Sadaka kumpa mzazi ni bora kuliko kuipeleka kwenye nyumba za ibada

Nimeupenda uzi wako ndugu ila soon nitakuja na somo zuri sana linalohusu sadaka na kanuni zake kwa mujibu wa Biblia Takatifu.
 
Usiwe na hasira; Tofautisha Sadaka na wajibu wa kawaida wa kuwasaidia wazazi wako kifedha

Yote unapaswa uyatekeleze kikamilifu
 
Kuna baraka za kumpa pesa mzazi na kutoa sadaka kanisani..

Malaki 3:10
Leteni zaka kamili nyumbani mwa Bwana...
1 Timotheo 5:8
Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
 
Somo la utoaji sadaka (Giving) ni pana sana, na watu wengi hawalielewi kiasi kwamba watoa sadaka zao bila kufuata misingi ya utoaji...Binafsi namshukuru Mungu amenipa neema ya kuweza kuelewa namna sahihi ya utoaji wa SADAKA.

Soon nitawaletea hilo somo. Mimi ni mgeni kwenye jukwa hili, ila nimefarijika sana ninavyoona wanajukwaa mnaposhirikishana habari zenye utukufu mbele ya Mungu.
 
WATU WENGI WANATOA SADAKA MAKANISANI NA MISIKITINI ILI WATU WAWAONE NA KUWASIFIA
 
Nyumbani kwa wazazi hupeleki Sadaka. Unapeleka Matumizi.

Sadaka ipelekwe Kanisani.

Pia saidia Maskini na wajane.

Fedha unayoipeleka Nyumbani/ kwa wazazi si alternative ya Sadaka.
Ila tukubaliane, sadaka ni ziada, haiwezekani Baba au Mama ana shida, alafu pesa upeleke msikitini au kanisani.

Matumizi unapeleka kwako, siyo kwa wazazi wako.
Sidhani kama kuna mtu anaeishi mbali na wazazi wake, hata kwenye mji mmoja ila nje ya nyumba ya wazazi wake, anaepeleka matuzi ya kila Siku, kama anavyopeleka kwenye nyumba anayoishi na mke wake pamoja na Watoto wake.

Unaweza usiwape chochote, mwenzi mzima na wasilalamike popote, ila fanya hivyo kwa mkeo uone, hivyo sadaka kuwapa wazazi wako ni halali kabisa.
 
Usiwe na hasira; Tofautisha Sadaka na wajibu wa kawaida wa kuwasaidia wazazi wako kifedha

Yote unapaswa uyatekeleze kikamilifu
Nani hasa muhitaji wa sadaka, yaani anaetakiwa kupewa, ila humu kuna wa imani tofauti.
 
Nani hasa muhitaji wa sadaka, yaani anaetakiwa kupewa, ila humu kuna wa imani tofauti.
Chagua moja usilalamike; kama hutaki kutoa sadaka usitoe tu, shida nini? Na usiende basi kanisani tuone😀
 
Samahani ijapokwa hii post ya mda kidgo ngoja na mimi niseme ..BINAFSI NIMEKUELEWA SANA TENA UMENIGUSA BINAFSI juzi kati nliwasiliana na mama yangu akaniambia Ana shida tena alikuwa Ana umwa nikajisemea hizi pesa nazo pelekaga sadaka si bora nikamtumia mama yangu .... kimandiko sijui ipoje kama ni dhambi nlicho kifanya na ntaendelea kufanya MUNGU atanisamehe kwakweli .... chchte ntakacho pata ntamtumia mama yangu ...wafia dini mtanisamehe.... hapa nimelenga hasa hasa xile sadaka 10% na za shukurani maana kuna watu wataniambia kama sitoi sadaka na kanisani nisiende sadaka ya ibada ntatoa cjakataa
 
Wazazi hawapewi sadaka ni jukumu lako mtoto (hasa wa kiume ila kama familia ina watoto wa kike pekee basi itawalazimu kuchukua hili jukumu) hii ni kulingana na mafunzo halisi ya kiislamu.

Sadaka toa kwa ndugu na wasiojiweza bila kuangalia dini, ila mzazi wako hapewi sadaka note that.
 
Kama kuna sadaka ulitaka kupeleka kanisani ahirisha mpe mama au baba.
Hiyo ndio tunaita sadaka kumpa mzazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…