Shing Yui
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 15,168
- 38,049
Mwezi May mwaka jana, Freeman Mbowe alisafiri kutoka Moshi kwenda Dodoma. Alipofika Arusha gari yake ikapata hitilafu kidogo. Akapiga simu ikaletwa gari nyingine, na ile ya awali ikapelekwa garage hapo Arusha (naihifadhi jina kwa sasa). Mbowe akaenda zake Dodoma.
Kumbe Sabaya alikua Arusha kwa ajili ya weekend. Akapewa taarifa kuwa Mbowe kaacha gari garage. Akiwa na mabaunsa wake wakaenda garage hiyo na kukuta mafundi wawili na mlinzi. Hakukua na mafundi wengi maana ilikua jumapili, ambapo kwa kawaida sio siku ya kazi.
Akawataka mafundi hao wampe funguo ya gari la Mbowe. Wakasita na kuhoji anazitaka za nini? Wakapigwa kwa madai wanaizuia serikali kufanya kazi yake. Wakapekuliwa na kukutwa na funguo hizo, kipigo kikaongezeka. Wakafungwa mikono na miguu na kufungiwa chooni. Sabaya akafungua bonet na kutia chumvi kwenye Engine.
Wakakaa chooni bila msaada. Saa 10 jioni fundi wa garage jirani akaenda na kukuta geti liko wazi lakini hakuna mtu. Akaita lakini hakujibiwa. Akasikia migumo chooni, alipoenda akawakuta mafundi wawili na mlinzi akawapa msaada.
Wakaripoti tukio hilo kituo kikuu cha polisi Arusha. Wakapewa askari wa upelelezi. Siku chache baadae Askari huyo akakutana na Sabaya kwenye klabu ya usiku. Mabaunsa wake wakamshushia kipigo kikali, na kumuonya asijaribu kuingilia mambo asiyoyajua.
Tukio likawa gumzo mjini Arusha. Inadaiwa alitaka kulipiza kisasi lakini wakubwa zake wakamsihi awe mtulivu. Sabaya hakufanywa lolote kwa sababu alikua anatekeleza wajibu wake wa "kuua upinzani". Leo yupo jela, upinzani unazidi kustawi na waliomtuma hawajui kama yupo jela. Karma.!