EllySkyWilly
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 2,204
- 2,085
Habari ndugu zangu wana JamiiForums.
Katika uzi huu nitaelezea sababu zinazofanya Magufuli apendwe na watanzania wengi zaidi.
Mimi mwenyewe binafsi najikuta sana navutiwa na mwanasiasa mchapakazi Dkt Magufuli kama ilivyo kwa watanzania wengine hili hata wanasiasa wa vyama upinzani wanalijua na hata wanachama pia wa vyama vya upinzani wanalielewa vilivyo maana lipo wazi.
Sababu ni hizi hapa
1. Magufuli ni Rais wa Afrika, kila pembe ya dunia inamtazama huyu Rais wa namna ya tofauti katika bara hili. Ndiye Rais aliyebaki kuwa na misimamo chanya dhidi ya bara la Afrika katika kujipatia maendeleo ya kiuchumi. Anatamani bara la Afrika liwe kama ulaya.
2. Magufuli ni mchapakazi sio mvivu anajituma kufanya kazi. Amejitoa kwa udi na uvumba kuisimamia Tanzania sio kazi ndogo. Na ni watu wachache Sana duniani wenye uwezo kama huo.
3.Magufuli ana kipaji cha uongozi. Na hili limethibitishwa na jinsi anavyo weza kusimamia kila wizara inayo hitaji kusimamiwa. Hachoki anaendelea kubuni mbinu za kusimamia zaidi mpaka Tanzania iendelee.
4. Magufuli ni mzalendo na kila mtanzania anaamini Magufuli akikabidhiwa Tanzania basi Tanzania itakuwa imewekwa mahali salama salimini.
5. Magufuli ni mcha Mungu. Ni Rais na kiongozi mwenye hofu ya Mungu. Na anayo imani kubwa sana kuwa Mungu ndiye kila kitu katika maisha. Na muda wote analiombea taifa letu toka moyoni sio mdomoni tu.
6. Magufuli ameondoa rushwa na maadili mabovu kazini.
7. Magufuli amefanya makubwa sana amefufua makampuni yetu makubwa, amehimiza na kujenga viwanda mbalimbali Tanzania vidogo kwa vikubwa. Viwanda vya kila namna vimejengwa katika awamu ya tano kwenye kila wilaya.
8. Anajenga mradi mkubwa Afrika wa kufua umeme utakao chochea maendeleo makubwa ya viwanda kama Ulaya.
9. Anajenga reli ya kisasa itakayo chochea usafirishaji wa malighafi na watu vitu ambavyo vitachochea ukuaji mkubwa wa uchumi na biashara.
10. Amerudisha Elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu. Watoto wetu sasa wanasoma bure kwa kutumia pesa ya serikali ya awamu ya tano.
11. Kwenye serikali ya Magufuli hakuna utakatishaji wa pesa tena za serikali au taasisi.
12. Amebuni mbinu mpya za kukusanya mapato pamoja na kupokea fedha kwenye taasisi mbalimbali, kwenye halmashauri za wilaya na mikoa. Njia ambazo mtu hana uwezo tena wa kuiibia serikali.
13. Naomba niishie hapa mambo mengine yapo kwenye hizi audio.
Hizi audio zinazo sababu za nyongeza ambazo zinafanya watanzania wengi kumpenda na kumkubali Magufuli.
Mitano tena kwa Magufuli.