Sababu zilizopelekea Dini za Hinduism na Budhism kushindwa kumea Afrika

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Hinduism na Budhism ni miongoni mwa Dini za kale sana zenye wafuasi wengi katika bara la Asia. Hinduism ndio Dini namba moja ya kale zaidi katika uso wa Dunia ikisemekana kuanzishwa miaka 1500 nyuma kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Hinduism ilianzia kwenye Nchi ya India na Nepal, na sasa ina wafuasi katika Nchi za Bangladesh, Indonesia, Pakistan, Sri Lanka, Mauritius, Fiji, Trinidad and Tobago, Guyana, Suriname, Malaysia na nchi zinginezo. Dini hii japokuwa ni ya kale lakini imeshindwa kumea wafuasi katika bara la Afrika, Ukaya, na huko Amerika. Hinduism ni moja kati ya Dini zenye kuingia vita na dini nyingine hasa uislamu, wakidai waislamu wanaoa dada zao kwa maksudi ya kuwasilimisha na kuwabadili dini hili wawe waislamu. Ukienda katika maeneo ya mipakani mwa India na nchi za kiarabu uwa inatokea vita kali na ubaguzi wa kidini zidi ya uislamu kwa sababu wanaamini waislamu wanalaghai ndugu zao hasa wa kike na kuwasilimisha au kuwabadilisha dini kwa mbinu za kilaghai kama kuwaahidi Ndoa au kupitia shida zao.

Tukija katika Budhism ni miongoni mwa dini za kale pia, ikidaiwa kuanzishwa miaka 600 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Mkuu wa Budhism uitwa Monk, na ni moja ya Dini zinazofundisha kujiami kwa mapigo mbalimbali ikiwemo mafunzo kama Kung Fu na Tai Chi. Budhism ina wafuasi katika nchi za Thailand, Japan, Myanmar (Burma), Sri Lanka, Cambodia, Vietnam, Laos, Korea Kusini, China, Taiwan na nchi nyinginezo.

Hinduism na Budhism ni dini zinazofanana katika misingi ya kiimani ikiwemo kufanya Meditation.

Licha ya Dini hizi kuwa na wafuasi wengi na maarufu Duniani lakini hazikufanikiwa kumea Afrika.

Sote tunaamini Ukristo na Uislamu ulienea Afrika kwa asilimia kubwa kupitia Ukoloni na Utumwa ambapo watumwa walifuata Dini za wakoloni kipindi hicho waarabu wakikamata watumwa na kuwauzia wazungu bila shaka hamtamsahau Sultan Sayyid Said wa Zanzibar aliyefanya kazi barabara kwa kukamata wafungwa kutokea bara na kuwapeleka Zanzibar kwa ajili ya kuwasambaza uarabuni, Amerika na Ulaya, wazungu nao wakichuuza watumwa kutokea kwa waarabu na kuwanunua, na wazungu wengine wakitumia mianya ya umishionari. Sasa mtumwa akiangukia katika utawala wa Masultani au Umwinyi basi lazima afuate dini ya Sultan ambayo ni uislamu, na ikitokea mtumwa akaanguka kwenye mikono ya wamishionari au wazungu basi lazima afuate dini ya mmishionari au mzungu ambayo ni Ukristo.

Kwa sababu Wachina, wahindi na watu wa mataifa ya Asia hawakushiriki katika Ukoloni wa Afrika ikawa ngumu kwa dini za Budhism na Hinduism kufika barani Afrika ukizingatia na umbali katika ya Asia na Afrika.

Uislamu na Ukristo zilienea kwa kiasi kikubwa kupitia biashara, uvumbuzi wa njia za baharini, na uenezaji wa falme za Kiislamu na za Kikristo. Hii ilisababisha kuenea kwa dini hizi kwa njia ya kibiashara na kijeshi kutoka Mashariki ya Kati na Ulaya. Hinduism na Budhism, kwa upande mwingine, hazikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na biashara na mawasiliano ya kimataifa na Afrika.

Ukristo na Uislamu zilisambazwa kwa kiasi kikubwa kupitia himaya za kikoloni za Ulaya na Waarabu. Waenezaji wa dini hizi walitumia nguvu ya kijeshi kama kutawala kwa nguvu na kulazimisha na ya kisiasa kueneza imani zao katika maeneo mapya, ikiwa ni pamoja na Afrika. Hinduism na Budhism hazikuwa na himaya kubwa za kikoloni kama hizi za kusambaza imani zao.

Uislamu na Ukristo zilikuwa na uwezo wa kuchanganya imani zao na tamaduni za wenyeji kwa kiwango fulani, ambacho kilisaidia katika kuwafanya waweze kuenea haraka zaidi katika maeneo mapya. Hinduism na Budhism, kwa upande mwingine, zilikuwa zinajikita sana katika tamaduni za Asia Kusini na Mashariki, na zilikuwa na muda mrefu wa utamaduni na mazoea ambayo hayakubadilishwa kwa urahisi.

