Sabaya afanyiwa upasuaji, kesi yaahirishwa

Sabaya afanyiwa upasuaji, kesi yaahirishwa

"General" nonsense.

Huo upasuaji wa kichwa alienda kufanyiwa kwa amri ya mahakama iliyotolewa lini? au inawezekana gerezani wakatoa ruhusa bila kuwasiliana na mahakama?
Kwani huo ugonjwa ulipata ruhusa ya mahakama kabla ya kumwingia Sabaya?
Kama mtu kutibiwa inabidi apate ruhusa ya mahakama, basi na ugonjwa nao inabidi upate ruhusa ya mahakama kabla ya kumpata mtuhumiwa.
 
Haka kamasai kalitaka kutikisa wachaga... woiiii amna rangi katacha ona mbe! Tena kakazingua wamachame bora warombo mzee wamachame nishida.
 
Kwani huo ugonjwa ulipata ruhusa ya mahakama kabla ya kumwingia Sabaya?
Kama mtu kutibiwa inabidi apate ruhusa ya mahakama, basi na ugonjwa nao inabidi upate ruhusa ya mahakama kabla ya kumpata mtuhumiwa.
🤣🤣🤣
 
Mawakili wa upande wa utetezi kesi namba mbili ya mwaka 2022, inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kuwa hali ya Sabaya ni mbaya baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa Julai 27 mwaka huu.

By Maryasumta Eusebi

Moshi.

Sabaya na wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka saba likiwamo la uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi wakati akiwa Mkuu wa wilaya hiyo.

Juni Mosi mwaka huu, Sabaya na wenzake wanne walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kusomewa mashtaka yanayowakabili mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey.

Hata hivyo Sabaya ambaye ni mshtakiwa namba moja katika kesi hiyo alifikishwa mahakamani hapo leo kichwa chake kikiwa kimeviringishwa bandeji huku mkononi akiwa na kifaa cha kuchomekea dripu.

Awali wakili wa Sabaya, Fridolin Bwemelo aliieleza mahakama hiyo kuwa Sabaya amefanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa kutokana na uvimbe aliokuwa nao na kwamba anahitaji kupata uangalizi wa karibu.

"Sabaya amefanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa na sio upasuaji mdogo hivyo anahitaji apate huduma muhimu na uangalizi wa karibu,"

Wakamtaka mwendesha mashtaka wa kesi hiyo kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo kwa kuwa walishaieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi umekamilika.

Wakili upande wa mashtaka Sabitina Mcharo aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi bado haujakamilika na kwamba wanasubiri kibali kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali cha kuipa uwezo mahakama hiyo kuendelea kuisikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo, Hakimu mkazi wa mahakama hiyo aliyekuwepo, Elibariki Philly aliahirisha kesi hiyo mpaka Agosti 12 mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi
Zidisheni dawa ya usingizi Ili afe, alikuwa malaika wa shetani jiwe.
 
Nimewahi kumuona mtu anapigwa hadi kichomwa Moto kwa tuhuma za wizi, Ila bahati mbaya wale warusha mawe na waliomchoma Moto wote hawajui ameiba nini Wala amemwibia nani, Ila wanachojua ni uaaaa mwiziiiii basi.

Nimekumbuka ghafra jinsi mkuu wa mkoa wa Mwanza alivyotukanwa na kukashfiwa baada ya kutumbuliwa, lakini ghafra anapongezwa sana baada ya kuteuliwa upya na watu walewale!!!!! Great thinkers!!!!!
 
Zidisheni dawa ya usingizi Ili afe, alikuwa malaika wa shetani jiwe.
Huyu hatakiwi kufa mapema. Tuna kawaida ya kusahau. Abaki tu... Ikiwapendeza wampe msamaha apate haki mahakama za serikali.
Nina imani mahakama za mitaani hatotoboa! Atapewa haki anayostahiki!
 
Back
Top Bottom