Sababu za Wanaume kutonufaika na ndoa

Sababu za Wanaume kutonufaika na ndoa

Wanaume hawanufaiki na ndoa!!!
1. Ana miaka 72.
2. Amestaafu kutoka katika huduma ya kazi.
3. Amejitolea maisha yake yote kuwalea watoto wake.
4. Amekataa starehe za maisha ili kugharamia ada ghali za shule na gharama za maisha ya watoto wake nje ya nchi.
5. Sasa wanaishi vizuri Ulaya, ama jijini Dar, Mwanza au Arusha
6. Mkewe, mwenye umri wa miaka 62, amehamia kuishi na watoto wao.
7. Yeye amebaki peke yake huko kijijini.
8. Watoto wake humpigia simu kidogo sana.
9. Anapaswa kuanza maisha upya kama mzalendo.
10. Anapambana na shinikizo la damu na magonjwa mengine yanayohusiana na uzee.
11. Atasurvive peke yake kwa muda gani zaidi?
12. Hii ndiyo hali halisi kwa wanaume wengi wa tabaka la kati: uzee wao mara nyingi ni wa upweke na, kwa visa vingi, huzuni.
13. Haijalishi jinsi mwanaume alivyo mzuri,aliyewajibika kwa familia yake, wanawake huonekana kuwapenda watoto wao zaidi ya waume zao. Kadri anavyozeeka, na waume zao kadri wanavyozeeka ndivyo inaonekana wana umuhimu mdogo kwao.
14. Kwa hivyo, wanaume wanufaikaje kweli na ndoa?
15. Wanatoa maisha mengi lakini wanapata kutambuliwa kidogo kwa kazi yao ngumu, huku mwanamke akionekana kuvuna faida zote.
Aliyeimba wanaume wameumbwa mateso kuhangaika huenda aliyaona haya pia .
Ukiwa kama mwanaume hali hii inaweza kuwa yako katika miongo michache ijayo.nini Unachofanya kuhusu hilo? Mpango wako wa kustaafu ni upi? Jali nafsi yako kama unavyojali familia yako. Jipende mwenyewe. Mungu akubariki.
 
So naweza kusema hiki kinachowatokea baadhi wanaume uzeeni ni come back au sio 😹

Yes Karma is debt and not favoritism

But we don't need to be judgmental because wanaume hasa sisi waswahili most of them we are not visionary , insightful and informative.

Tupo tunasafiri in different level of consciousness.

Kuna MTU anajitambua at 20s mwingine 30s na mwingine 40s na wengine hadi 50s ,60s

So unabidi kujua mwanaume wa kiswahili Mara nyingi huwa anaoa ili apate access ya ngono na sio kutengeneza familia bora .

Inapotekea akachoka ngono kwa mkeo anaanza kutafuta side chick Huku na huku. na mwisho anatelekeza familia yake

So tusiwahukumu ikiwa tunalijua tatizo lilipo.
 
Wanajizima data [emoji81][emoji81][emoji81]
Kuna mama mwanae kamuita Marekani kagoma kurudi tizii, mume analalamika watoto wamrudishie mkewe.!!
Ni kwenda tu ubalozi kumripoti kesho wanamleta unaenda kumpokea airport.
 
Baba yako na mama yako hawa ni watu muhimu ambao wamebeba hazina zako.


MTU yeyote anayemkataa na kumtelekeza mzazi wake anabidi kujua anapanda mbegu mbaya ambayo itamuangamiza yeye mwenyewe.


Wazazi ni kila kitu hapa duniani.
Nakubaliana na wewe lakini wakati mwingine sisi wababa tunafeli sana katika malezi,hatuna bond na watoto wetu,,,hii hupelekea watoto ukubwani kuwa mbali na wewe
 
Mie siamini kama mtu umeishi vizuri na mke, na watoto haujawahi kumuabuse mke mbele ya watoto.....from no where tu wakutenge hii kitu haipo.

Ujue kumtandika mke (mama wa watu, na wenyewe wanakuona) sio jambo jema na hawasahau hata ipite miaka na miaka.
Shida iliyopo kila analofanya mwanaume kama baba na kama mume huwa somehow linageuzwa kuwa abuse.

