Strategically, mpango wa CCM chini John Pombe Magufuli akiwatumia viongozi wateule wake baadhi akiwemo huyu Sabaya pamoja na kutumia mifumo ya kiserikali, ilikuwa kumdhoofisha kiuchumi kabisa Mr Freeman Mbowe...
Walijua kabisa, kuwa, ukitaka kulisambaratisha kundi la kondoo (CHADEMA), basi anza kwa kumpiga mchungaji (M/Kiti wa chama - Mr. Mbowe) na kondoo wake wote (wanachama na wafuasi wa chama chake) wote watasambaa na chama kufa.....!!
Cheki mkakati wao;
1. Haribu vitega uchumi vyake vyote, Mfano;
å Jamaa wakaharibu shamba lake maua lenye uuwekezaji wa thamani ya zaidi ya Tshs. 500,000,000
SABABU: Analima kwenye chanzo cha maji kwa miaka zaidi ya 60 tangu kuanzishwa kwa shamba hilo..!!
å Waliifunga na kisha baadaye kulibomoa jengo alilokuwa analitumia kama Night Club [Club Bilicanas] kwa kuwekeza fedha nyingi na kutoa ajira kwa makumi ya watanzania....
SABABU: Eti halipii kodi ya pango la jengo hilo alilokuwa na ubia na NHC...!!
å Mwendazake kwa kuitumia TRA kisiasa, akaamuru kumbakizia kodi kubwa kwenye vitega uchumi vyake ktk biashara yake za hotel huko Moshi - Kilimanjaro...
SABABU: Eti alikuwa halipi kodi ya serikali kwenye biashara zake....!!
å Jamaa wakamfungia bank accounts zote za kwake binafsi na za makampuni yake ya kibiashara na kisha kukomba fedha zote eti ili serikali ipate mapato yake aliyokwepa...!!
LAKINI CHA AJABU;
¶ Pamoja na mikakati hii miovu ya kumdhoofisha huyu mwamba, jamaa hakuwahi ku - give up wa ku - surrender na kisha kujisalimisha CCM..!!!
¶ BADALA YAKE, kila aliyeshiriki ujinga na uhuni huu direct or inderect mmoja mmoja anatolewa relini na shina la uovu lenyewe (Mwendazake Magufuli) likakatwa na kutupwa na kisha kuchomwa moto. Sasa matawi yake (Sabaya, Makonda, Dotto James, Chalamil, Polepole, Bashiru, Ndugai nk ) moja baada ya jingine hayana pa kujishikiza, yananyauka na kujifia yenyewe...
Freeman Mbowe anaendelea ku restore kila kilichoharibiwa kimoja baada ya kingine. Na CHADEMA hao tena wanakuja kwa speed ya Nyambizi....!
2. Fungulia kesi za kisiasa za kutosha za makosa ya kubumba tu ili mradi sisi ni serikali, tutahakikisha anaozea jela mpaka aseme, jamani eeeeh, basi tuyamalizeni tu. Nipeni kadi ya CCM....!!