Sababu za Tanzania kupitwa kimaendeleo na nchi nyingine

Nini kifanyike? Jamii ndo iamuke itoke kwenye ujinga kama ni elimu watu wa zamani wengi hawakupata elimu na ndo tatizo lilianzia hapo walisoma wachache na haohao kupata ajira moja kwa moja na vizazi vyao wamewapa elimu nzuri na ajira ni zawao tu maana wale waliokosa elimu hawakuona uzuri na umuhimu wa kuwapa watoto wao elimu nzuri labda watoto waliolazimisha kusoma kwa lazima au kwa msaada ndo tunaona wanavyeo nao wanajipendelea tu, hivyo tukazanie elimu za vizazi vyetu Kwanza Ili wengi waelimike na kujitambua na mazingira ya kuwekeza yataleta faida imagine mpaka Sasa bado tunaishi kizamani kwa kupoteza muda tu kama mtu kulima kwa jembe la mkono mazao kidogo yasiyo na faida, kushinda mtu anazunguka na mifugo kama vile na yeye ni mfugo badala ya kutengeneza au kuzalisha chakula cha mifugo na kufuga kisasa tena kama kampuni inayojitosheleza na mahitaji ya mifugo yake Sasa watu wenye akili za kizamani kama hizi wataweza kuzungusha uchumi kiasi cha wenye madaraka kutetemeka na kufanya mambo makubwa? Maana watu wakifanya mambo kisasa yanaleta ajira nyingi sana mfano elimu ya English medium inaajili watu wengi kuliko hizi za kata na hata huduma zingine kama kilimo kikiwa kisasa kinaleta pesa nyingi na ajira nyingi.
 
Huu mjadala ni wa moto sana , ni kweli kabisa hali ya nchi inasikitisha sana ukilinganisha na rasilimali tulizo nazo .
Tatizo hizo rasilimali tunazosema tunazo hatuna maamuzi nazo hivyo kama jamii Kwanza ijiangalie kifamilia ipambane kutumia muda vizuri kujiletea maendeleo na kukataa kutumia muda vibaya kwa mambo ya wengine inatakiwa mtu ajute muda wake unapokuwa umetumika vibaya kwaajili ya mambo yasiyompa faida.
 
Kutumia kiingereza kufundisha watoto wetu ni moja ya sababu ya sisi kuwa maskini
Hapana kabisa kiingereza ni lazima tangu watu walipoanza kwenda kutafuta shule za kiingereza nje na mwisho kuzileta hapa nchini ndo unaona hata matumizi ya vitu vya kisasa na teknologia ndo vinaingia nchini kwa Kasi sana maana hata simu za kiswahili sijaona na teknologia ipo kwa kiingereza zaidi Sasa unataka watu warudi kwenye kusomewa barua, mikataba na matumizi ya vitu kwa kutumia wakalimani wa Nchi za nje jamani? Hapana kabisa kiingereza ni lazima kwa Kila mtu maana tumechoka kuwa na wajinga wengi hivi hata Tv za nyumbani sizinamfumo wa kiingereza Sasa kwanini tujiweke kwenye mazingira ya ujinga? Na hicho kiswahili kinachotumika na Nchi moja yenye akili moja na wakati kiingereza kinatumika na wengi na wenye akili tofauti?
 

hili ndio watu wengi hatuliangalii, tunapenda kuwanyooshea vidole walioko madarakani ilihali nao wametoka miongoni mwetu, tabia zile zile walizonazo ndio tulizonazo huku uraiani....

Tabia za wizi, uzinzi, uongo, usaliti, umalaya, unafiki, uchawi nk hizi ni tabia ambazo wote tuko nazo huku uswahili na sisi ndio tunaweza kuwa viongozi tukaendekeza ujinga huohuo..

La msingi ni watu katika ngazi ya familia kulea familia katika misingi inayowaweka mbali na tabia za hovyo hovyo kama wizi, uzinzi, uchawi nk....wote tukiyasimamia haya basi tutakuwa na jamii imara..
 
