Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unatetea nini hapa YEHODAYA ?!.Tatizo sio elimu duni dunia nzima nchi zote zilizoebdelea technolojia huguduliwa na watu binafsi sio serikali zao
Tanzania tumesomesha mijitu kibao nchi hizo zinazosifiwa kwa elimu kubwa kuanzia chekechea hadiI PhD lakini hawana LA maana walilogundua kubadilisha kuanzia maisha yao wenyewe wanadandia siasa tu wawe akina Tundu Lisu au mbatia ambao walisoma ulaya kwenye elimu bora ni waganga njaaa tu kama wasoma kayumba
.Hata ma diaspora yaliyobaki nje yakapata elimu bora huko yaliko yanajitwika mabox tu misiba ikitokea inakuja kutuchangisha Huku Tanzania haina hela milofa tu
Akili ndogo kukariri upumbavuKingereza kisingeweza kuunganisha makabila zaidi ya 100 yaliyopo hapa Tanzania. Wengi wangerudia kuongea lugha za makabila yao maana kingereza ni kigumu na ni lugha ya kigeni. Na hicho kingeleta ukabila alioupiga vita Nyerere.
Tz kama nchi tunahitaji kiingereza mara 100 kuliko kiswahili ili tuweza ku integrate na uchumi wakimataifa, viongozi wetu wanatupumbaza kati wao wanaoeleka watoto wao shule za English mediumAkili ndogo kukariri upumbavu
Mfano wako wa Rwanda. Umeharibu point zako nzuri!Mfano wa Rwanda unatuambia “ili tuendelee tunahitaji uongozi bora”. Vita vya kimbari vilileta mauaji ya kutisha Rwanda 1994. Walichinjana watu laki nane.
Baada ya vita, Rais Kagame akachukua nchi. Ilikuwa kama failed state, lakini sasa ona waliko. UONGOZI BORA is the conditio sine qua non for development.
Rwanda haina ardhi kubwa. Wamebanana sana. Watu, ardhi na siasa safi siyo vitu vilivyoleta maendeleo Rwanada. Ni uongozi bora, full stop.
Ukivuka nje ya mipaka yetu kiswahili hakina maana yoyote .Tz kama nchi tunahitaji kiingereza mara 100 kuliko kiswahili ili tuweza ku integrate na uchumi wakimataifa, viongozi wetu wanatupumbaza kati wao wanaoeleka watoto wao shule za English medium
Mkuu ungefafanua kwasbb kiingereza chenyewe hatukijui, tuna ongea kiswahili nakujua kiswahili kwa 98% ila elimu bado duni ushindani wa kazi za kimatafa bado sana ugunduzi na ubunifu hamna ujuzi hamna, kwahiyo tatizo sio kiingereza tatizo ni kitu kingine kabisa.Kutumia kiingereza kufundisha watoto wetu ni moja ya sababu ya sisi kuwa maskini
Kweli eti kuzindua vyoo ,dah hiyo si kazi ya mwenye kiti wa mtaa sijui mkuu wa wilaya. Dah sisiem hoyeeekichwa cha habari jibu lake ni hili hapa!
ccm bado inatumia zana ikifanya maendeleo yote watakosa pengine kupigwa kula kama unavojua waziri kaenda kuzindua vyoo.
mabadiliko ya katiba na keki ya taifa.
Hili nakubaliana na wewe,angalia nchi kama DRC walivyo na raslimali na bado ni maskini wa kutupwaKuna kitu kinaitwa " the paradox of plenty" - Nchi zile zenye rasilimali nyingi kubakia kuwa maskini tofauti na ilivyotegemewa kuwa rasilimali hizo zingeboresha maisha na hali zao.
Huu ndio ukweli, angalia nchi kama uswiswi, milima, vijiji, barafu, lakini uswiswi ina GDP per capita ya dola 73,000. Tanzania na hali nzuri ya hewa, rasilimali kibao tuna GDP per capita ya hardly 1200 USD
Kinacho takiwa ni change of "MINDSET" kwa kila mtu, maana utegemezi wa serikali ktk kutoa ajira ni too much. Ila kinachotakiwa ni exposure ya watu pia "HONESTY" Yani uwazi,ukweli nyani hapa bana tunafeli sisi temezidi yani "Upigaji" au "kurushana" ni kwingi, uwongo mwingi. Kwaiyo mpaka tubadilike hapo ndipo itakuwa rahisiSababu ya elimu duni kwa kizazi cha zamani na hata Sasa bado Kuna asilimia kubwa isiyo na elimu nzuri ila tunakoelekea asilimia kubwa watakuwa na elimu nzuri nambo mazuri yatakuja na kazi zitapatikana nyingi tofauti na Sasa hizo za Kila mtu kuwa chinga tena eneo moja la mjini maana vijijini watu hawana elimu na kufanya uwekezaji usiwepo vijijini maana wao wanajua kuishi ni kula tu na maisha mengine yenye kusipport jamii na kuleta ajira wamewaachia watu wa mjini tu.
