Uchaguzi 2020 Sababu zinazofanya Magufuli apendwe na Watanzania wengi

Uchaguzi 2020 Sababu zinazofanya Magufuli apendwe na Watanzania wengi

Naomba nichukue fursa hii kujibu maswali yako kama ifuatavyo,

2. Hata marais wa miaka ya nyuma wanajua na wanamwamini Magufuli kwamba ni mchapakazi na hana mchezo katika kazi. Hivyo hiyo sababu inajibu swali lako unaloniuliza....
10: acha uwongo ninasomesha mdogo wangu juzi nimetoka kulipia ela ya ada na usajili wa mitihani kidato cha sita usionge usiyoyajua.
 
Hapo kwenye namba 10 napinga kabisa hakuna elimu ya bure, hivi mtoa post unajua maana ya neno bure basi waulize majiran zako watakumbia maana yake.
Kwani wewe unaelewaje hiyo point chief. Chief nadhani unakumbuka zamani akati tunasoma shule tulikuwa tunalipa ada na pesa ya tahadhari. Kwa shule za kataa tulikuwa tunalipa ada elfu 20 na tahadhari ilikuwa kama elfu 15 hivi.

Saivi hiyo michango haipo tena. Kwa shule za bweni tulikuwa tunalipia elfu 70 ada jumlisha na tahadhari ni kama 85 elfu hivi. Lakini saivi hiyo michango ilishaondolewa. Walimu wakuu wanaingiziwa pesa za kuendeshea shule kila mwezi
 
Mkuu kwa hali ya kawaida huwezi kutumbua jeshi, kama nilivyosema kwa sababu za kiusalama.

Tambua pia wapo wasomi wazuri mitaani ambao wana vyeti vizuri na taaruma nzuri lakini hawakupata nafasi kwa sababu ya watu waliokua na vyeti fake ambao wapo makazini.
Hii sio hoja
Alitakiwa awalipe mafao yao wale wote aliowatumbua kwa vyeti feki ndiyo ingekuwa ubinadamu.
 
Wananchi ndio tumeamua tunamhitaji Magufuli. Tunahitaji Rais atakaye tuletea tren za umeme, ndege, atujengee miundombinu imara, na umeme wa uhakika,
Tena waambie huku jf hamuwezi kuchagua Rais, atachaguliwa na wananchi walio wengi hasa wa vijijini. Ila huku jf TL amekuwa Rais, hongereni tukutane 28 October.
 
Naomba nichukue fursa hii kujibu maswali yako kama ifuatavyo,

2. Hata marais wa miaka ya nyuma wanajua na wanamwamini Magufuli kwamba ni mchapakazi na hana mchezo katika kazi. Hivyo hiyo sababu inajibu swali lako unaloniuliza.

4. Watanzania wanamchukulia Magufuli kama mzalendo kwasababu anaipenda Tanzania pamoja na watu wake na rasilimali zote zilizomo Tanzania. Magufuli anachukia watu wanaoibia Tanzania na wasioipenda Tanzania na anaiombea Tanzania kwa moyo wa dhati.

7. Kampuni zilizofufuliwa ni TTCL, ATCL n. k

8. Mradi wa umeme anayojenga Magufuli ndio utakaoondoa kabisa shida ya umeme Tanzania.

10. Elimu ni bure kabisa bila hata senti watoto wa ndugu zangu wote wanasoma bure kabisa. Wazazi wamebaki kuzaa tu kuhusu kusomesha waiachie serikali ya awamu ya tano na sita

Hizo ndege za ATCL zinapiga route ya wapi ,, hadi zinataftiwa route sijui kubeba samaki hasara tupu
 
Magufuli hategemei kura bali anategemea madaraka yake kutangazwa mshindi. Mtu anayeamini kupata kura hana jazba, na wala hawezi kutishia wapiga kura ili wampigie yeye.
unapoteza muda kumjibu hiyo hajielewi
 
Njaa itatawala pale ambapo mtashindwa kuwalipa wakulima wa korosho pesa zao,kuwalipa wakulima wa pamba pesa zao,mtashindwa kuongeza watumishi mishahara, mtashindwa kuweka mazingira mazuri ya ukuzaji wa sekta binafsi.
Endelea kusubiri, asipopita huyo unaetegemea akuboreshee maisha yako,kwenye uchaguzi huu. Endelea kulalamika humu kwenye majukwaa ya Jf, ukisubiria Miaka mitano mingine, ili Kama atapita akusaidie.
 
