Sabaya ataporudi uraiani kwa ushindi mkuu, Mbowe na wenzake watajisikia vipi?

Sabaya ataporudi uraiani kwa ushindi mkuu, Mbowe na wenzake watajisikia vipi?

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Visasi vya kisiasa mara nyingi huzaa malicious prosecution. Malicious prosecution huharibu maisha ya watu kwa kuvuruga maisha yao na hata nyadhifa zao.

Mpaka sasa inaonekana prosecution walitumika vibaya ili wamharibie maisha yake ya kisiasa Sabaya. Yote hii ni kumpa furaha mwanasiasa Mbowe.

Mpaka sasa prosecution wanahangaika kama mtoto mdogo aliyemsingizia mwenzake kuiba peremende ili siku ipishe.

Soon Sabaya anarudi uraiani huku Mbowe akipata aibu maana hakuna cha ziada alichovuna, ubunge wa Hai alishapoteza.

Wapi uliona Mwenyekiti wa usalama wa wilaya akachukua Ak 47 kwenda kupora sh laki tatu?
 
Kwani anashughulikiwa kwa sababu ya Mbowe?

Mimi tu kwa ile clip niliyomuona wamemvamia yule Mwarabu wa Arusha kihuni naunga mkono ashughulikiwe ipasavyo na akipatikana na hatia atumikie kifungo stahiki.
Clip ilionyeha wanavamia ili waibe simu na laki tatu? Hujui kuwa Mbowe anahusika?
 
Sabaya alikuwa analisha familia yaki? Naona njaa imeingia jikoni na mfukoni unaombea kesi iishe faster.
 
Clip ilionyeha wanavamia ili waibe simu na laki tatu? Hujui kuwa Mbowe anahusika?
Sabaya ameshitakiwa ARUSHA mjini.

Suala hilo linapaswa likufikirishe kujua uzito wa tuhuma zinazomkabili.

Je, Sabaya ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Arusha mjini?

Pia Sabaya anatuhumiwa kumteka na kumtesa diwani wa CCM, chama chake mwenyewe.
 
Visasi vya kisiasa mara nyingi huzaa malicious prosecution. Malicious prosecution huharibu maisha ya watu kwa kuvuruga maisha yao na hata nyadhifa zao...

Kwani huyo jamaa yako yuko mahakamani na gerezani kwa sababu ya Mbowe au kwa sababu ya dhambi na makosa yake mwenyewe...?? How is that supposed to be Mbowe's business?

Yaani kwa kuwa wewe unafikiri kijinga, basi unataka wote tufikiri kama wewe.

Pole na utaniwia radhi kwa kutumia lugha ngumu na kali kidogo. Lakini imenipasa nifanye hivyo ili akili yako iamke.
 
Una maana Mbowe ndiye alimuagiza Rais Samia amsimamishe kazi Sabaya ili achunguzwe kwa jinai alizotenda? Huyu Mbowe ni mtu mkubwa nchi kiasi anatoa maagizo kwa Rais na yanatekekelezwa.
 
Sabaya na CCM yake ni watu katili sana kupata kutokea Tanzania. Ukatili wa Sabaya na CCM yake ni mkubwa kiasi kwamba hata shetani anawashangaa. Uvumilivu wa Mbowe na Subira ni mkubwa mno kiasi cha kustahili kuishi na malaika.

Ndio huenda Sabaya asifungwe maana alikuwa anatekeleza maagizo ya CCM ya kupora , kuua, kubaka, kuteka watu na kukata masikio. Maana sina ushahidi kama Iddi Amini au Nguema, au Mobutu, au Hitler al8wahi wafunga wafuasi wake kwa ukatili.
 
Back
Top Bottom