Hinduism na Budhism zilijitokeza katika mazingira ya Asia Kusini na Mashariki, na zilikuwa zimeathiriwa sana na tamaduni za eneo hilo. Mazingira ya utamaduni na kihistoria ya Afrika ilikuwa tofauti sana na ilikuwa na dini zake za jadi na mifumo ya imani.

Wakati Hinduism na Budhism zilikuwa zinajitokeza, bara la Afrika lilikuwa limekwishaingiliwa na mifumo mingine ya dini kama vile Ukristo na Uislamu, ambazo zilikuwa na nguvu zaidi katika kusambaza na kueneza imani zao.

Dini hizo za ukristo na uislamu zilienea sana kiasi kwamba hazikutoa fursa kwa dini zingine kama Budhism na Hinduism kumea na kupata wafuasi.

Hata leo hii Muislamu akizaa watoto atataka wafuate misingi ya dini yake ya kiislamu. Vilevile mkristo akizaa mtoto atataka afuate misingi ya kiimani ya dini yake ya kikristo. Hii inanyima fursa kwa Dini nyingine kujipenyeza kwa sababu hata vizazi vya watu hawa vinakuwa vimeishaingia katika mfumo wa dini ya kikristo au kiislamu.

Dini za Afrika za asili zilipotea na kusahaulika gafla baada ya ukoloni kuingia Afrika. Inashangaza kuona leo hii Muafrika anambagua muafrika mwenzake kisa misingi ya kidini ambayo ililetwa kama njia ya Ukoloni.

NB: Endapo Wahindi na Wachina nao wangefanikiwa kututawala au kuingiza mifumo ya dini zao enzi za Ukoloni basi uenda leo hii Afrika ingekuwa na wafuasi wengi wa dini za kibudha au kihindu. Hata wewe Mgalatia au Mvaa kobazi ungekumbwa na wimbi la Dini za Budhism au Hinduism kama wachina au Wahindi wangefanikiwa kututawala. Na wewe hivi sasa ungekuwa busy kutetea Uhindu au Ubudha kama unavyotetea Ukristo au Uislamu
 
Hapo kwenye vita kati ya hizo dhehebu na uislam kwamba wanaume wa kiislam wanarubuni binti za Hinduism kwa lengo la Ndoa nk, hawajakosea ndiyo ukweli.

Moja ya silence agenda ya Islamic religion ni kutapakaa duniani na kuwa wengi, mbinu wanazotumia ndiyo hizo kuwarubuni binti sayuni au binti yeyote asiye muslin na kuzaa naye watoto wengi iwezekanavyo na baadaye kumtosa.

Mbinu hii ni siri kati yao na inafanya kazi sana, binti wengi wanalia na kusaga meno kwa ahadi fake.
 
Bandiko lenye maarifa ndani yake.

SHUKURANI KWA ELIMU.

PambanaZaidi/CottonandMore
 
Nilishindwa kujiunga kwenye dini za wahindi kwasababu napenda kula mishkaki na kwao ng'ombe ndo mungu
Hapana ng`ombe sio Mungu wao waindi wahindu ni utamaduni wao kutokula ng`ombe na hichi wanachogomba na wahindi waislam wao ngombe wanaokula huku nguruwe wanampiga vita mhindu nguruwe anakula
 
Biblia ndio msingi wa kuanzishwa kwa Ukristo na Uislam

Biblia tunayoijua leo ilaanza kuandikwa wakati wa Wayahudi wanarudi kutoka Utumwani Babeli kipindi cha Kuhani Ezra.

Msingi wa kuandikwa Biblia ilikuwa ni kumpa binadamu matumaini licha ya mapito yake hatakama ni magumu kiasi gani.

Ukristo au Mafunzo ya Biblia humvuta mtu bila shuruti kwa sababu watunzi wake walijua hakuna dawa ya matatizo kuliko matumaini ya kesho iliyobora.

Ndio maana mataifa ya kiislam hayaruhusu Wakristo wafundishe kwa uhuru sababu ni hatari kwa dini yao, angalia watu ambao hujaa kwa Mwamposa na Wachungaji wa aina yake, ni wengi sana na wakutoka imani tofauti.

Au nenda kasikilize gospel za kisekula za akina Paul Clement, Walichupa, Godfrey Steven, Zovaro, etal.
 
Na dini zetu asilia zimeshindwa kujipenyeza ulaya, Mashariki ya kati, Asia , Marekani ya Kaskazini na kusini.

Dini zetu waafrika kidogo imeweza kujipenyeza Haiti na Brazil.

