SABATO SABATO SABATO wanafunzi 8 wa teku wafukuzwa baada ya kukaidi kufanya mtihani jumamosi!

SABATO SABATO SABATO wanafunzi 8 wa teku wafukuzwa baada ya kukaidi kufanya mtihani jumamosi!

Status
Not open for further replies.
Haya mafungu hayaoneshi ushahidi wa Yesu kufanya kazi Kama kazi! Labda unisaidie maana sioni tendo la kazi hapo na majibu ya Yesu yako wazi na yanaeleweka!

Kweli we msabato mbishi sana! Unanikumbusha kaka yangu mmoja mtoto wa mama mkubwa aliyetoka kwenye dhehebu lake la tangu utotoni na kuingia usabato halafu kwa ubishi wa kisabato akalazimisha kumuoa mjane (mke wa marehemu mdogo wake) alikufa kwa UKIMWI huku akitusomea vifungu kibao vya biblia!! And you know what, hakumaliza hata mwaka akavuta box!
 
So jibu lako ni ndiyo?

Biblia inasema Sabato ni Agano la Mungu kati yake na Wana wa Israel TU. Ndio maana Injili ilipotufikia Mataifa hakukuwa na habari ya Sabato, kama ipo lete hapa.
 
Kila mara husemwa kuwa
“Mungu ndiye alianzisha sabato
katika shamba la Edeni” kwa sababu
ya uhusiano kati ya Sabato na
uumbaji katika Kutoka 20:11. ingawa
starehe ya Mungu siku ya Sabato
(Mwanzo 2:3) iliangazia sheria ya
Sabato iliyokua inakuja, hakuna
maelezo yoyote ya Bibilia juu ya
Sabato kwa watoto wa Israeli kabla
watoke Misri. Hakuna maandiko
katika Bibilia au dondoo lolote
linaloonyesha kuwa Adamu na Musa
waliitunza Sabato.
Neno la Mungu laiweka wazi kuwa
kuitunza Sabato ilikua ishara
maalumu kati ya Mungu na Waisraeli:
“Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli
watishika sabato, kuiangalia sana
hiyo sabato katika vizazi vyao vyote,
ni agano la milele. Ni ishara kati ya
mimi na wana wa Israeli milele;
kwani kwa siku sita BWANA alifanya
mbingu na nchi, akastarehe kwa siku
ya saba na kupumzika” (Kutoka 31:
16-16).
Katika Kumbukumbu La Torati 5,
Musa anazirudia amri kumi kwa kizazi
kingine cha Israeli. Hapa baada ya
kuamrisha jinsi ya kuitunza sabato
katika aya ya 12-14, Musa anatoa
sababu ya sabato ambayo sabato
ilipewa kwa taifa la Israeli: “Nawe
utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa
mtumwa katika nchi ya Misri, na
akuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa
huko kwa mkono wenye nguvu, na
mkono ulionyoshwa; kwa sababu
hiyo BWANA Mungu wako,
alikuamuru uishike
sabato” (Kumbukumbu La Torati
5:15).
Lengo la Mungu kupeana sabato kwa
Waisraeli haikuwa kukumbuka
uumbaji, bali waukumbuke utumwa
wa Wamisri na kule kuokolewa na
Bwana. Kumbuka yanayohitajika kwa
kuitunza sabato: mtu aliyewekwa
chini ya hiyo sheria hangeweza
kutoka kwa boma yake (Kutoka
16:29), hangewakisha moto (Kutoka
35:3), angeruhusu mtu yeyote
kufanya kazi (Kumbukumbu La Torati
5:14). Mtu mwenye angivunja shreria
ya sabato angeuwawa (Kutoka 31:15;
Hesabu 15:32-35).
Uchunganusi wa ukurasa wa Agano
Jipya watuonyesha mambo mane
muimu: 1) Popote Kristo alionekena
baada ya kufufuka kwake na siku
zimetajwa, kila wakati ni siku ya
kwanza ya Juma (Mathayo 28:1,9, 10;
Mariko 16:9; Luka 24:1,13,15; Yohana
20:19, 26). 2) Wakati pekee sabato
imetajwa kutoka kwa kitabu cha
Matendo ya Mitume hadi ufunuo ni
kwa sababu ya lengo la uinjilisti kwa
Wayahudi kwenye Masinagogi
(Matendo Ya Mitume 13-18). Paulo
aliandika, “Nilikuwa kama Myahudi
kwa Wayahudi, ili niwapate
Wayahudi” (1 Wakorintho 9:20).
Paulo hakuenda kaitka Masinagogi
kuwa na ushirika na kuwajenga
waumini, bali alienda ili
awathibitishie injili na kuwaokoa
walikuwa wamepotea. 3) Mara moja
Paulo anasema, “tangu sasa
nitakwenda kwa watu wa
Mataifa” (Matendo Ya Mitume 18:6),
sabato tena haitajwi kamwe. Na 4)
Badala ya kupendekeza kuwa
waitunze siku ya sabato, sehemu
nyingine ya Agano Jipya iliyobaki
yasema kinyume ( ikijumulisha
sehemu ya tatu ilioachwa nche hapo
juu, inapatika katika Wakolosai 2:16).
Kwa kuingalia hoja ya nne kwa
makini, tutafumbua kwamba, hakuna
jukumu lolote la kuitunza sabato
kwa waumini wa Agano Jipya. Pia
tutaonyesha kuwa dhana ya Jumapili
“Sabato ya Wakristo” si ya kibibilia.
Vile imejadiliwa hapo juu, hakuna
wakati sabato imetajwa baada ya
Paulo kuanza kuangazia Mataifa,