Yeye Nyerere alishindwa nini kuindeleza nchi iliyokuwa na raia milioni 9 tu huku akiwa ameachiwa na viwanda kabisa na wakoloni?.Badala ya kuwahimiza raia waliokuwa wapowapo tu kupambana kujitengenezea uchumi ili kuchangia katika maendeleo ya nchi kwa ujumla,yeye akalazimisha raia wachache kina mzee MWAMINDI waliokuwa wamejiongeza kwenye kilimo,wawagawie sehemu za mashamba yao raia wavivu ili hali mapori yalikuwa yamejaa.Nyerere alisema ili tuendelee twahitaji
Ardhi (tunayo)
Siasa safi (je tunayo?)
Watu (wapo au tupo. Ila tuna uwezo kiasi gani kuyatawala mazingira yetu kwa kukuza uzalishaji wenye tija)
Siasa safi (hapa tuna mjadala mkubwa sana. Polepole ameweka wazi siasa ndani ya chama cha zina mizengwe, uchawi, fitna; ukizubaa tu, ndio hivyo. JK wakati mmoja akiwa mkulu, aliweka wazi wanachama wa chama chake hawaachiani glass za vinywaji).
Ukiona tumefika pahala ambapo "kuna wale na sisi", tuna makundi ya Urais yalianza toka 1994 enzi za boys2men,wakaja wana-mtandao, mara mtandao ukafa kukawa na virungu chungu mzima, maana yake, nchi hii inahitaji reforms za "kufa mtu"
Rwanda PK kajitahidi sana kuiweka nchi kwenye ramani ya Afrika na ulimwenguni.
Tanzania tunakwama kwa kukosa nini kifanyike ili rasilimali watu izalishe kwa tija na kufanya biashara kukidhi mahitaji ya soko la ndani na then twende walau soko la EA na SADC.
Mpaka sasa elimu yetu ni a for apple na sio elimu yenye maswali kama apple zinatoka SA kuja hapa kwa miaka mingi, kwa ukubwa wa ardhi ya nchi hii ambayo ni virgin, nini tufanye ili ndani ya miaka 10 ijayo Tz iwe kwenye ramani ya exports ya apple zenye ubora kwa nchi zaidi ya 15 (8 za jirani & SADC)
Tuna viongozi wanaosaidia wakulu wenye fikra za nini nifanye niendelee kumpendeza mkulu. So, ni matamko, mipango, kuonekana kwa media ila ukipima kuna effors ndogo sana kukuza uzalishaji wa kibiashara.
Tunalima mahindi kila mwaka mpaka yanakosa soko, kwanini kusifanyike tafiti kule kwenye ukanda mahindi yanakubali tukazalisha breed inayokamuliwa mafuta ili ku-cover deficit ya mafuta ya kula worth 600bn kwa mwaka?
Watawala wetu badala ya kufikiri wa picha kubwa, wanawaza viwanda vidogo. Na kuna mmoja na masters holder akiwa waziri akawa anasema machine ya kuponda tofali au cherehani ni kiwanda kidogo. Very low sense of accountability.
Tukipata strategic thinkers kwenye leadership, tunaweza kusogea haraka sana. Ila kama ni hawa waimba hiena hiena na wale wanajiita "mimi ni chawa wa ...." mimi nina degree 4, tunazidi kuchelewa sana.
Ntakujibu vema tu.Yeye Nyerere alishindwa nini kuindeleza nchi iliyokuwa na raia milioni 9 tu huku akiwa ameachiwa na viwanda kabisa na wakoloni?.Badala ya kuwahimiza raia waliokuwa wapowapo tu kupambana kujitengenezea uchumi ili kuchangia katika maendeleo ya nchi kwa ujumla,yeye akalazimisha raia wachache kina mzee MWAMINDI waliokuwa wamejiongeza kwenye kilimo,wawagawie sehemu za mashamba yao raia wavivu ili hali mapori yalikuwa yamejaa.
Kwa upande wangu mimi Nyerere siyo mfano kabisa wa kukua kwa uchumi wa nchi yetu.
Sasa tusiangalie Nchi peke yake kupitwa na familia nayo ijiangalie pia kwanini ipitwe kimaendeleo? Familia ikiwa na watu waliosoma vizuri na vipato vizuri itakuwa rahisi kuisema serikali ilete maendeleo yenye viwango vya watu wanaopenda kuishi vizuri.Nini sababu ya nchi nyingine nazo kupitwa kimaendeleo na nchi nyingine ikiwemo Tanzania...