Hizo ndege za ATCL zinapiga route ya wapi ,, hadi zinataftiwa route sijui kubeba samaki hasara tupu
Sasa ndege zimeshanunuliwa, usipopanda wewe, tamutapanda hata sisi watu ambao uchumi wetu unaruhusu.
 
Hizo ndege za ATCL zinapiga route ya wapi ,, hadi zinataftiwa route sijui kubeba samaki hasara tupu
Kwanza ikumbukwe kwamba hizo ndege ndio zilikwenda kuchukua ndugu zetu na watanzania wenzetu waliokuwa wamekwama China na India katika kipindi cha Corona
 
Magufuli hategemei kura bali anategemea madaraka yake kutangazwa mshindi. Mtu anayeamini kupata kura hana jazba, na wala hawezi kutishia wapiga kura ili wampigie yeye.
Na wala hawezi kugawa na kuahidi vyeo wakati wa kampeni
 
Habari ndugu zangu wana JamiiForums.

Katika uzi huu nitaelezea sababu zinazofanya Magufuli apendwe na watanzania wengi zaidi.

Mimi mwenyewe binafsi najikuta sana navutiwa na mwanasiasa mchapakazi Dkt Magufuli kama ilivyo kwa watanzania wengine hili hata wanasiasa wa vyama upinzani wanalijua na hata wanachama pia wa vyama vya upinzani wanalielewa vilivyo maana lipo wazi.

Sababu ni hizi hapa
1. Magufuli ni Rais wa Afrika, kila pembe ya dunia inamtazama huyu Rais wa namna ya tofauti katika bara hili. Ndiye Rais aliyebaki kuwa na misimamo chanya dhidi ya bara la Afrika katika kujipatia maendeleo ya kiuchumi. Anatamani bara la Afrika liwe kama ulaya.

2. Magufuli ni mchapakazi sio mvivu anajituma kufanya kazi. Amejitoa kwa udi na uvumba kuisimamia Tanzania sio kazi ndogo. Na ni watu wachache Sana duniani wenye uwezo kama huo.

3.Magufuli ana kipaji cha uongozi. Na hili limethibitishwa na jinsi anavyo weza kusimamia kila wizara inayo hitaji kusimamiwa. Hachoki anaendelea kubuni mbinu za kusimamia zaidi mpaka Tanzania iendelee.

4. Magufuli ni mzalendo na kila mtanzania anaamini Magufuli akikabidhiwa Tanzania basi Tanzania itakuwa imewekwa mahali salama salimini.

5. Magufuli ni mcha Mungu. Ni Rais na kiongozi mwenye hofu ya Mungu. Na anayo imani kubwa sana kuwa Mungu ndiye kila kitu katika maisha. Na muda wote analiombea taifa letu toka moyoni sio mdomoni tu.

6. Magufuli ameondoa rushwa na maadili mabovu kazini.

7. Magufuli amefanya makubwa sana amefufua makampuni yetu makubwa, amehimiza na kujenga viwanda mbalimbali Tanzania vidogo kwa vikubwa. Viwanda vya kila namna vimejengwa katika awamu ya tano kwenye kila wilaya.

8. Anajenga mradi mkubwa Afrika wa kufua umeme utakao chochea maendeleo makubwa ya viwanda kama Ulaya.

9. Anajenga reli ya kisasa itakayo chochea usafirishaji wa malighafi na watu vitu ambavyo vitachochea ukuaji mkubwa wa uchumi na biashara.

10. Amerudisha Elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu. Watoto wetu sasa wanasoma bure kwa kutumia pesa ya serikali ya awamu ya tano.

11. Kwenye serikali ya Magufuli hakuna utakatishaji wa pesa tena za serikali au taasisi.

12. Amebuni mbinu mpya za kukusanya mapato pamoja na kupokea fedha kwenye taasisi mbalimbali, kwenye halmashauri za wilaya na mikoa. Njia ambazo mtu hana uwezo tena wa kuiibia serikali.

13. Naomba niishie hapa mambo mengine yapo kwenye hizi audio.

Hizi audio zinazo sababu za nyongeza ambazo zinafanya watanzania wengi kumpenda na kumkubali Magufuli.





Mitano tena kwa Magufuli.


Kakojoe ulale.
 
Ni kazi ngumu sana kuwaamuru watu wampende mtu asiye na upepo wa kupendwa...

Wana CCM wenyewe wanavumilia maana hawana pa kusemea!!
Sitaki kumwona wala kumsikia wala kumnusa nitatapika hadi nyongo. He is very repulsive ni wa kukwepwa kama mwenye ukoma.
 
Back
Top Bottom