Tatizo ni elimu ya kikalekale kama historia Fulani isiyo na ukweli kwasababu watu wengi walikuwa wajinga wakawa wanaogopa wengine wasiwe welevu wakawazidi ndo yote haya bado yameganda kwenye vichwa, ndo maana bado tunaogopa kizazi kipya kikijua kiingereza kikawa na maarifa ya kimataifa kitatuzidi welevu na kutushangaa kwanini tunaishi kama wanyama wasio na maarifa, mtu kuchezea muda kwa kukaa shambani siku nzima kwa kulima tuta moja eti ndo ufahari badala ya kutumia majembe ya kisasa na kulima mazao mengi kwa muda mfupi na muda mwingine ukatumika kwa mambo mengine ya uchumi, ona Leo gesi ilivyookoa upishi wa muda mfupi lakini bado Kuna watu wanaona kutumia Kuni ndo ufahari yaani akili hazitumiki kabisa.
 
Kuna vita ya kagera iliturudisha nyuma sana na pia kuzisaidia nchi za kusini mwa Africa kupigania uhuru wao nayo ilichangia
miaka 40 tangu vita ya kagera hatuja rekabisha uchumi watu kweli, kipindi hicho nchi nyingi kama Zimbabwe SA nk zilikua hazijapata uhuru, zimepata uhuru na kutupita, kwanini Tz hatuende mbele kiuchimi?
 
Ukisema nchi imeendelea ni vigezo gani unavyotumia? Kama GDP si kigezo kimoja - tutajie hivyo vigezo vya kusema nchi imeendelea kuliko Tz. Yaani wewe maendeleo ni kuchukua fikra/ mambo ya ulaya na kuleta Tanzania.
 
Umeongea kishabiki bila hoja yoyote ya maana, umeshindwa kuunganisha doti kuhusiana na utawala wa ccm na umaskini wa watanzania ambao wamefikia hatua ya kuona fahari kwa kuwaita "Wanyonge". Poor you.

Wewe ndo pumba kwa kuwa unadanganyika kuwa Chama ndo Shida ya maendeleo yetu. Utasubiri sana. Hata hivyo Tz tuko vizuri. Sijui unajifananisha na nani. You can not have it all my brother.

Viongozi Ni wachache sana kuliko hao mliopo maofisni na wakamilishaji miradi. Huko ndo wanaiba sana hela zetu na kujenga.

Wanaopindisha mambo wengi wako mkoani na wilayani. Hao Ni wanachama wa vyama vyote.

Wavivu Ni wanachama wa vyama vyote

Wengi tumesoma ulaya na Marekani. Vyuo Bora. Lakini tukirudi tunataka tuibe haraka au tunakutana na wale wa la saba la mwaka 1947, kila ukipendekeza mabadiliko Utaskia wenzako ulitukuta na utatuacha.

Akitoke kiongozi mkali wa kutaka actions. Mnaanza wenyewe siasa.

Watz mmejiroga. Na siku mtakayokubali kukaa chini kajitafakari na kuacha kunyoesheana vidole ndo siku ya ushindi.
 
Sababu zote ulizotoa siyo sahihi; sababu kubwa ni kuwa Tanzania tunapenda sana shortcut, ambayo ndiyo inayozalisha hayo uliyotaja. Kwa mfano, tamaa ya shortcut inafanya kila mtu awe shabiki wa kisiasa ili aambulie chochote kule. Ukisema ubane shortcuts zote nchini ili kila mtu afuate njia inayotakiwa, utapata taabu sana. Dira ipo, ila kushorcuts katika utekelezaji wa dira hiyo ndilo tatizo. Kufahamu kiingereza siyo tatizo kwani Cote d'ivoire hawaongei kiingereza lakini umewaweka katika listi yako. Lugha ya kiingereza itakuja yenyewe kwa mtu iwapo ataona anaihitaji; kwa mfano wanamuziki wengi tanzania siku hizi wanajua kiingereza kwa sababu wanakihitaji.

Ondoa shortcut zote na mold watu kujua kuwa inabidi wafanye kazi kweli ili kujipatia riziki halali siyo kwa njia za mkatomkato, utaona nchi inaendelea haraka sana.
 