Nimesoma maelezo yako umezungumzia Mambo mengi! Nikuulize swali kidogo! Wewe Si muisrael kiroho? Kweli sabato kwa Mara ya kwanza imetajwa Edeni bustanini. Na pia ikaja kwenye Kutoka20:11. Vipi kuhusu kitabu cha ufunuo 14:12.? Maana hapo tena sheria imetajwa na Kwayo ndo sabato IMO? Here is the patience of the Saints; here are those who keep commandments of God and faith of Jesus. Revelation 14:12. Kwahiyo Sio lazima sabato itajwe kwenye vifungu!
 
hii imekaaje wakuu, katiba iliyopo inazungumziaje issue hii!
Katiba haiwezi kuu-adress ujinga wa namna hii. Serikali ni secular haipaswi kujihusisha na masuala ya imani za watu binafsi ila ina uwezo wa kuingilia kati itakapobaini udanganyifu au mwenendo katika makundi wenye mwelekeo wa kuiletea madhara jamii.
Inashangaza jinsi baadhi ya watu wanavyoweza kuwashawishi hata wasomi wenye elimu kufuata mtindo fulani wa maisha hata kama ni dhahiri mbele kutakuwa na madhara!
Binafsi nilishuhudia mtoto aliyeokolewa na polisi baada ya wazazi wake kukataa katakata asiongezewe damu! Mtoto yule aliyekuwa na umri wa miaka saba alipelekwa Hospitalini akiwa na Hb 5g/dl ambapo wazazi walikataa asiongezewe damu hata baada ya kubembelezwa wiki nzima huku Hb ikiendelea kushuka hadi gramu 3! Ndipo Daktari Mkuu wa Hospitali ile alipotumia busara ya kuwasiliana na mkuu wa kituo cha Polisi kilichokuwa karibu. Kwa bahati nzuri Mkuu wa kituo alilielewa tatizo na kuamuru wazazi wazuiwe, mtoto apate damu. Mtoto yule alitoka Hospitali siku mbili baada ya kuongezewa damu huku wazazi wakiwa wamenuna lakini mtoto alipata ujasiri wa kuwaambia wauguzi "asante kwa kuyaokoa maisha yangu" jambo lilolofanya hata baadhi ya wagonjwa na wauguzi kibubujikwa machozi ya furaha.
Baadae niliambiwa wazazi wale walikuwa wafuasi wa dhehebu la Mashahidi wa Jehova!
La muhimu Katiba mpya itamke wazi juu ya ulinzi wa waathirika wa ghiliba za watu wa namna hii. Tazama masikini wanafunzi wale waliipoteza fursa ya kufanya mitihani kwa ghiliba za kiimani zinazosimamiwa na 'wasomi'.
 
