Sadaka ya kujimaliza ya kwa Mwamposa inatia watu umasikini

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Juzi Bi. mkubwa wangu kanitembelea nyumbani, sasa yeye ni mmoja wa waumini wa kwa Mwamposa.

Baada ya salamu za hapa na pale akaomba awekewe channel ya Mwamposa aangalie ibada.

Wakati tukiangalia kulikuwa ni kipindi cha sadaka, kilichonishanga ni hii sadaka ya kujimaliza yaani toa chote ulichonacho ili ubarikiwe zaidi.

Nikamuuliza Bi mkubwa na wewe huwa unajimaliza? Akanijibu ndio kuna siku nilijimaliza nikakosa mpaka nauli nikachoka.
 
Juzi Bi mkubwa wangu kanitembelea nyumbani, sasa yeye ni mmoja wa waumini wa kwa Mwamposa.

Baada ya salamu za hapa na pale akaomba awekewe channel ya Mwamposa aangalie ibada.

Wakati tukiangalia kulikuwa ni kipindi cha sadaka, kilichonishanga ni hii sadaka ya kujimaliza yaani toa chote ulichonacho ili ubarikiwe zaidi.

Nikamuuliza Bi mkubwa na wewe uwa unajimaliza? Akanijibu ndio kuna siku nilijimaliza nikakosa mpaka nauli nikachoka.
Wajinga ndio waliwao
 
Watu wako brainwashed kabisa, huo ni ujinga unamtajirisha tapeli Mwamposa mchana kweupe kwa uvivu wa kufikiri.
 
Yani unaambiwa, ukijaribu kuwaelimisha...ni kama umeanzisha vita kuu ya tatu ya dunia. Bi Mkubwa mwenyewe alikuwa anatuma ma dola kwa T.B....saa hivi hilo liteni linavyompiga chenga, anakaaga kuuliza "hivi ni nini kimenipata?" (Yani na hapo, akipata tu, utaskia kachomoa sadaka ya shukrani)
 
Juzi Bi mkubwa wangu kanitembelea nyumbani, sasa yeye ni mmoja wa waumini wa kwa Mwamposa.

Baada ya salamu za hapa na pale akaomba awekewe channel ya Mwamposa aangalie ibada.

Wakati tukiangalia kulikuwa ni kipindi cha sadaka, kilichonishanga ni hii sadaka ya kujimaliza yaani toa chote ulichonacho ili ubarikiwe zaidi.

Nikamuuliza Bi mkubwa na wewe uwa unajimaliza? Akanijibu ndio kuna siku nilijimaliza nikakosa mpaka nauli nikachoka.
kuna mke wa mtu huko kigamboni dar es salaam alipewa ahifadhi milioni kumi 10 ya maendeleo, mwanamke akaenda kujimaliza na milioni 10 kwa mwamposa, mumewe alipoitaka pesa akaambiwa nimejimaliza baada ya siku tatu ntarudishiwa, jamaa akafura kama Mamba, akazama kwa mwamposa akapiga bonge la mkwara akarudishiwa pesa yake, ni habari very recent
 
Nilienda kwa Mwamposa miaka michache iliyopita nilikuwa A level sasa nilipofunga vibe lote la matukio nilikuwa naenda. Ulikuwa mwaka mpya ule mkesha tulikuwa wengi sana viwanjani pale. Watumishi wamevaa vifulana kama bodaboda muda wa sadaka wakaja na majaba ya wastani kama lita 30 hivi, ni makubwa kuliko ndoo. Wakawa wanapita tunatoa sadaka. Ila kabla ya sadaka inabidi muinyanyue juu kuibariki. Hapo kila mtu kanyanyua 5000, 2000, 10000 ikabidi nami nitoe 2000 ninyanyue. Tulitoa sadaka mara tatu hivi, ibada sikuimaliza niliondoka kama saa saba usiku maana niliingia saa tatu hivi. Uko nyuma sijui walitoa sadaka nyingine.

Nilioenda nao niliwaacha nikaja shtukia kumbe hela nilobaki nayo haitoshi nauli za usiku ule. Nilitembea mpaka saa kumi. Nikapata gari baadae ndani niliingia saa 11 alfajiri hata niliowaacha kule washalala.

Kule nilikutana na slay queens wa zamani, wadada waliowahi kujichubua, waliovaa kwa stara ila wana tattoo likely from their previous lifestyle, wavaa ushungi. Mambo ya uongo na kweli ya kutosha kule. Natamani nirudi nione kinachoendelea
 
Ila pale kwa Mwamposa kuna baadhi ya vitu havipo sawa. Kuna mzee alipata ajali Musoma akavunjika mguu. Ndugu yake akaamua kumleta Dar kwa matibabu zaidi. Alipofika huku akiwa katika matibabu ya hospitali (ikiwa anatumia magongo kutembelea) akasikia kuhusu Mwamposa.
Akaamua kwenda kuombewa huko.

Alipofika akaitwa mbele kwenye ibada maalum akaambiwa atupe magongo keshapona. Sasa sijui ilikuwa mzuka wa imani akaweza kutembea mpaka nje ya kanisa. Kufika kituo cha daladala kwa kuchechemea mguu ukamchachia hakuweza kutembea tena na pesa yote katoa sadaka ya kujimaliza. Ikabdi apigie simu ndugu waende kumchukua. Na mpaka kupona kwake ilibidi kutumia fimbo ya fagio maana magongo aliacha kanisani.
 
Juzi Bi mkubwa wangu kanitembelea nyumbani, sasa yeye ni mmoja wa waumini wa kwa Mwamposa.

Baada ya salamu za hapa na pale akaomba awekewe channel ya Mwamposa aangalie ibada.

Wakati tukiangalia kulikuwa ni kipindi cha sadaka, kilichonishanga ni hii sadaka ya kujimaliza yaani toa chote ulichonacho ili ubarikiwe zaidi.

Nikamuuliza Bi mkubwa na wewe uwa unajimaliza? Akanijibu ndio kuna siku nilijimaliza nikakosa mpaka nauli nikachoka.
Afya ya akili mkuu
 
Nje ya mada kidogo: Hivi ''bi mkubwa'' huwa ina maana gani? Ni uhusiano wa aina gani?
 
Back
Top Bottom