Uchumi wa wachuuzi, tutegemee nini??
Ukiwe mwekezaji TRA wanalala na kuamka na wewe. Kodi utitiri! Bora kulipa 20elfu ya kitambulisho cha ujasiliamali! Uishi kibishi

Hapa tunakosea sana. Labda tuwe na Mawaziri waliowahi kufanya biashara. Au waende field kufanya biashara kwa muda flani, wawe wakulima, hata wawe Machinga, wajifunze kabla ya kuwa Mawaziri.

Tunaweza kupata sera zitakazo wasaidia Watanzania wengi.
 
Sababu kubwa ni moja; UONGOZI MBOVU NA HOVYO WA CHAMA CHA MAPINDIZI.
 
Ni muhimu kuangalia English kama ni sehemu moja muhimu itayowasaidia Watanzania to be proper connected to Duniani, kujifunza mengi, kufanya biashara za kimataifa, kupata elimu.

Internet, Science, technology, historia ya Afrika, ya dunia imeandikwa kwenye lugha ya Kiingereza.

Hata uchumi, ajira, biashara zinaweza kuimarishwa kwa kujua kiingereza.
 

Ajabu nyingine ni kwamba mahakama zetu, maagizo mengi ya serikali, hukumu muhimu, vitu muhimu vinaandikwa Kiingereza wakati wengi hawajuhi hata wamehukumiwa nini, document zinasema nini? Mawakili nao wana- struggle to intepret hukumu.
 
Ukisema nchi imeendelea ni vigezo gani unavyotumia? Kama GDP si kigezo kimoja - tutajie hivyo vigezo vya kusema nchi imeendelea kuliko Tz. Yaani wewe maendeleo ni kuchukua fikra/ mambo ya ulaya na kuleta Tanzania.
Nakujibu maana wewe wataka kujua, si wale wanaotukana!
Ili nchi iitwe imeendelea, kwanza wananchi wake waoneshe wameendelea. Unaweza kulipima hili katika mambo yanayoonekana na mambo dhahania. Yanayoonekana kama, per capita income (kila Mtanzania angalau awe anapata wastani wa sh. milioni 12 kwa mwaka, sawa na $ 4,500 ( sh. elfu 33 au $12.5 kwa siku). Au kwa maneno mengine: ana uwezo wa kula milo mitatu ya wastani- inayoendana na matakwa ya mwili. Kwa hilo tu, nakuhakikishia hata asilimia 10 ya Watanzania hawalimudu. Tazama per capita ya nchi zinazofanana nasi kwa idadi ya watu, ujue nani kaendelea. Ufaransa $42,900 UK : $ 41,100 Kenya: $1,500.... Hapa Tanzania $ 980 kwa mwaka! (au dola 12 kwa mwezi badala ya siku moja)!
Maendeleo mengine yanapimwa kwa idadi ya watu waliosoma (vizuri), Idadi ya watu wanaohudumiawa na daktari mmoja nk. Katika yote hayo, tuko nyuma mno----twaishi ishi tu.
Utasema: lakini maendeleo kama hayo huchukua muda! Ni kweli. Ila narudia kichwa cha habari kwamba kutokana na vitu tulivyonavyo ingekuwa tuishavuka kwenye pato la dola 12 kwa mwezi, ingekuwa tuishafika kwenye pato la dola 12 kwa siku. Nchi nyingi zimefanya hivyo ambazo hazina tulivyonavyo.
 
Huu ndiyo uhalisi mkuu!Kuna watu wengi sana wana wabeza marais Mwinyi na Kikwete kwa kuwa kwao uchumi wa mtu mmoja mmoja siyo kigezo cha maendeleo ya nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaaaa...umeua mkuu
 
Agreed with you
 
Umesahau 1 muhimu. KATIBA BORA. Katiba iliyopo ni ya CCM chama Twawala.Bila kuwa na Katiba mpya tofauti na hii ya 1977 inayoibeba SerikalI ya CCM basi Maendeleo Tanzania ni sawa na ndoto za Alinacha.
 
Umeongea kishabiki bila hoja yoyote ya maana, umeshindwa kuunganisha doti kuhusiana na utawala wa ccm na umaskini wa watanzania ambao wamefikia hatua ya kuona fahari kwa kuwaita "Wanyonge". Poor you.
Achana nae, kwani humjui kuwa ni kada wa chama tawala humu jf?
 
Nakuelewa vizuri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…