Nimesoma maelezo yako umezungumzia Mambo mengi! Nikuulize swali kidogo! Wewe Si muisrael kiroho? Kweli sabato kwa Mara ya kwanza imetajwa Edeni bustanini. Na pia ikaja kwenye Kutoka20:11. Vipi kuhusu kitabu cha ufunuo 14:12.? Maana hapo tena sheria imetajwa na Kwayo ndo sabato IMO? Here is the patience of the Saints; here are those who keep commandments of God and faith of Jesus. Revelation 14:12. Kwahiyo Sio lazima sabato itajwe kwenye vifungu!

Ndio, mi ni Muisrael wa Kiroho.
 
Taratibu naona unaanza kulainika...Thanks to the Holy Ghost maana anaanza kutenda kazi yake..

Umeanza kua na busara! Niache Aleyn wangu tunajadili neno! Na Kama wwe unapenda karibu! Ila lugha chafu dhihaka so nzuri! Aleyn anajadili vizuri!
 
Ndio, mi ni Muisrael wa Kiroho.

Sasa Kama ni Muisrael wa kiroho pitia mafungu ya Yesu alozungumzia juu ya sabato, sheria n.k. Ebu soma Kama uko na biblia matayo15:9 Na Luka6:46.
 
Biblia inasema Sabato ni Agano la Mungu kati yake na Wana wa Israel TU. Ndio maana Injili ilipotufikia Mataifa hakukuwa na habari ya Sabato, kama ipo lete hapa.

Mbona tena unasema wewe ni Muisrael kiroho!? Kwahiyo wewe katika hili agano haupo?
 
Kweli we msabato mbishi sana! Unanikumbusha kaka yangu mmoja mtoto wa mama mkubwa aliyetoka kwenye dhehebu lake la tangu utotoni na kuingia usabato halafu kwa ubishi wa kisabato akalazimisha kumuoa mjane (mke wa marehemu mdogo wake) alikufa kwa UKIMWI huku akitusomea vifungu kibao vya biblia!! And you know what, hakumaliza hata mwaka akavuta box!

Mossadi hili tumeshaliweka sawa na Aleyn na limeeleweka! Pitia basi post zangu hapo nyuma utaona usawa! Kuongea sana hakusaiidi kitu!
 
Sasa Kama ni Muisrael wa kiroho pitia mafungu ya Yesu alozungumzia juu ya sabato, sheria n.k. Ebu soma Kama uko na biblia matayo15:9 Na Luka6:46.

Mkuu Sheria kwa matendo ya mwili na si Roho. Kumbuka kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa roho ni Roho 'Yohana 3:6_7'. Ndio maana tukibatizwa tunapokea Nguvu ya R/Mtakatifu na yeye ndie kiongozi wetu, na tukiongozwa Roho Mtakatifu HATUONGOZWI tena na Sheria, Soma Yoeli 2:28'.
 
stupid wa kwanza ni wewe na akili zako finyu.

ha ha ha ha ha! once stupid always stupid! we ni stupid tu na lazima utakubali sheria zenu za kisabato zimepitwa na wakati! ndani ya usawa huu wa maisha na uchumi wa kubangaiza unawafundisha watu eti wasiwashe wala kupika na wasifanye kazi siku ya jmosi! what a nonsense! wale mawe!!?
 
Mkuu Sheria kwa matendo ya mwili na si Roho. Kumbuka kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa roho ni Roho 'Yohana 3:6_7'. Ndio maana tukibatizwa tunapokea Nguvu ya R/Mtakatifu na yeye ndie kiongozi wetu, na tukiongozwa Roho Mtakatifu HATUONGOZWI tena na Sheria, Soma Yoeli 2:28'.

