Kila mara husemwa kuwa
Mungu ndiye alianzisha sabato
katika shamba la Edeni kwa sababu
ya uhusiano kati ya Sabato na
uumbaji katika Kutoka 20:11. ingawa
starehe ya Mungu siku ya Sabato
(Mwanzo 2:3) iliangazia sheria ya
Sabato iliyokua inakuja, hakuna
maelezo yoyote ya Bibilia juu ya
Sabato kwa watoto wa Israeli kabla
watoke Misri. Hakuna maandiko
katika Bibilia au dondoo lolote
linaloonyesha kuwa Adamu na Musa
waliitunza Sabato.
Neno la Mungu laiweka wazi kuwa
kuitunza Sabato ilikua ishara
maalumu kati ya Mungu na Waisraeli:
Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli
watishika sabato, kuiangalia sana
hiyo sabato katika vizazi vyao vyote,
ni agano la milele. Ni ishara kati ya
mimi na wana wa Israeli milele;
kwani kwa siku sita BWANA alifanya
mbingu na nchi, akastarehe kwa siku
ya saba na kupumzika (Kutoka 31:
16-16).
Katika Kumbukumbu La Torati 5,
Musa anazirudia amri kumi kwa kizazi
kingine cha Israeli. Hapa baada ya
kuamrisha jinsi ya kuitunza sabato
katika aya ya 12-14, Musa anatoa
sababu ya sabato ambayo sabato
ilipewa kwa taifa la Israeli: Nawe
utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa
mtumwa katika nchi ya Misri, na
akuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa
huko kwa mkono wenye nguvu, na
mkono ulionyoshwa; kwa sababu
hiyo BWANA Mungu wako,
alikuamuru uishike
sabato (Kumbukumbu La Torati
5:15).
Lengo la Mungu kupeana sabato kwa
Waisraeli haikuwa kukumbuka
uumbaji, bali waukumbuke utumwa
wa Wamisri na kule kuokolewa na
Bwana. Kumbuka yanayohitajika kwa
kuitunza sabato: mtu aliyewekwa
chini ya hiyo sheria hangeweza
kutoka kwa boma yake (Kutoka
16:29), hangewakisha moto (Kutoka
35:3), angeruhusu mtu yeyote
kufanya kazi (Kumbukumbu La Torati
5:14). Mtu mwenye angivunja shreria
ya sabato angeuwawa (Kutoka 31:15;
Hesabu 15:32-35).
Uchunganusi wa ukurasa wa Agano
Jipya watuonyesha mambo mane
muimu: 1) Popote Kristo alionekena
baada ya kufufuka kwake na siku
zimetajwa, kila wakati ni siku ya
kwanza ya Juma (Mathayo 28:1,9, 10;
Mariko 16:9; Luka 24:1,13,15; Yohana
20:19, 26). 2) Wakati pekee sabato
imetajwa kutoka kwa kitabu cha
Matendo ya Mitume hadi ufunuo ni
kwa sababu ya lengo la uinjilisti kwa
Wayahudi kwenye Masinagogi
(Matendo Ya Mitume 13-18). Paulo
aliandika, Nilikuwa kama Myahudi
kwa Wayahudi, ili niwapate
Wayahudi (1 Wakorintho 9:20).
Paulo hakuenda kaitka Masinagogi
kuwa na ushirika na kuwajenga
waumini, bali alienda ili
awathibitishie injili na kuwaokoa
walikuwa wamepotea. 3) Mara moja
Paulo anasema, tangu sasa
nitakwenda kwa watu wa
Mataifa (Matendo Ya Mitume 18:6),
sabato tena haitajwi kamwe. Na 4)
Badala ya kupendekeza kuwa
waitunze siku ya sabato, sehemu
nyingine ya Agano Jipya iliyobaki
yasema kinyume ( ikijumulisha
sehemu ya tatu ilioachwa nche hapo
juu, inapatika katika Wakolosai 2:16).
Kwa kuingalia hoja ya nne kwa
makini, tutafumbua kwamba, hakuna
jukumu lolote la kuitunza sabato
kwa waumini wa Agano Jipya. Pia
tutaonyesha kuwa dhana ya Jumapili
Sabato ya Wakristo si ya kibibilia.
Vile imejadiliwa hapo juu, hakuna
wakati sabato imetajwa baada ya
Paulo kuanza kuangazia Mataifa,