Kuna wanawake wengi wa Afrika wanapenda mwanamme mbabe, mwenye maneno ya kibabekibabe, hususan akiwa na madaraka.
Hawa wengi wana saikolojia na baiolojia ya kutaka kuwa na mtu mbabe anayeweza kuwatetea.Hiyo ni saikolojia ya muda mrefu, si kwa watu tu, bali hata wanyama wanayo.
Hivyo, kuna wanawake wengi wanampenda bila hata kujua hilo.
Wanaume wengine pia wana saikolojia ya kumkubali "Alpha male in the pack".
Washajua usipomkubali unaweza kupigwa risasi ukajeruhiwa au kuuawa.
Tabia hii si kwa watu tu, hata nyani na sokwe wanayo.
Nyani mdogo anatakiwa kumkubali Alpha male wa eneo, ama kama hamkubali ahame eneo atafute eneo lake jipya.
Ndiyo maana utasikia "Magufuli babalao, kama hamtaki hameni nchi".
Hizi si sababu zote, na kuna wengi wanampenda kwa mengi.
Lakini nimewaangalia watu wengine, hususan watu masikini ambao utawala wa Magufuli haujawasaidia lolote binafsi, na bado wanamshabikia, nikagundua kuna watu wengi wanataka kuwa sehemu ya "timu ya ushindi" tu, wampigie jarambe "Magufuli babalao, Alpha Male.Tingatinga".
By the way hata Malecela alishaitwa Tingatinga, alivyoshikishwa adabu, na jina akanyang'anywa.
Hilo linaonesha jinsi gani kuna watu wanaopenda viongozi wababe nchini mwetu.