Mkuu Haya mafungu unayoyasema unayasoma yote vizuri? Hiyo yohana 3 Yesu anamfundisha Yule farisayo Nikodemas juu ya ubatizo yani kuzaliwa upya! Na Si Kama unavosema wewe juu ya kuzaliwa kwa mwili na roho! Yaani ubatizo! Jaribu kusoma mafungu yote utaelewa! Jesus answered; most assuredly, I say to you, unless. One is born of water and spirit , he cannot enter the kindom of Gog!
 
ha ha ha ha ha! once stupid always stupid! we ni stupid tu na lazima utakubali sheria zenu za kisabato zimepitwa na wakati! ndani ya usawa huu wa maisha na uchumi wa kubangaiza unawafundisha watu eti wasiwashe wala kupika na wasifanye kazi siku ya jmosi! what a nonsense! wale mawe!!?

Maisha ni bora kuliko Mungu?
 
Mkuu Haya mafungu unayoyasema unayasoma yote vizuri? Hiyo yohana 3 Yesu anamfundisha Yule farisayo Nikodemas juu ya ubatizo yani kuzaliwa upya! Na Si Kama unavosema wewe juu ya kuzaliwa kwa mwili na roho! Yaani ubatizo! Jaribu kusoma mafungu yote utaelewa!

Nimekuwekea hapo kuhusu Ubatizo nilidhani kuwa kwa mbaaali unaweza ukaelewa kumbe bado. Ok, twende mbele. Yesu kabla hajafika Miaka 30 alikulia na kuifata Torati kama ilivyo, na alifanya kwasababu
1. Roho Mtakatifu hakushuka Rasmi kwake.
2. Wayahudi wasipate neno lolote lile la kumshtaki.
Alipobatizwa TU, ndipo kazi yake ilianza rasmi, kumbuka alipobatizwa Roho Mtakatifu alimshukia na Mungu alimdhihirisha hapo. Umejiuliza tofauti kuu ya Ubatizo wa Yohana na Yesu ni upi??? Ubatizo wa Yesu umetupatia Roho Mtakatifu ambae tunaongozwa na huyo, SI TORATI.
 
hii imekaaje wakuu, katiba iliyopo inazungumziaje issue hii!

...........
Huu unaitwa wendawazimy tu hakuna kIngIne ni ushamba na kukariri dini aisee....wafukuzwe tu vyuo vya uinjilist vipo Vingi!!!!!! YA MINGU MPE MUNGU VIVYO HIVYO YA KAISARI MPE HUYOHUYO KAUSARI.....
 
Ndugu,kwa hiyo ktk zile amri 10,hiyo 1 ya sabato ni useless kwa sasa?kama jibu ni ndio naomba unipe fungu linaloonesha kufutwa ka amri hiyo.Tuelimishane.

Ata Mimi nasubiri atupe Hilo fungu la ushahidi anielimishe!
 
wewe utakuwa unafikiri kwa kutumia makalio.acha kugeneralize mambo.
kama we ni mkristo kweli fungua kutoka 20:8 .Mwenyezi Mungu alijua kuna vilaza kama wewe ndio maana amri hii ikaanza na ikumbuke siku ya sabato na uitakase.siku sita fanya kaz utende mambo yako yote lakini siku ya saba ni sabato ya bwana Mungu wako.siku hiyo usifanye kazi yoyote,wewe ,wala mwana wako,.............(malizia).
sasa usilazimishe watu wote kuvunja amri ya MUNGU kwa makusudi.

uzuri wake wasabato nimekuwa nao kuanzia kwenye familia, shuleni, chuoni kazini, kwenye biashara na katika maisha ya kawaida hivyo hunishangazi! wengi wa wasabato ni kama wewe!: WANAFIKI SANA! mnaamini mcha mungu ni anayesali jmosi tu!! dhambi zingine kama dhuruma, uongo, uzinzi kwenu siyo issue!! nilikuwa na classmates wangu pale MIST wao usiwambie kuingia darasani kabisa siku ya jmosi lakini walikuwa wanaishia kwa hawara zao mitaa ya nzovwe, forest, kanisani kwao mabatini na isanga the same huku makazini! So kwa hili usinidanganye kwa kunisomea vifungu vya biblia!!
 
Cjawai ona watu wenye misimamo ya kijinga kama wa sda.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom