Sababu za TPLB kusogeza mbele Mechi ya Simba na Azam kutoka Novemba 28, 2023 hadi Jan 1, 2024 hazijaniingia akilini

Sababu za TPLB kusogeza mbele Mechi ya Simba na Azam kutoka Novemba 28, 2023 hadi Jan 1, 2024 hazijaniingia akilini

Kama una stress..habarika na Gentamycine nawe utaponywa..siku itaenda vizuri.
 
acha nimpe maua yake huyu jamaa ni KING OF SPORTS habari zake ni za uhakika ukibisha we juha. [emoji23][emoji23]
Watu Wana wivu husuda tu, for me Genta namkubali ,mambo mengine Ni mapungufu madogo madogo tu
 
Sema jamaa unique sana habari zako huwa zinaibua fikra
Hiyo mechi imepelekwa mbali mno
 
Ila kwa wenye Akili Kubwa duniani (GENTAMYCINE na baadhi) tunajua kuwa Usimba ndani ya TFF (TPLB ikiwemo ndani yake) umechangia na kilichofanyika hapa ni Kuikoa Simba SC na Kipigo Kitakatifu kingine kutoka kwa Azam FC.

Hali ambayo inaweza kuzidisha Mgogoro Klabuni, Amani kutoweka ila Kubwa ni kutaka Kuibeba Simba SC kwa kumpa angalau muda kidogo Kocha Mkuu mpya ambaye huenda Siku Tatu hizi kuanzia leo Ijumaa hadi Jumapili akatangazwa aweze Kukijenga vyema Kikosi huku Viongozi nao wakiwekana sawa ili yanayoendelea yamalizike kabisa na Utulivu uanze Kutawala.

Sasa nyie Tanzania Premier League Board (TPLB) nami GENTAMYCINE (tena nikiwa ni Mshabiki Tukuka wa Simba SC) nawaambieni hapa hapa Jamiiforums kuwa hata kama baadhi yenu mnatumia Usimba wenu Kuiokoa na Kuibeba Simba SC isiendelee kupata Matokeo mabaya na Mgogoro Kuzidi ukweli ni kwamba hata kama hii Mechi ya Simba na Azam iliyokuwa ipigwe tarehe 28 Novemba, 2023 mmeipeleka mbele hadi tarehe 1 January, 2024 bado nawahakikishia kwa Mapungufu makubwa yaliyoko katika Uongozi, Benchi la Ufundi na kwa Wachezaji wa (Kikosi cha) Simba SC bado tu Siku hiyo Simba SC itafungwa vile vile na Matatizo kuendelea.
Itakuwa bodi ya Ligi wamegundua Azam nao wataihujumu Tena,kwa kuwatumia akina kapombe, Chama,Manula nk.maana ule ushindi wa kununua na namungo amepita mulemule
 
Uliona Simba Sc atafungwa goli ngapi kwenye hiyo mechi na Azam?
 
Simba asipokong'otwa na Azam, atakong'otwa kimataifa...

Timu wameiparaganya viongozi wenyewe
 
Ndio mechi itolewe November hadi January? ili timu ifanye usajiri ?[emoji2772][emoji2772]
Wewe ulitaka itolewe November ipelekwe wapi? March!

Timu ya taifa sasa hivi iko kambini, watoke huko wajikusanye waanze game za CAF, ni ujinga kuamini Simba Sc inawaogopa Azam zaidi ya wapinzani wa CAF.
 
acha nimpe maua yake huyu jamaa ni KING OF SPORTS habari zake ni za uhakika ukibisha we juha. [emoji23][emoji23]
Sio zote!

Ila Iko stori moja ya msemaji wa Yanga Ali alimponda sana huku watu hatujui kitu chochote baadae heee tukashangaa dogo ndo huyo huyo amekuwa semaji lenye barka Yanga! Sijui alizipataje za ndani kuwa Ali yumo anagombea!
 
Back
Top Bottom