Uchaguzi 2020 Sababu zinazofanya Magufuli apendwe na Watanzania wengi

Uchaguzi 2020 Sababu zinazofanya Magufuli apendwe na Watanzania wengi

Ana mambo mengi ya kuchukiza ndio maana watu wanamkataa mchana kweupe soma hapa:
Steven Makigo ni Swahiba wa Rais John Pombe Magufuli... hawakukutana barabarani!! Hawa wamesoma pamoja Lake Secondary School.

Akiwa kama waziri wa ujenzi, mwaka 2012 JPM alimteua Steven Makigo kuwa Mjumbe wa TEMESA. TEMESA hii ni ile ile ambayo ilinunua boti kwa mabilioni ya pesa huku boti yenyewe ikiwa na speed sawa na mtumbwi!!

Ni boti ile ile ambayo, ili kuwakata watu midomo wasiijadili, JPM yule yule akaipeleka boti hiyo jeshini! Yaani, Jeshi linapewa boti yenyewe mwendo wa kinyonga!!!

REMEMBER: Zabuni ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato iliweka sharti kwamba Contractor LAZIMA awe ni wa Kanda ya Ziwa!!

Yaani "National Project" inaweka condition ya ku-eliminate Watanzania wengine!!!!

Tena hapa tukumbushane kwamba, hiyo ni aina moja wapo ya Grand Corruption! YES, I mean it... a type of the GRAND CORRUPTION ambayo kwa makusudi watu wanaweka baseless conditions only to eliminate other competitors in favor of their guy!!!

SO, Kuna atakayeshangaa tukisema Mradi wa ujenzi wa Chato International Airport uliletwa maalumu ili tenda apewe Mayanga Construction Ltd, and ONLY Mayanga?!

Halafu ngoja, nimekumbuka!!

Hivi mnakumbuka JPM enzi zake akiwa Waziri wa Ujenzi akaja na "Wakandarasi Wazalendo"?!

Hoja tamu kweli kweli ambayo mtu ukiitia doa utaonekana unapingana na mtu anayekusudia kuwainua Wakandarasi Wazalendo lakini ukweli ni kwamba hiyo ilikuwa ni janja janja nyingine ya kui-favor Mayanga Construction!!

Wakati Wizara ya Ujenzi chini ya Magu ilipokuwa na mpango wa kujenga Daraja la Mbutu, Magu alijua kabisa Mayanga hatakuwa na ubavu wa kushindana na kampuni za kigeni na ndipo likaja suala la Wakandarasi Wazalendo, na Mayanga Construction akala shavu akiwa na "wazalendo" wengine!!
 
Babu yenu hawezi mshinda Tundu Lissu, labda neccm imtangaze kibabe!
Hivi kuna mtanzania ambaye hatompigia kura Magufuli kweli. Mimi nipo tayari tucheze kamari nawewe mkuu. Tuweke ngapi ngapi
 
Hivi kuna mtanzania ambaye hatompigia kura Magufuli kweli. Mimi nipo tayari tucheze kamari nawewe mkuu. Tuweke ngapi ngapi

Magufuli hategemei kura bali anategemea madaraka yake kutangazwa mshindi. Mtu anayeamini kupata kura hana jazba, na wala hawezi kutishia wapiga kura ili wampigie yeye.
 
Ni kazi ngumu sana kuwaamuru watu wampende mtu asiye na upepo wa kupendwa...

Wana CCM wenyewe wanavumilia maana hawana pa kusemea!!
 
Magufuli hategemei kura bali anategemea madaraka yake kutangazwa mshindi. Mtu anayeamini kupata kura hana jazba, na wala hawezi kutishia wapiga kura ili wampigie yeye.
Magufuli ni mtu mmoja mwenye uwezo mkubwa sana kichwani mkuu. Mambo aliyo yafanya Magufuli kwenye awamu hii si ya kubeza hata kidogo.
Amefanya mambo makubwa na anastahili kuigwa na viongozi wengine
 
Huyu mwaka huu tunalalanae mbele ujinga hatutaki. Magufuli amesaidia sana kuwaamsha watanzania.
 
Ni kazi ngumu sana kuwaamuru watu wampende mtu asiye na upepo wa kupendwa...

Wana CCM wenyewe wanavumilia maana hawana pa kusemea!!
Mbona sisi tunampenda sasa. Magufuli anapiga kazi sana. Please mpe kura yako Magufuli. Hata kama ndio chuki ya vyama hapana kwakweli.
 
Tutamkataa Magufuli kupitia sanduku la kura tuone hiyo NEC kama itaweza kupambana na nguvu ya wananchi
 
Babu yenu hawezi mshinda Tundu Lissu, labda neccm imtangaze kibabe!
Hakuna cha kibabe Mambo yote yapo wazi Magufuli ndiye Rais tunaye mhitaji. Tunahitaji Treni za umeme, na umeme wa uhakika,
 
Tutamkataa magufuli kupitia sanduku la kura tuone hiyo NEC kama itaweza kupambana na nguvu ya wananchi
Wananchi ndio tumeamua tunamhitaji Magufuli. Tunahitaji Rais atakaye tuletea tren za umeme, ndege, atujengee miundombinu imara, na umeme wa uhakika,
 
Mtu anayedhalilisha Mama zetu na Shangazi zetu, anayedharau taasisi ya Urais na karibu kila kitu Nchini ambacho kinastahili kuheshimiwa na kuthaminiwa. Mtu kama huyu utasemaje anapendwa na Watanzania?
 
Tarehe 28/10 watanzania tusifanye makosa, tumpigie kura nyingi Rais Mzalendo JPM, Rais aliyefanya restructure kubwa katika sector mbalimbali, nchi yetu sasa inasonga mbele. JPM miaka mitano mingine
 
Magufuli ni mtu mmoja mwenye uwezo mkubwa sana kichwani mkuu. Mambo aliyo yafanya Magufuli kwenye awamu hii si ya kubeza hata kidogo.
Amefanya mambo makubwa na anastahili kuigwa na viongozi wengine

Hakuna anayebisha mtazamo wako kwake, sio kila mtu lazima amkubali kwa huo mtazamo wako. Hebu taja hayo mambo aliyoyafanya, ambayo kiongozi mwingine angeshindwa.
 
Magufuli ni mtu mmoja mwenye uwezo mkubwa sana kichwani mkuu. Mambo aliyo yafanya Magufuli kwenye awamu hii si ya kubeza hata kidogo.
Amefanya mambo makubwa na anastahili kuigwa na viongozi wengine
Magufuli ameua diplomasia na mataifa makubwa kama Kenya. Kwa sasa tunacheki upepo mwingine
 
Back
Top Bottom