Uchaguzi 2020 Sababu zinazofanya Magufuli apendwe na Watanzania wengi

Uchaguzi 2020 Sababu zinazofanya Magufuli apendwe na Watanzania wengi

Hakuna anayebisha mtazamo wako kwake, sio kila mtu lazima amkubali kwa huo mtazamo wako. Hebu taja hayo mambo aliyoyafanya, ambayo kiongozi mwingine angeshindwa.
Mfano tu alivyoshughulikia ishu ya Corona, vyeti fake, mishahara hewa n.k
 
Hakuna anayebisha mtazamo wako kwake, sio kila mtu lazima amkubali kwa huo mtazamo wako. Hebu taja hayo mambo aliyoyafanya, ambayo kiongozi mwingine angeshindwa.
Kaondoa rushwa yote. Karejesha maadili kazini, kayabana majizi na mafisadi. Kazuia upoteaji wa mapato, kajenga viwanda, Kathubu kwenye mradi mkubwa wa umeme, kathubutu kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma, Karudisha elimu bure, karudisha heshima kazini, kazuia uizi wa madini yetu.
 
Mfano tu alivyoshughulikia ishu ya Corona, vyeti fake, mishahara hewa n.k

Issue ya Corona alizuia taarifa, na hiyo Corona haukuwa ugonjwa hatari kwa hili eneo leo. Vyeti fake alivishughulikia kwa double standard, alipaswa aingie mpaka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, au kwakuwa madictator hutegemea vyombo vya dola kutawala ndio maana akawafumbua macho? Mishahara hewa ilianza kushughulikiwa toka enzi za JK, labda kwakuwa yeye alipoingia ndio alikuta utaratibu umeenza akatembeans mchakato.
 
Mapungufu yanayosemwa kuhusu Dk Magufuli ni ya kawaida kwa binadamu yoyote au kiongozi yoyote hawezi kuwa 100% lakini Ukweli ni exceptional President in Africa.

Wanatamani na wengine wapate Rais kama yeye. Na Kikubwa zaidi ana ujasiri wa kutenda makubwa ya kimaendeleo. Bravo Mr President
 
Mapungufu yanayosemwa kuhusu Dk Magufuli ni ya kawaida binadamu yoyote. Ukweli ni exceptional in Africa. Wanatamani na wengine wapate Rais kama yeye. Kikubwa ana ujasiri wa kutenda makubwa ya kimaendeleo. Bravo Mr President
Wengine kina nani na umewajuaje?
 
Watanzania wanakupenda Jiwe hata 200 hawafiki mkuu, na kwasasa anatembelea nyota za diamond, harmonize na kiba
 
Hakuna anayebisha mtazamo wako kwake, sio kila mtu lazima amkubali kwa huo mtazamo wako. Hebu taja hayo mambo aliyoyafanya, ambayo kiongozi mwingine angeshindwa.
Kwa hilo lazima tutofautiane, kama juhudi na kutenda kwa Magufuli kwa miaka hii mitano kukagezwa na marais wajao nchi itasonga mbele haraka.
 
Kaondoa rushwa yote. Karejesha maadili kazini, kayabana majizi na mafisadi. Kazuia upoteaji wa mapato, kajenga viwanda, Kathubu kwenye mradi mkubwa wa umeme, kathubutu kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma, Karudisha elimu bure, karudisha heshima kazini, kazuia uizi wa madini yetu.

Kazuia rushwa au vyombo vya habari haviko huru kutangaza habari za rushwa? Kabana majizi kisha yeye mwenyewe kaenda kupora korosho na fedha za watu kwenye bureau de change! Hakuna ufisadi wowote kapambana nao, zaidi ya kuwakomoa matajiri mahasimu wake kabla hajawahi rais. Niambie sakata la escrow mpaka leo kiongozi gani wa serikali yupo ndani? Kimsingi hapambani na ufisadi bali anapambana na matumizi ya neno fisadi.

Viwanda vilikuwa vinajengwa hata kabla hajawa rais, yeye alisema ataleta Tanzania ya viwanda huku akiagiza viwanda 100@mkoa, weka list ya viwanda 100 kila mkoa na sio karakana. Kwenye kampeni hizi umesikia akiongelea Tanzania ya viwanda? Ni kweli kathubutu kwenye mradi wa umeme wa maji ambao ni 2015mg.

Ni kwanini asingewekeza hizo hela kwenye umeme wa gas ambao tuliambiwa utatoa 10,000mg? Aliwahi kukupa maelezo ya kwanini umeme wa maji kwa hela zote hizo, na sio umeme wa gas ambao kwa hela hizo tungepata mg nyingi kuliko huo wa maji?

Kuhamia Dodoma ilikuwa ni wazo sahihi enzi za Nyerere, lakini kwa zama hizi ni kama kupoteza hela, kwani mambo mengi ya serikali yanafanyika kwa mitandao na sio kuonana face to face kama zamani.

Elimu bure kaiga cdm, tena wao waliahidi toka kindergarten mpaka chuo kikuu. Karudisha heshima kazini, lakini kuna impact ndogo ya hilo. Kazuia uizi wa madini, ila mikataba ni siri! Kama mikataba ni siri unajua kilichomo ndani ya mikataba? Hayo nimejibu unayomsifia nayo, sijaweka mapungufu yake hapa.
 
Issue ya Corona alizuia taarifa, na hiyo Corona haukuwa ugonjwa hatari kwa hili eneo leo
Wewe unafikiri kuzuia taarifa tu ndo ilisaidia? Magufuli alimtanguliza Mungu kwa taifa zima, akawasihi watanzania kuomba kwa siku 3. Mungu akatuepusha na hili janga kwa kiasi kikubwa.
 
Vyeti fake alivishughulikia kwa double standard, alipaswa aingie mpaka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, au kwakuwa madictator hutegemea vyombo vya dola
Mkuu tumia akili tu ya kawaida, umeshasema vyombo vya ulinzi na usalama, hivi unawezaje kutumbua vyeti fake? Na ikiwa kuna watu wameingia kwenye majeshi n.k kwa vipaji vyao tu. Lazima uzingatie usalama wa nchi.
 
Kwa hilo lazima tutofautiane, kama juhudi na kutenda kwa Magufuli kwa miaka hii mitano kukagezwa na marais wajao nchi itasonga mbele haraka.

Weka deni la taifa kwenye kipindi chake, linganisha na deni alilokuta la miaka 50+, kisha nipe return ya miradi aliyojenga kuendana na deni alilokopa. Sina hakika kama unajua terms za mikopo ya sasa na marejesho yake. Kama unamudu hoja hizo rejea.
 
Back
Top Bottom