Watoto wakichapwa kwa makosa na utomvu wa nidhamu huwa inageuka abuse.

Mama akileta uzembe mfano kutotunza watoto vema, kuleta mazoea ya kindezi na wanaume nje ya ndoa, na kadhalika mume akiwa mkali na mkaksi then inaonekana ni abuse.

Mwanaume akiwa strict na maamuzi yake yenye faida kwa familia anaonekana mkoloni na dikteta hivyo ni abuser.

Kimsingi wanawake wa kisasa mna swaga za kuharibu sana mahusiano ya kifamilia kuliko kuyajenga. Ndio maana wanaume wa kisasa wakishapata mtoto ukimletea ugaigai anakuacha na watoto uendeshe familia wewe kama wewe sababu si unajua sana maisha na unaweza kila kitu hadi majukumu ya kiume. Wanakaa kando hajihusishi na chochote. Lea mwenyewe mtoto akishakua watakutana huko mtaani wataendelea walipoishia.

Story zote za chuki ulizomlisha mtoto baba anakuja kuzipangua kiulaini, na anampa mtoto ukweli wa mambo juu ya tabia na vituko vya mama vilivyosababisha yeye kusepa. Mtoto na baba wanaelewana wanaungana kukuchukia pamoja wanakutenga, unapata pressure na kisukari unaumwa unakufa, wanairudia nyumba ukiyojenga kwa shida kwa kuuza juice na matunda wanaiuza wanahamia kwenye nyumba ya babake life linaendelea kama haukuwapo vile. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ishini na wanaume vizuri haitawagharimu chochote.
 
Ndio hivyo tatizo wanajisahulisha, ila hata ingekuwa mimi nishafika kwa Biden nirudi nchi ya tozo kufanya nini??
Huyo mume atajiju si ahudumie mifugo [emoji81][emoji81][emoji81]
Utarudi tu utake usitake, kwenu kule, una ndugu zako kule, ujana tumalize pamoja halafu uzee niteseke pekee yangu wakati makubaliano ni hadi kifo kitudelete.
 
Haya mambo unaweza kuona kama ya kusadikika, lakini yanatokea sana. I know mzee mmoja (RIP), ambaye alivyostaafu akahamishia familia yake kijijini kwao, ambako alishajenga nyumba nzuri sana ya kustaafia. Mkewe alikaa muda mfupi, akatimkia Canada kwa binti yake.

Mzee alikaa, ikafika muda akaona cha kufia nini... akavuta dogodogo, akaanza maisha upya.

Cha muhimu mwanaume, tengeneza na future yako. Familia ikienda upande wake, ubaki na kitu cha kushikiria
 
Ukitaka hayo yakukute basi weka familia iwe kipaumbele

Tafuta muda wa kukaa na watoto, wakuzoee

Si umejinyima anasa ili ulipe ada? Jinyime na kwenda bar upate muda wa kwenda nyumbani

Jinyime na ile misifa eti 'mwanaume hakai nyumbani' ujaribu kushinda kwako jumapili

Usidhani kwamba kisa unafanya kazi sana unachoka sana basi una haki ya kuwa mkali kama mbogo watoto wakuogope
 
Hata umbebe Magoma na mdundiko km kifungashio tutakutana uzeeni, nitakapoenda kwa watoto wangu kula supu za firigisi wewe umebaki bush kufungulia kuku na kuhesabu jioni zikirudi [emoji81][emoji81][emoji81]
Huko unakwenda kutana na mkwe a.k.a mama wa familia. Nahakikisha napata namba yake. Figisu ntakaloleta ukikaa mwaka hapo ndani niite mbwa.

Hakuna mwanamke atakubali kukaa nyumba moja na mama mkwe hata awe mpole vipi. Mimi kila siku napiga simu namlilia mkwe wangu kipenzi aongee na mwanangu wamrejeshe mama yao kwenye mji wake maana ameshapumzika vya kutosha.

Kubabake ntakuharibia hadi urudishwe. Na kukuongezea balaa naaanza kupigia chapuo na ndugu za mke kuanzia baba, mama na mashemeji nao wapate haki ya kuja kwa ndugu yao kuishi. Kubabake lazima ubalaswe kama balale.
 
Back
Top Bottom