Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Hinduism na Budhism ni miongoni mwa Dini za kale sana zenye wafuasi wengi katika bara la Asia. Hinduism ndio Dini namba moja ya kale zaidi katika uso wa Dunia ikisemekana kuanzishwa miaka 1500 nyuma kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Hinduism ilianzia kwenye Nchi ya India na Nepal, na sasa ina wafuasi katika Nchi za Bangladesh, Indonesia, Pakistan, Sri Lanka, Mauritius, Fiji, Trinidad and Tobago, Guyana, Suriname, Malaysia na nchi zinginezo. Dini hii japokuwa ni ya kale lakini imeshindwa kumea wafuasi katika bara la Afrika, Ukaya, na huko Amerika. Hinduism ni moja kati ya Dini zenye kuingia vita na dini nyingine hasa uislamu, wakidai waislamu wanaoa dada zao kwa maksudi ya kuwasilimisha na kuwabadili dini hili wawe waislamu. Ukienda katika maeneo ya mipakani mwa India na nchi za kiarabu uwa inatokea vita kali na ubaguzi wa kidini zidi ya uislamu kwa sababu wanaamini waislamu wanalaghai ndugu zao hasa wa kike na kuwasilimisha au kuwabadilisha dini kwa mbinu za kilaghai kama kuwaahidi Ndoa au kupitia shida zao.
Tukija katika Budhism ni miongoni mwa dini za kale pia, ikidaiwa kuanzishwa miaka 600 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Mkuu wa Budhism uitwa Monk, na ni moja ya Dini zinazofundisha kujiami kwa mapigo mbalimbali ikiwemo mafunzo kama Kung Fu na Tai Chi. Budhism ina wafuasi katika nchi za Thailand, Japan, Myanmar (Burma), Sri Lanka, Cambodia, Vietnam, Laos, Korea Kusini, China, Taiwan na nchi nyinginezo.
Hinduism na Budhism ni dini zinazofanana katika misingi ya kiimani ikiwemo kufanya Meditation.
Licha ya Dini hizi kuwa na wafuasi wengi na maarufu Duniani lakini hazikufanikiwa kumea Afrika.
Sote tunaamini Ukristo na Uislamu ulienea Afrika kwa asilimia kubwa kupitia Ukoloni na Utumwa ambapo watumwa walifuata Dini za wakoloni kipindi hicho waarabu wakikamata watumwa na kuwauzia wazungu bila shaka hamtamsahau Sultan Sayyid Said wa Zanzibar aliyefanya kazi barabara kwa kukamata wafungwa kutokea bara na kuwapeleka Zanzibar kwa ajili ya kuwasambaza uarabuni, Amerika na Ulaya, wazungu nao wakichuuza watumwa kutokea kwa waarabu na kuwanunua, na wazungu wengine wakitumia mianya ya umishionari. Sasa mtumwa akiangukia katika utawala wa Masultani au Umwinyi basi lazima afuate dini ya Sultan ambayo ni uislamu, na ikitokea mtumwa akaanguka kwenye mikono ya wamishionari au wazungu basi lazima afuate dini ya mmishionari au mzungu ambayo ni Ukristo.
Kwa sababu Wachina, wahindi na watu wa mataifa ya Asia hawakushiriki katika Ukoloni wa Afrika ikawa ngumu kwa dini za Budhism na Hinduism kufika barani Afrika ukizingatia na umbali katika ya Asia na Afrika.
Uislamu na Ukristo zilienea kwa kiasi kikubwa kupitia biashara, uvumbuzi wa njia za baharini, na uenezaji wa falme za Kiislamu na za Kikristo. Hii ilisababisha kuenea kwa dini hizi kwa njia ya kibiashara na kijeshi kutoka Mashariki ya Kati na Ulaya. Hinduism na Budhism, kwa upande mwingine, hazikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na biashara na mawasiliano ya kimataifa na Afrika.
Ukristo na Uislamu zilisambazwa kwa kiasi kikubwa kupitia himaya za kikoloni za Ulaya na Waarabu. Waenezaji wa dini hizi walitumia nguvu ya kijeshi kama kutawala kwa nguvu na kulazimisha na ya kisiasa kueneza imani zao katika maeneo mapya, ikiwa ni pamoja na Afrika. Hinduism na Budhism hazikuwa na himaya kubwa za kikoloni kama hizi za kusambaza imani zao.
Uislamu na Ukristo zilikuwa na uwezo wa kuchanganya imani zao na tamaduni za wenyeji kwa kiwango fulani, ambacho kilisaidia katika kuwafanya waweze kuenea haraka zaidi katika maeneo mapya. Hinduism na Budhism, kwa upande mwingine, zilikuwa zinajikita sana katika tamaduni za Asia Kusini na Mashariki, na zilikuwa na muda mrefu wa utamaduni na mazoea ambayo hayakubadilishwa kwa urahisi.
Hinduism na Budhism zilijitokeza katika mazingira ya Asia Kusini na Mashariki, na zilikuwa zimeathiriwa sana na tamaduni za eneo hilo. Mazingira ya utamaduni na kihistoria ya Afrika ilikuwa tofauti sana na ilikuwa na dini zake za jadi na mifumo ya imani.
Wakati Hinduism na Budhism zilikuwa zinajitokeza, bara la Afrika lilikuwa limekwishaingiliwa na mifumo mingine ya dini kama vile Ukristo na Uislamu, ambazo zilikuwa na nguvu zaidi katika kusambaza na kueneza imani zao.
Dini hizo za ukristo na uislamu zilienea sana kiasi kwamba hazikutoa fursa kwa dini zingine kama Budhism na Hinduism kumea na kupata wafuasi.
Hata leo hii Muislamu akizaa watoto atataka wafuate misingi ya dini yake ya kiislamu. Vilevile mkristo akizaa mtoto atataka afuate misingi ya kiimani ya dini yake ya kikristo. Hii inanyima fursa kwa Dini nyingine kujipenyeza kwa sababu hata vizazi vya watu hawa vinakuwa vimeishaingia katika mfumo wa dini ya kikristo au kiislamu.
Dini za Afrika za asili zilipotea na kusahaulika gafla baada ya ukoloni kuingia Afrika. Inashangaza kuona leo hii Muafrika anambagua muafrika mwenzake kisa misingi ya kidini ambayo ililetwa kama njia ya Ukoloni.
NB: Endapo Wahindi na Wachina nao wangefanikiwa kututawala au kuingiza mifumo ya dini zao enzi za Ukoloni basi uenda leo hii Afrika ingekuwa na wafuasi wengi wa dini za kibudha au kihindu. Hata wewe Mgalatia au Mvaa kobazi ungekumbwa na wimbi la Dini za Budhism au Hinduism kama wachina au Wahindi wangefanikiwa kututawala. Na wewe hivi sasa ungekuwa busy kutetea Uhindu au Ubudha kama unavyotetea Ukristo au Uislamu