Nafikiri dini za asili za Afrika, uHindu, uBuddha, Taoism za Asia zinatambua kuwa hakuna haja ya kusashawishi wengine nje ya jamii zao kujiunga nazo.

Tofauti na Ukristo au Uislam ambazo zinafurukuta, zinalazimisha, kushawishi jamii zingine ziingie ukristo au uislam kwa ubabe, shuruti na ulazima kupitia ukoloni, utumwa na kwa njia ya vita vya upanga

Dini za asili za Afrika , Asia ya Karibu na Asia ya mashariki ya mbali zinafafana kwa kutambua kuwa jamii za dunia zipo tofauti na kuziheshimu utofauti pia hazina utamaduni wa kulazimisha aliye nje ya jamii zao kuingia ktk imani zao.

Huwezi kuona wahindu, Buddha, taoism yaani wahindi, wa Vietnam, waJapan, Wachina wakijenga mahekalu (temples) kwa utitiri nje ya jamii zao hata za jamii ya diaspora zao lakini angalia utitiri wa makanisa na misikiti inajengwa nje ya jamii kubwa za kikiristo au kids lamu kwa madhumuni ya kubatiza na kusilimisha waumini wapya walio nje ya jamii zao.

Huwezi kusikia kuwa kuna NGOs za kutoka China, Japan, India zimeanzishwa kufadhili ujenzi wa mahekalu lakini kuna NGOs nyingi kutoka Ulaya, Marekani ya Kaskazini zinazofadhili ujenzi wa makanisa pia NGOs za kutoka Arabuni zinafadhili ujenzi wa misikiti baada ya kupewa miradi mikubwa na serikali ya Tanzania lazima watumie upenyo huo wapenyeze ushawishi wa dini zao.
 
Hinduism na Budhism ni miongoni mwa Dini za kale sana zenye wafuasi wengi katika bara la Asia. Hinduism ndio Dini namba moja ya kale zaidi katika uso wa Dunia ikisemekana kuanzishwa miaka 1500 nyuma kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Hinduism ilianzia kwenye Nchi ya India na Nepal, na sasa ina wafuasi katika Nchi za Bangladesh, Indonesia, Pakistan, Sri Lanka, Mauritius, Fiji, Trinidad and Tobago, Guyana, Suriname, Malaysia na nchi zinginezo. Dini hii japokuwa ni ya kale lakini imeshindwa kumea wafuasi katika bara la Afrika, Ukaya, na huko Amerika. Hinduism ni moja kati ya Dini zenye kuingia vita na dini nyingine hasa uislamu, wakidai waislamu wanaoa dada zao kwa maksudi ya kuwasilimisha na kuwabadili dini hili wawe waislamu. Ukienda katika maeneo ya mipakani mwa India na nchi za kiarabu uwa inatokea vita kali na ubaguzi wa kidini zidi ya uislamu kwa sababu wanaamini waislamu wanalaghai ndugu zao hasa wa kike na kuwasilimisha au kuwabadilisha dini kwa mbinu za kilaghai kama kuwaahidi Ndoa au kupitia shida zao.

Tukija katika Budhism ni miongoni mwa dini za kale pia, ikidaiwa kuanzishwa miaka 600 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Mkuu wa Budhism uitwa Monk, na ni moja ya Dini zinazofundisha kujiami kwa mapigo mbalimbali ikiwemo mafunzo kama Kung Fu na Tai Chi. Budhism ina wafuasi katika nchi za Thailand, Japan, Myanmar (Burma), Sri Lanka, Cambodia, Vietnam, Laos, Korea Kusini, China, Taiwan na nchi nyinginezo.

Hinduism na Budhism ni dini zinazofanana katika misingi ya kiimani ikiwemo kufanya Meditation.

Licha ya Dini hizi kuwa na wafuasi wengi na maarufu Duniani lakini hazikufanikiwa kumea Afrika.

Sote tunaamini Ukristo na Uislamu ulienea Afrika kwa asilimia kubwa kupitia Ukoloni na Utumwa ambapo watumwa walifuata Dini za wakoloni kipindi hicho waarabu wakikamata watumwa na kuwauzia wazungu bila shaka hamtamsahau Sultan Sayyid Said wa Zanzibar aliyefanya kazi barabara kwa kukamata wafungwa kutokea bara na kuwapeleka Zanzibar kwa ajili ya kuwasambaza uarabuni, Amerika na Ulaya, wazungu nao wakichuuza watumwa kutokea kwa waarabu na kuwanunua, na wazungu wengine wakitumia mianya ya umishionari. Sasa mtumwa akiangukia katika utawala wa Masultani au Umwinyi basi lazima afuate dini ya Sultan ambayo ni uislamu, na ikitokea mtumwa akaanguka kwenye mikono ya wamishionari au wazungu basi lazima afuate dini ya mmishionari au mzungu ambayo ni Ukristo.

