa wa kukua kwa uchumi wa nchi yetu.
 
Ntakujibu vema tu.
Ila nianze kujua toka kwako, kwa kumbukumbu zako toka vyanzo rasmi Nyerere aliachiwa viwanda vingapi na wakoloni?

Ili tukimlaumu/kumhukumu tuwe na solid grounds za kufanya hivyo
 
Nini sababu ya nchi nyingine nazo kupitwa kimaendeleo na nchi nyingine ikiwemo Tanzania...
Sasa tusiangalie Nchi peke yake kupitwa na familia nayo ijiangalie pia kwanini ipitwe kimaendeleo? Familia ikiwa na watu waliosoma vizuri na vipato vizuri itakuwa rahisi kuisema serikali ilete maendeleo yenye viwango vya watu wanaopenda kuishi vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…