Kwa sababu Wachina, wahindi na watu wa mataifa ya Asia hawakushiriki katika Ukoloni wa Afrika ikawa ngumu kwa dini za Budhism na Hinduism kufika barani Afrika ukizingatia na umbali katika ya Asia na Afrika.

Uislamu na Ukristo zilienea kwa kiasi kikubwa kupitia biashara, uvumbuzi wa njia za baharini, na uenezaji wa falme za Kiislamu na za Kikristo. Hii ilisababisha kuenea kwa dini hizi kwa njia ya kibiashara na kijeshi kutoka Mashariki ya Kati na Ulaya. Hinduism na Budhism, kwa upande mwingine, hazikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na biashara na mawasiliano ya kimataifa na Afrika.

Ukristo na Uislamu zilisambazwa kwa kiasi kikubwa kupitia himaya za kikoloni za Ulaya na Waarabu. Waenezaji wa dini hizi walitumia nguvu ya kijeshi kama kutawala kwa nguvu na kulazimisha na ya kisiasa kueneza imani zao katika maeneo mapya, ikiwa ni pamoja na Afrika. Hinduism na Budhism hazikuwa na himaya kubwa za kikoloni kama hizi za kusambaza imani zao.

Uislamu na Ukristo zilikuwa na uwezo wa kuchanganya imani zao na tamaduni za wenyeji kwa kiwango fulani, ambacho kilisaidia katika kuwafanya waweze kuenea haraka zaidi katika maeneo mapya. Hinduism na Budhism, kwa upande mwingine, zilikuwa zinajikita sana katika tamaduni za Asia Kusini na Mashariki, na zilikuwa na muda mrefu wa utamaduni na mazoea ambayo hayakubadilishwa kwa urahisi.

Hinduism na Budhism zilijitokeza katika mazingira ya Asia Kusini na Mashariki, na zilikuwa zimeathiriwa sana na tamaduni za eneo hilo. Mazingira ya utamaduni na kihistoria ya Afrika ilikuwa tofauti sana na ilikuwa na dini zake za jadi na mifumo ya imani.

Wakati Hinduism na Budhism zilikuwa zinajitokeza, bara la Afrika lilikuwa limekwishaingiliwa na mifumo mingine ya dini kama vile Ukristo na Uislamu, ambazo zilikuwa na nguvu zaidi katika kusambaza na kueneza imani zao.

Dini hizo za ukristo na uislamu zilienea sana kiasi kwamba hazikutoa fursa kwa dini zingine kama Budhism na Hinduism kumea na kupata wafuasi.

Hata leo hii Muislamu akizaa watoto atataka wafuate misingi ya dini yake ya kiislamu. Vilevile mkristo akizaa mtoto atataka afuate misingi ya kiimani ya dini yake ya kikristo. Hii inanyima fursa kwa Dini nyingine kujipenyeza kwa sababu hata vizazi vya watu hawa vinakuwa vimeishaingia katika mfumo wa dini ya kikristo au kiislamu.

Dini za Afrika za asili zilipotea na kusahaulika gafla baada ya ukoloni kuingia Afrika. Inashangaza kuona leo hii Muafrika anambagua muafrika mwenzake kisa misingi ya kidini ambayo ililetwa kama njia ya Ukoloni.

NB: Endapo Wahindi na Wachina nao wangefanikiwa kututawala au kuingiza mifumo ya dini zao enzi za Ukoloni basi uenda leo hii Afrika ingekuwa na wafuasi wengi wa dini za kibudha au kihindu. Hata wewe Mgalatia au Mvaa kobazi ungekumbwa na wimbi la Dini za Budhism au Hinduism kama wachina au Wahindi wangefanikiwa kututawala. Na wewe hivi sasa ungekuwa busy kutetea Uhindu au Ubudha kama unavyotetea Ukristo au Uislamu
Sahihi ✅
 
Sababu hatukutawaliwa na Wahindi au Wachina ambao hizo ni Dini zao.
Ni Bora hata wangetutawala wao kwakuwa Dini zao ni za Amani.
Kutawaliwa na Mwarabu na kuleta Uislamu kumetupa madhira mengi sana.
Madhira ya Ugaidi.
Madhira ya kuchapwa viboko tukila hadharani Mwezi wa Mzee Ramadhani.
Na kudharauliwa
Ni jambo la kusikitisha sana sana.
Na kuitwa Makafiri na kuchukiwa bila sababu.
Tumeletewa Dini ya chuki kwa sisi tusio wa hiyo Dini.
 
Hizo ni dini zisizotafuta wafuasi pia,
 
Back
Top Bottom